PostGE2025 Askofu Bagonza: Kuna “vita” imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe Kalikawe Lwakalinda Bagonza kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook anasema;

WARAKA WA TEC: Kuna Watu Wanaiharibia Serikali.

Kuna “vita” imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini. Vita hiyo inaiumiza serikali kuliko walengwa wa vita hiyo. Nashauri tuiache serikali ijiharibie na uwezo huo inao. Tafakari haya yanayosemwa na watu wasiojisikiliza wakati wanaongea:

1. BANDARI: Kwa hiyo miaka yote TEC wanakwepa kodi, wanauza madawa ya kulevya na mambo mengine machafu, na serikali zooooote zilizopita ziliwaacha mpaka awamu hii ya sita?!

2. VURUGU ZA UCHAGUZI MKUU: Kwa hiyo TEC ndiyo iliyoharibu uchaguzi, ikaua watu, ikaharibu mali, ikazima internet nk?

3. MATAMKO YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI: Kwa hiyo SADC, AU, EU, State Department na Balozi zooote zilizosema uchaguzi ulikosa viwango, wote hao ni Wakatoliki au walishinikizwa na TEC?!

4. UTEKAJI: kwa hiyo, wakatoliki ndio walioagiza watu watekwe, wakampiga na Fr Kitima, wakateka mapadre na kuwadhalilisha au TEC hao hao wakafunga midomo ya viongozi kutokemea vitendo hivyo?

5. WASIOJULIKANA: Kwa hiyo hawa TEC ndio wasiojulikana ambao wanaogopwa na serikali kiasi cha kutofungua midomo kuwakemea?

6. MAANDAMANO: Kwa hiyo TEC ina nguvu ya kuwahamasisha vijana wa dini zote, vyama vyote, jinsia zote kuingia barabarani? Kwa hiyo TEC ina nguvu kuliko serikali na wazazi?

7. RUSHWA NA UFISADI: kwa hiyo TEC ndiyo inanyamazia ripoti za CAG, inagawa rushwa ndani na nje ya vyama wakati wa uchaguzi? TEC ndiyo inawalipa wanaotumia mitandao kuitukana serikali na sasa imewalipa ili waitukane TEC?

TEC ndiyo inayoagiza watu wale rushwa bila hofu ya TAKUKURU?

8. MAUAJI YA RWANDA: Kanisa Katoliki Rwanda lilihukumiwa kwa dhambi mbili. Kwanza, baadhi ya mapadre na maaskofu kuunga mkono serikali ya Habyalimana katika kuwabagua Watusi. Pili, baadhi mapadre na maaskofu kukaa kimya wakati hayo yanaendelea. Kundi la kwanza lilienda mbali na kushirikiana na polisi (kwa kuwaonyesha walipo Watusi) ili wauawe. Sasa Je TEC yetu imefanya lipi kati ya hayo mawili ili iwaombe radhi watanzania? Inaunga mkono serikali katika kuvitesa vyama vya upinzani?! Je iko kimya kama TEC ya Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari?!

Nijuacho mimi, TEC kwa ukubwa wake, ikikaa kimya ni taabu, Ikisema ni taabu. Haya sasa, waondoeni wakatoliki wooote kila mahali na funga midomo yao, tuone kama matatizo yetu yatayeyuka kama umande!

Jamani, Tutafute watu wazuri na wabobevu wa kuwasema TEC. Hawa waliojitokeza, wanawasafisha TEC wakati si lengo lao kuwasafisha.

NARUDIA: Kuna kitu hakikwenda sawa tarehe 29/10/2025. Yawezekana halikuwa lengo hilo lakini kikatokea. Kusema SAMAHANI haiondoi wala kupunguza heshima yetu. Kama taifa, tunalazimika kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.

Baba wa Taifa aliwahi kutuadithia kisa cha dereva wa Ikulu aliyekuwa anapiga “rivasi” akamkanya mtoto wake na kumuua. Aliumia lakini akaendelea na msafara na kurudi baadaye kwa mazishi. Uzalendo una gharama.

Ugumu wa moyo haujawahi kuleta amani wala suluhisho. Serikali yetu siyo malaika.
 
