PostGE2025 Askofu Bagonza: Kuna โ€œvitaโ€ imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini

PostGE2025 Askofu Bagonza: Kuna โ€œvitaโ€ imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Vipi Mum bila msaada wa kulipiwa mishahara ya malecture wao wanaweza hata kussustain mwez mmoja? Toka walivyopewa na serikali hivi wamefanikiwa hata kuongeza tawi jingine?
Hivi MUM ni chuo au Madrasa ya watu wazima??
Nachoka mie kilembwe wa Clemence mwandambo.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Kabisa,hawa hawana jeuri yoyote ndani ya nchi hii hawa kenge.

Kwanza wanaifilisi sana nchi hii kwa kuchota mamillion ya fedha serikalini eti kwa kigezo cha kutoa huduma,huduma gani wanatoa hawa ili hali huduma sisi tunalipia??

Dawa yao ni kukata hiyo mirija tuone jeuri yao inatoka wapi kima hawa
Hivi Serikali ikichukuwa majengo yake pale Morogoro na kuyarudisha Tanesco waislam watabaki na chuo gani?
 
Kabisa,hawa hawana jeuri yoyote ndani ya nchi hii hawa kenge.

Kwanza wanaifilisi sana nchi hii kwa kuchota mamillion ya fedha serikalini eti kwa kigezo cha kutoa huduma,huduma gani wanatoa hawa ili hali huduma sisi tunalipia??

Dawa yao ni kukata hiyo mirija tuone jeuri yao inatoka wapi kima hawa
Kwanini serikalini isianzishe huduma nafuu kwa wananchi, ili miradi hiyo unayodai ijifie yenyewe
 
Tec tunataka MoU ifutwe, vyuo vikuu vyao vikose fedha ili vifungwe
Mou iliwekwa kwa ajili ya maswala ya afya na sio Elimu.
Na pia MOU ilikuwa kwa ajili ya madheebu yote ya kikiristo na sio Katoliki pekee- kumbuka kina mama Wajawazito na Watoto na wenye TB,HIV,Sukari,Ukoma,....na Wazee bila kujali dini wanatibiwa Bure MOU ndo kazi yake, Elimu ,Ipo Bodi ya mikopo isiyo na dini. Acha Chuki zisizo na mashiko
 
Mou iliwekwa kwa ajili ya maswala ya afya na sio Elimu.
Na pia MOU ilikuwa kwa ajili ya madheebu yote ya kikiristo na sio Katoliki pekee- kumbuka kina mama Wajawazito na Watoto na wenye TB,HIV,Sukari,Ukoma,....na Wazee bila kujali dini wanatibiwa Bure MOU ndo kazi yake, Elimu ,Ipo Bodi ya mikopo isiyo na dini. Acha Chuki zisizo na mashiko


Msingi wa makubaliano hayo ni makanisa kuhakikishiwa kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kwao kutoa huduma za elimu na afya.

Makubaliano hayo yamegawanywa katika maeneo makubwa mawili, ambayo ni sekta ya elimu na afya na kila sekta ikiwa imetengenezewa bodi yake ndani ya mtandao wa makanisa kupitia CCT na TEC.
 
Kuutetea uongo yataka moyo sana,mbaya zaid zero brain ndo wanatumwa waje kujibu waraka wa tec. Kwa kifupi huu ndio mwisho wa utawala wa kiimla.
 
Yaani ondoa wenye D mbili kwenye matokeo ya kidato cha nne, mtoto wa darasa la saba tu hawezi kumuelewa mkoloni wa kijani.
 
Sawa,tunataka hizo mou zifutwe sasa muanze kujitegemea...mnalitia hasara sana taifa hili.

Yaone yamejazana serikalini huko kazi kuiba fedha za umma na kukimbilia kutoa sadaka makanisani kama vichaa vile
Hua unakaa na kujitafakari lakini!!!... Mtu mwenye akili hawezi kujaa chuki tu bila sababu. Wakatoliki kufika hapo walipo sio jambo la kukurupuka km mnajindanganya mmempa mtoto wenu unaibu akafaulishe shule za kiislam ni kichekesho.Jifunzeni na kua watulivu mihemko km yako ww ndo imewajaa wengi wenu.
 
