Askofu Bagonza: Kuna kila dalili serikali inahusika na watu kupotea, kutokana na kauli za viongozi wake

Askofu Bagonza: Kuna kila dalili serikali inahusika na watu kupotea, kutokana na kauli za viongozi wake

Sidhani kama amekosea, kupotea kwa Mdude lawama zilienda moja kwa moja kwa Mkuu wa mkoa,ushahidi wa tuhuma hizo haukuwepo. Chalamila kasimama hadharani na kutamka yale yale aliyo tuhumiwa nayo Mkuu wa mkoa mwingine dhidi ya Mdude, maana yake ametuweka wazi kuwa wana mamlaka ya kupoteza watu.
Tuwapongeze Chacha na Chalamila kwa kuufuta uvumi uliokuwepo siku nyingi.
Kusema unapoteza watu kama vile unapoteza kuku kirahisi ni baya sana hata kwa kizazi chake maana utawala una kikomo ila kizazi chake kinaendelea kuwepo.
 
Ukipoteza kwani hutapotea njia yetu ni moja tu Mungu ndo anajua , wakati unapoteza wenzio jua nawewe ndo unapotea siku za Mungu huhesabika pia.
 
-Hili nalo ni la kuongelewa?
-Kwa lengo lipi?

Niseme tu,wizara ya ulinzi iendelee kukazia katika michakato ya kupinga makundi na vikosi vya kujitegemea katika taifa letu,huku uraiani wapo watu hatari na mioyo yao imekuwa myeusi sana,wamesha kufa na kuishi kwa mara nyingine,wamepoteza,walionewa na wengine wamepewa sumu kali sana kwa yaliyotokea na yanayotokea.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kusema unapoteza watu kama vile unapoteza kuku kirahisi ni baya sana hata kwa kizazi chake maana utawala una kikomo ila kizazi chake kinaendelea kuwepo.
Tujilaumu sisi waswahili ubongo wetu unachelewa kutafakari jambo,kwa kauli ile maandamano yalitakiwa yaanzie pale pale kudai ndugu zetu ambao hawajulikani walipo,kwa sababu kuna watu wamepotea akiwa ni Mkuu wa mkoa.
 
Chalamila ni mtu hatari sana, na pia ana ttz la afya ya ubongo bilashaka,nitashangaa kama Rais hatompiga chini.
Samia anapenda wakorofi, wakatiri, wenye historia chafu dizaini ya Makonda utasikia kapewa uwaziri.
 
Ukipoteza kwani hutapotea njia yetu ni moja tu Mungu ndo anajua , wakati unapoteza wenzio jua nawewe ndo unapotea siku za Mungu huhesabika pia.
Kila kitu unamwachia Mungu,hapa duniani upo kufanya nini?
Pambana ili hata kama anakuja kukusaidia akukute jasho na damu imelowanisha ngozi yako
 
Sidhani kama amekosea, kupotea kwa Mdude lawama zilienda moja kwa moja kwa Mkuu wa mkoa,ushahidi wa tuhuma hizo haukuwepo. Chalamila kasimama hadharani na kutamka yale yale aliyo tuhumiwa nayo Mkuu wa mkoa mwingine dhidi ya Mdude, maana yake ametuweka wazi kuwa wana mamlaka ya kupoteza watu.
Tuwapongeze Chacha na Chalamila kwa kuufuta uvumi uliokuwepo siku nyingi.
Kweli hajasema kwa bahati mbaya alidhamiria kufikisha ujumbe kama Chacha.
 
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Askofu Bagonza amesema kuna kauli za viongozi zinatolewa kwa vitisho kuwachukulia hatua watu wasiokubaliana au kutoisikiliza Serikali.

Amesema, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, alisikika akiwaambia madereva kuwa asiyemsikiliza ahakikishe ameiaga familia yake.

Kuna kiongozi wa CCM alisikika akisema, wakiwapoteza wapinzani polisi isihangaike kuwatafuta.

Kauli kama hizi zinatia shaka kama kweli serikali haihusiki, amesema.

View attachment 3682196

Kauli ya Bagonza imekuja baada ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoa ufafanuzi kuwa video ya Chalamila iliyosikika ilikuwa imekatwakatwa.

Akihitimisha ujumbe wake, Askofu Bagonza amesema binafsi hapendi migomo vilevile hapendi kunyima watu haki ya kugoma, lakini pia hapendi ubabe.
ICC waanze humu,waturejeshee wote wasiojulikana walipo!
 
Alianza Pole pole, akafuata Nchimbi, Amefuata Cha-cha. Na sasa Chalamila.

Wanazidi kuonesha wazii.
 
Back
Top Bottom