THE BIG SHOW njoo huku utapake uisilamu wako.
 
Tec tunataka MoU ifutwe, vyuo vikuu vyao vikose fedha ili vifungwe
Halafu hivyo vyuo vyao vikuu vikifungwa, wanafunzi wote watahamia Muslim University ya Morogoro siyo! Aisee kuna watu mna akili fupi sana. Eti tunataka Mou ifutwe! Aliyekuambia Kanisa Katoliki linaishi kwa kutegemea hiyo Mou yako ni nani?
 
Kabisa,hawa hawana jeuri yoyote ndani ya nchi hii hawa kenge.

Kwanza wanaifilisi sana nchi hii kwa kuchota mamillion ya fedha serikalini eti kwa kigezo cha kutoa huduma,huduma gani wanatoa hawa ili hali huduma sisi tunalipia??

Dawa yao ni kukata hiyo mirija tuone jeuri yao inatoka wapi kima hawa
 
Utasubiri sana !!Kanisa Katoliki siyo Maskini kihivyo.
Wanavyuo vikuu vingi kuliko serikali na makanisa mengine
Wana hospitali za kutosha kuliko makanisa yoyote.
Sasa kama wana vyuo na hospital why wasiendeshe wenyewe hizo.hospital hadi waombe pesa serikalini??

Hawana lolote ni omba omba tuh
 
Sadaka za jumapili ya mwezi mmoja tu zinafund huo upupu wote unaoomba ufutwe
Sawa,tunataka hizo mou zifutwe sasa muanze kujitegemea...mnalitia hasara sana taifa hili.

Yaone yamejazana serikalini huko kazi kuiba fedha za umma na kukimbilia kutoa sadaka makanisani kama vichaa vile
 
Tec tunataka MoU ifutwe, vyuo vikuu vyao vikose fedha ili vifungwe
Malaria
TEC haiwezi kukosa pesa, ni watu wabunifu na siyo wafujaji, hizo kodi au unafuu waliokuwa wanapata kutoka serikalini ilikuwa kama "subsidies" siyo kweli kuwa ni masikini. Angalia investments zao hata kabla ya uhuru, hao watu wenu kama JK hawangesoma kama siyo TEC na mashirika ya dini ya Kikristo.
Tosamaganga, St Georges Mkwawa, Kibaha, St Marys Pugu, Forodhani nk nk.
Angalia na Mahospitali yenu.

Mbinu: TEC ni Thinkers. Nyie Madrassa ni Majungu- badala ya kutafiti na kupata mradi ili muingie ubia na Serikali ili nanyi muendeleze Taasisi zenu mnakalia kuwa ati Serikali ifute Taasisi za Kikatoliki. Sijui akili ya wapi hii.
 
Sadaka za jumapili ya mwezi mmoja tu zinafund huo upupu wote unaoomba ufutwe
Wasingeingia huo mkataba wa kitapeli,wewe na padre sivalon nani anajua?.. sivalon kwenye kitabu chake 'kanisa katoliki na siasa tz' anasema bila serikali kusaidia miradi ya kanisa ingekufa,yaani Kodi zetu zinasaidia miradi ya kanisa
 
Viongozi wengi wa Tz wanesoma seminary…amiwemo mzee wa pwani…liacheni kanisa katoliki…Narudia tena…mkasome tena vitabu vya historia kulijua hili kanisaa…Missionaries ni genesis si tu Tanzania bali ni Africa na Dunia kiujumla..
 
Halafu hivyo vyuo vyao vikuu vikifungwa, wanafunzi wote watahamia Muslim University ya Morogoro siyo! Aisee kuna watu mna akili fupi sana. Eti tunataka Mou ifutwe! Aliyekuambia Kanisa Katoliki linaishi kwa kutegemea hiyo Mou yako ni nani?
Kanisa siku zote wanategemea fedha za wizi kama sadaka kutoka kwa kondoo wao na mou kutoka serikalini na kupenda dezo dezo kwa kupitisha uchafu wao pale bandarini kwa mgongo wa dini,hawana ujanja wa kutafuta chochote TEC ni kama mashoga tuh
 
Back
Top Bottom