Hua unakaa na kujitafakari lakini!!!... Mtu mwenye akili hawezi kujaa chuki tu bila sababu. Wakatoliki kufika hapo walipo sio jambo la kukurupuka km mnajindanganya mmempa mtoto wenu unaibu akafaulishe shule za kiislam ni kichekesho.Jifunzeni na kua watulivu mihemko km yako ww ndo imewajaa wengi wenu.
Kumbe Naibu Waziri anaweza kufaulisha Wanafunzi. Nilikuwa sifahamu hili. Shukurani kwa kunijengea uelewa.๐Ÿ™
 
Kumbe Naibu Waziri anaweza kufaulisha Wanafunzi. Nilikuwa sifahamu hili. Shukurani kwa kunijengea uelewa.๐Ÿ™
Uchaguzi umeona kimefanyika nn hebu jipe mda tu utakumbuka hili.. Tuendako ni shimoni tumekubali vilaza waruongoze
 
Axha
Sawa,tunataka hizo mou zifutwe sasa muanze kujitegemea...mnalitia hasara sana taifa hili.

Yaone yamejazana serikalini huko kazi kuiba fedha za umma na kukimbilia kutoa sadaka makanisani kama vichaa vile
Acha wivu shehe wahimize ndg wakasome, vigezo kuajiriwa serikali ni elimu dunia tuu!.
Baadhi ya waislam haswa ambao sio bakwata wamelitambua hili na wanafanya vzr sana...nyie wa bakwata bakini hivyo hivyo na ujinga wenu!.
 
Tec tunataka MoU ifutwe, vyuo vikuu vyao vikose fedha ili vifungwe
Hivyo vyuo vikuu huwa vinasajili wakristo pekee?Hapana!
Ni kila dini, rangi,kabila hata wageni toka nje!

Hii ni hasara kwa taifa au kwa taasisi?
Lets reason like we are in 2030 people, lets be reasonanble!
 
Tec tunataka MoU ifutwe, vyuo vikuu vyao vikose fedha ili vifungwe
Haitatokea hiyo sahau.
Kila Jumapili wanachangisha pesa.
Kila kipato cha mkatoliki anachangia kaisa lao 10%.
Bado mavuno na michango mingine. Ndiyo maana wananunua maeneo na kuwekeza miradi mingi mikubwa.
Mkianza hiyo Vita na wao wakajibu kwa kuwapa huduma wakatoliki pekee, haki itakuwa mabaya sana kwa Serikali na wa dini nyingine.
Ukumbuke serikali ya Tanganyika/Tanzania yenyewe ndiyo aliyo Anza kupewa msaada na kanisa katoliki. Mfano shule ziizo chukuliwa na serikali.
 
Hivi MUM ni chuo au Madrasa ya watu wazima??
Nachoka mie kilembwe wa Clemence mwandambo.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Pale MUM nasikia mpaka viboko vilikuwa vinatumika wakati fulani. Ni siku hizi tu ndiyo nasikia hali imetengemaa.
 
Msingi wa makubaliano hayo ni makanisa kuhakikishiwa kuwa serikali itaweka mazingira mazuri kwao kutoa huduma za elimu na afya.

Makubaliano hayo yamegawanywa katika maeneo makubwa mawili, ambayo ni sekta ya elimu na afya na kila sekta ikiwa imetengenezewa bodi yake ndani ya mtandao wa makanisa kupitia CCT na TEC.
Wakati nyinyi mko busy kupokea misaada ya kujengea misikiti ili mswali swala tano kwa siku, wenzenu walikuwa busy kununua maeneo makubwa ya pembezoni na kujenga mashule vyuo vikuu na mahospitali! Matokeo yake ndiyo haya sasa. Mmejaa tu chuki nyingi zisizo na kichwa wala miguu. Toeni hiyo Mou yenu hata kesho halafu tuone nani ataathirika.
 
