Pre GE2025 Askofu Bagonza: KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu, Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja

Pre GE2025 Askofu Bagonza: KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu, Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siku chache baada ya Askofu Dkt. Fredrick Shoo kueleza matamanio yake ya kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akipewa muhula wa pili wa uongozi wa Taifa letu baada ya muhula wake wa kwanza kumalizika, wadau mbalimbali wameibuka na hisia tofauti wapo wale walioonesha kumuunga mkono lakini pia wapo wale walioonesha kutokubaliana na hoja hiyo

Mmoja wa waliojitokeza na kuipinga hoja hiyo kwa ukali na uwazi ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe Askofu Dkt. Benson Bagonza ambaye amesema kilichozungumzwa na Askofu Dkt. Shoo si msimamo wa KKKT bali ni msimamo wake binafsi ambao pia pengine mipaka yake inapaswa kuishia kwenye Dayosisi yake pekee

"Nona KKKT imepamba moto kutokana na matamshi ya mmoja wa Maaskofu wake, kwa kimbelembele nilichonacho naomba umma wa Watanzania uelewe yafuatayo:-

(i) KKKT ina Mkuu mmoja tu (wa Kanisa ambaye ni Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa), dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja;

(ii) KKKT hakuna cheo kinaitwa 'Mkuu wa Kanisa mstaafu', tunaweza kuwa na cheo cha 'liyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa', hivi sasa tuna 'aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa' ambaye amechaguliwa tena kuwa Mkuu wa Kanisa, kama angekuwa mstaafu asingechaguliwa, inawezekana 'aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa' akachaguliwa kuwa Mkuu tena, sitashangaa aliyepita hivi karibuni kuchaguliwa tena;

(iii) Kama kuna mstaafu, 'astaafu', si lazima kuhudhuria; si lazima kusema, ukipenda, usipende kwa niaba, ukichukia, usichukie kwa niaba, kila ulimi una uwezo wa kuonja wenyewe;

(iv) KKKT ni shirikisho, siyo Kanisa moja, ukitaka kusema kwa niaba ya shirikisho, unashawishi siyo kuburuza, hatujashawishika na hatujakaa;

(v) Nampenda Rais Samia (Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) lakini sijatumwa na Kanisa, naweza kumpenda na kukikosoa chama chake (Chama cha Mapinduzi -CCM), naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye, hayo nitayasemea Karagwe siyo penginepo, na nikiyasema, ni yangu na tumbo langu siyo ya Wanyambo wala Walutheri walio wenye vyama vyao (yaani wanaotoka kwenye vyama tofauti vya siasa) kwa Nyambo haturuhusu mgeni kupiga mluzi katika nyumba ya mwenyeji;

(vi) Kanisa lina wanachama wa vyama vyote na waumini wasio na vyama, CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) msitutolee macho na CCM (Chama cha Mapinduzi) msishangilie, shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda unakatwa;

(vii) Rais Samia (Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ana uwezo wa kujiharibia, tusimharibie, CCM ina uwezo wa kujiharibia, haijaomba msaada wa kuisaidia kuharibu, lipo kundi linalodhani linamsaidia Rais Samia wakati linamharibia, lipo linalodhani linamharibia lakini linamjenga, anayesimama na 'haki' anamsaidia Rais Samia;

(viii) Tuna tatizo Kitaifa, kuna watu wanatumia Dini kueneza siasa, na kuna watu wanatumia siasa kueneza Dini, mimi si mmoja wa hao wawili (2), mimi natumia ujinga kueneza Dini na siasa, wajinga tu ndio wananisikiliza na kunifuata, wewe mjuaji kaa pembeni tuendelee na safari;

(ix) Nikisema jambo mkanishangilia, mnanipa kiburi cha kusema bila kufikiri, nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari, si kuhemka, mkishangilia, mnamnyima msemaji nidhamu ya kufikiri kabla ya kusema, anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana;

(x) Mungu analipenda Taifa hili (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) kuliko mtu au chama chochote kinavyoweza kudai kulipenda, usiombe Mungu akuonyeshe anavyolipenda hili Taifa, ina gharama nzito kushuhudia Mungu anavyolipenda hili Taifa, hata anayerudi nyuma ana mbele anakoelekea, ukisifiwa kuwa na mbio, jihadhari usipitilize nyumbani kwenu" -Askofu Dkt. Bagonza

Andiko la Askofu Dkt. Bagonza bila shaka huenda likaibua hisia mseto kama ilivyokuwa tamko la Askofu Dkt. Shoo kutokana na ukweli na kwamba watu hao wawili wana ushawishi wao binafsi lakini pia ushawishi wao ni ngumu kuutenganisha na Kanisa la KKKT
 
Nimeshawishika kulisoma Kwa ukamilifu andiko la baba askofu Dr Bagonza

Nilichokiona Kwa Uwezo wa roho Mtakatifu ni Kwamba Askofu Dr Bagonza ana mashaka huenda Ukuu wa KKKT ukawa unazunguka miongoni mwa Maaskofu Wawili tu Dr Malasusa na Dr Shoo

Ikumbukwe Askofu Dr Malasusa alishamaliza Mihula yake ya Ukuu wa KKKT lakini Katiba ukabadilishwa na sasa amerudi tena Kwa Katiba mpya

Naye Dr Shoo alishamaliza Mihula yake Kwa Katiba ilipita na ndio sababu Askofu Dr Bagonza amesema " Shoo hajastaafu anaweza kurudi" alimaliza muda wake Kwa Katiba Ile siyo hii

Andiko la baba askofu Dr Bagonza ni la Kiufundi sana

Mungu wa Mbinguni awafanyie Wepesi KKKT

Ahsanteni sana 😄
 
Malasusa ni chawa!
 
Saa mbovu kuna wakati pia inasoma sawa
 
Unadhani Watanzania wanapenda mabadiliko yoyote, chief? Ufahari wa Bongo ni kutunishiana misuli twitani, Insta, FB na kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Baada ya hapo, watu wanasalimiana kwa furaha, wenye kununa nao walee; tunalala halafu kesho yake inatukuta mzigoni tukiganga yaliyopo na yajayo.

Ndiyo maana haishangazi kuwakuta watu kiduchu kwenye mikutano, mijadala na maamuzi nyeti kabisa kitaifa.
Kweli kabisa Chief !
Ulichosema ndicho kinachofanyika !
 
Hili Kanisa tatizo lilianza pale walipoamua kujitenga na Kanisa mama la Roman Catholic, wakijitambua , kuacha ujeuri, kiburi na tamaa za pesa wanaweza kujirudi ndani ya Kanisa Mama la RC

Tumsifu Yesu Kristu.
Sababu 95 za Padri Martin Luther kuondoka Katoliki na kuanzisha kanisa zote ni za msingi sana, unataka nikutajie 5 za msingi?
 
Askofu Dr Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amesema Kwa sasa Taifa limefika Mahali pagumu sana sana

" Kuna watu wanatumia Dini Kueneza Siasa na kuna watu wanatumia Siasa Kueneza Dini Mimi natumia Ujinga Kueneza Dini na Siasa"

Source: Jambo TV

Aliyemuelewa baba askofu naomba Ufafanuzi tafadhali nisije kuchuma Dhambi Bure 🐼
Kasema hiviiii" KANISA MOJA TU TAKATIFU LA MITUME"
 
Back
Top Bottom