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe Kalikawe Lwakalinda Bagonza kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook anasema;

WARAKA WA TEC: Kuna Watu Wanaiharibia Serikali.

Kuna โ€œvitaโ€ imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini. Vita hiyo inaiumiza serikali kuliko walengwa wa vita hiyo. Nashauri tuiache serikali ijiharibie na uwezo huo inao. Tafakari haya yanayosemwa na watu wasiojisikiliza wakati wanaongea:

1. BANDARI: Kwa hiyo miaka yote TEC wanakwepa kodi, wanauza madawa ya kulevya na mambo mengine machafu, na serikali zooooote zilizopita ziliwaacha mpaka awamu hii ya sita?!

2. VURUGU ZA UCHAGUZI MKUU: Kwa hiyo TEC ndiyo iliyoharibu uchaguzi, ikaua watu, ikaharibu mali, ikazima internet nk?

3. MATAMKO YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI: Kwa hiyo SADC, AU, EU, State Department na Balozi zooote zilizosema uchaguzi ulikosa viwango, wote hao ni Wakatoliki au walishinikizwa na TEC?!

4. UTEKAJI: kwa hiyo, wakatoliki ndio walioagiza watu watekwe, wakampiga na Fr Kitima, wakateka mapadre na kuwadhalilisha au TEC hao hao wakafunga midomo ya viongozi kutokemea vitendo hivyo?

5. WASIOJULIKANA: Kwa hiyo hawa TEC ndio wasiojulikana ambao wanaogopwa na serikali kiasi cha kutofungua midomo kuwakemea?

6. MAANDAMANO: Kwa hiyo TEC ina nguvu ya kuwahamasisha vijana wa dini zote, vyama vyote, jinsia zote kuingia barabarani? Kwa hiyo TEC ina nguvu kuliko serikali na wazazi?

7. RUSHWA NA UFISADI: kwa hiyo TEC ndiyo inanyamazia ripoti za CAG, inagawa rushwa ndani na nje ya vyama wakati wa uchaguzi? TEC ndiyo inawalipa wanaotumia mitandao kuitukana serikali na sasa imewalipa ili waitukane TEC?

TEC ndiyo inayoagiza watu wale rushwa bila hofu ya TAKUKURU?

8. MAUAJI YA RWANDA: Kanisa Katoliki Rwanda lilihukumiwa kwa dhambi mbili. Kwanza, baadhi ya mapadre na maaskofu kuunga mkono serikali ya Habyalimana katika kuwabagua Watusi. Pili, baadhi mapadre na maaskofu kukaa kimya wakati hayo yanaendelea. Kundi la kwanza lilienda mbali na kushirikiana na polisi (kwa kuwaonyesha walipo Watusi) ili wauawe. Sasa Je TEC yetu imefanya lipi kati ya hayo mawili ili iwaombe radhi watanzania? Inaunga mkono serikali katika kuvitesa vyama vya upinzani?! Je iko kimya kama TEC ya Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari?!

Nijuacho mimi, TEC kwa ukubwa wake, ikikaa kimya ni taabu, Ikisema ni taabu. Haya sasa, waondoeni wakatoliki wooote kila mahali na funga midomo yao, tuone kama matatizo yetu yatayeyuka kama umande!

Jamani, Tutafute watu wazuri na wabobevu wa kuwasema TEC. Hawa waliojitokeza, wanawasafisha TEC wakati si lengo lao kuwasafisha.

NARUDIA: Kuna kitu hakikwenda sawa tarehe 29/10/2025. Yawezekana halikuwa lengo hilo lakini kikatokea. Kusema SAMAHANI haiondoi wala kupunguza heshima yetu. Kama taifa, tunalazimika kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.

Baba wa Taifa aliwahi kutuadithia kisa cha dereva wa Ikulu aliyekuwa anapiga โ€œrivasiโ€ akamkanya mtoto wake na kumuua. Aliumia lakini akaendelea na msafara na kurudi baadaye kwa mazishi. Uzalendo una gharama.

Ugumu wa moyo haujawahi kuleta amani wala suluhisho. Serikali yetu siyo malaika.
Usiwajibu hawa Masheik ubwabwa ,utapoteza muda wako bure ,tuachie sisi
 
๐ƒ๐ ๐–๐จ๐ซ๐ฅ๐ ๐ˆ๐ฅ๐ข๐ฏ๐ฒ๐จ๐ณ๐ข๐ฆ๐š ๐๐ข๐ฅ๐ข ๐œ๐ก๐š๐Ÿ๐ฎ ๐ณ๐š ๐“๐„๐‚ ๐๐š๐ง๐๐š๐ซ๐ข ๐ฒ๐š ๐ƒ๐š๐ซ, ๐ง๐š ๐ก๐ฎ๐จ ๐ฎ๐ค๐š๐ฐ๐š ๐ง๐๐ข๐จ ๐ฆ๐ฐ๐š๐ง๐ณ๐จ ๐ฐ๐š ๐œ๐ก๐ฎ๐ค๐ข.
Tangu mwaka 1957, TEC imekuwa ikiishi kwenye kivuli cha nguvu na heshima. Machoni pa umma, ni taasisi ya kiroho inayohubiri maadili na utulivu wa taifa.

Lakini ndani ya kuta zake zenye utulivu, kulijengwa mfumo wa siri uliounganisha dini, biashara, na siasa, mfmo uliotengeneza mabilioni chini ya kivuli cha sadaka na misaada.

Mwaka 2022, serikali ilipoanza mazungumzo na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji ya DP World kwa ajili ya kuendesha Bandari ya Dar es Salaam, TEC iliona tishio lisiloelezeka.

Kwa muda mrefu, bandari hiyo ilikuwa kitovu cha biashara zake zisizo rasmi, makontena yaliyosafiri chini ya majina ya taasisi za dini, yakiwa yamejaa โ€œvifaa vya misaadaโ€ vilivyopokea msamaha wa kodi.

Lakini ndani yake kulikuwa bidhaa zenye thamani kubwa, dawa za kulevya, vifaa vya kielektroniki vya magendo, na hata fedha taslimu zilizotoka kwenye mitandao ya kifedha ya kimataifa.

Mfumo wa TEC ulikuwa umejikita ndani ya serikali katika vitengo vingi vyeti kwa lengo tu la kusaidia harakati na michongo ya TEC. Wafanyakazi wa umma waliokuwa washirika walihudhuria ibada za kifahari, walibarikiwa hadharani, nyuma ya pazia wakiwa walinzi wa maslahi ya mtandao huo wakinyonyaji.

Mikataba ya ujenzi, usafirishaji, na forodha ilipangwa kupitia โ€œmiradi ya kijamiiโ€ ya TEC, huku ripoti za ukaguzi zikiwa haziyaoni haya yote.

Kuibuka kwa DP World kulikuwa kama kengele ya hatari. Kampuni hiyo iliahidi mfumo wa kisasa wa kidigitali wa kufuatilia mizigo, teknolojia ambayo ingeweka kila shehena wazi kwa mamlaka za kimataifa.

Kwa TEC, hili halikuwa jambo dogo, lilikuwa tishio kwa mfumo mzima uliowajengea nguvu na utajiri kwa miongo kadhaa.

Lakini wakati upepo wa mabadiliko ukivuma, Rais Samia Suluhu Hassan aliingia madarakani akiwa na maono mapya. Alisisitiza uwazi, ufanisi, na mageuzi ya sekta ya bandari ili Tanzania iwe kitovu cha biashara cha Afrika Mashariki.

Wakati wengi waliona hatua hiyo kama mapinduzi ya kiuchumi, kwa baadhi ya watu ndani ya TEC, ilikuwa ni vita.

Vita vya waziwazi dhidi ya serikali ya Rais Samia Suluhu vikaanza, mimbari zikaanza kuhubiri kuhusu โ€œuhuru wa kiuchumiโ€ na โ€œulinzi wa rasilimali za taifa,โ€ huku nyuma ya pazia barua zikipelekwa kwa viongozi wa serikali, zikishinikiza kuahirishwa kwa makubaliano ya DP World.

Wengine wanasema hata baadhi ya wanasiasa waliokuwa na uhusiano wa karibu na TEC walitumia uzito wao ndani ya bunge kupinga mkataba huo kwa hoja za kizalendo, ilhali nia halisi ilikuwa kulinda mtandao wa siri.

Hata hivyo, chini ya uongozi thabiti wa Rais Samia, serikali haikurudi nyuma. Mabadiliko ya kidigitali yaliendelea kutekelezwa, na mifumo ya kidhibiti mizigo ikawekwa, hatua iliyofichua mambo mengi yaliyokuwa yakifichwa kwa jina la dini. TEC ilitetemeka.

Na huu ndio ulikuwa mwanzo wa chuki kati ya TEC na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mabadiliko yaliyokuwa yakiletwa kupitia mageuzi ya bandari yalitikisa mizizi ya mtandao uliokuwa umezoea kufanya kazi gizani kwa miaka mingi.

Kampuni nyingi zilizo chini ya mwavuli wa taasisi hiyo ya kidini zilianza kupoteza vibali, akaunti zikagandishwa, na washirika wao serikalini wakaanza kuogopa kivuli chao wenyewe.

Kama ilivyokuwa kwa nguvu yoyote inayokataa kuondoka, TEC ilianza kutumia silaha yake kuu ya ushawishi, waraka baada ya waraka kila siku zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye majukwaa ya yao ya dini, baadhi yakihubiri โ€œuhuru wa taifa,โ€ mengine yakilalamikia โ€œudikteta .โ€

Kila sentensi ilikuwa na lengo moja, kugeuza imani kuwa kivuli cha upinzani.
Ndani ya kumbi za siri, mikutano ilifanyika kati ya maafisa wa serikalini wenye maslahi na TEC, wakijadili njia za kuvujisha taarifa, kudhoofisha kazi za serikali, na kuibua taharuki.

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, iliyoamini katika uwazi na mageuzi, haikuogopa. TEC ikaona wazi zama zao za ushawishi zimeanza kufika ukomo, na hapa ndipo chuki ikazaliwa kwa kiwango kikubwa sana.

Kila mvutano, kila taharuki unayoiona leo, ni matokeo ya mnyororo ulioanza tangu mwaka 2022, pale mazungumzo ya DP World (DPW) yalipoanza rasmi. Ilikuwa ni kipindi ambacho TEC imezoea kuendesha mambo kinyume na sheria, baada ya kuona mabadiliko yakija kwa kasi kama kwenye teknolojia hasa ukaguzi wa kidigitali na uwazi wa kifedha, kwa TEC, huu ulikuwa mwanzo wa mwisho wao.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi mwaka 2025, baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumchagua tena Rais Samia Suluhu Hassan kama mgombea wao wa urais. Ndipo hofu ikazidi kushika mizizI.

Waliamini kwamba, endapo angeendelea kuongoza, wangekuwa na hali mbaya zaidi, kwani wao tayari wana mtu wao waliyetegemea angeingia mwaka 2025, hii iliwauma sana.

Hizi vurugu zote na machafuko yaliyotokea na ambayo yanaendelea kupangwa muda huu, hayana uhusiano wowote na ukombozi wa nchi, uhuru, ulinzi wa rasilimali za Tanzania wala kupinga rushwa na utekaji, bali ni azma ya Kanisa Katoliki chini ya TEC kumuondoa madarakani Rais Samia Suluhu ili waweze kutimiza malengo yao ya wizi na ufisadi chini ya mwamvuli wa dini.

KATAA AGENDA ZA MAKANISA NA MAASKOFU ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
 
Back
Top Bottom