Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani kaongea nini kibaya?
Nyie mnajuaje kasema yote? Mlikuwepo kwenye kikao au ni hisia zenu zinawatuma kuwa Lissu kaongea yote? Mnajuaje kazungumza kuwawin wazee wa kulisha maneno kaamua kuwawahihata mimi nililiona hili, nadhani hakupaswa kusema hayo yote..ingekuwepo na summary ya pande zote.
Rais ni rais tu..lazima apewe heshima yake
Si askofu wenu- wewe nani unapingana na askofu tena wa KKKT na mshauri wa kiroho wa Lissu
Sikiliza wewe- Lissu kakosea na kakosea big time
Inawezekana hujamuelewa askofu. Ni kweli Lissu hakutakiwa kutoa taarifa ya walichozungumza unless otherwise kama wamekubaliana.Rroho na ikuume tu. Nchi imelipuka kwa shangwe.
Sioni kosa la Bagonza ni maoni yake tu.
Tundu hakukutana na Rais kuomba maji, barabra na umeme. Kaongea maswala mtambuka ya watanzania kama Taifa.
Ni mambo yale yale ya siku zote. Siri ya nini?
Askofu Dkt. Bagonza ameeleza haya baada ya Rais Samia kukutana Tundu Lissu, naa baadaye Lissu kuongelea kile alichozungumza na Rais.
Lissu anaweza kuwa amekosea kwenda in detail ya mazungumzo na Rais, na wasaidizi wa rais wanaweza kuwa wamekosea kurusha picha za Lissu kukaguliwa, kusisitiza nani kaomba kukutana, usuluhishi unahitaji restraint, Rais anapotoshwa, Lissu akiendeshwa na mashabiki"
Pia soma
- BRUSSELS, UBELGIJI: Rais Samia akutana na Tundu Lissu na kufanya mazungumzo mafupi
- Summary ya Maongezi ya Rais Samia na Tundu Lissu yaliyofanyika Ubelgiji
Kasema kwa faida ya nani?? In protocol hii imekaaje ukutane na Rais halafu Rais asiseme mmezungumza nini na wewe ukaenda kubwabwaja? Sio sawa!Kwa hili napingana na Dkt Boganza. Lissu kafanya vema sana kusema ukweli & uwazi wa kilicho zungumzwa! La sivyo wachawi wasingekawia kumtungia stories za kusaliti au kusalimu amri!
Ni kweli Lissu na Mwendazake kuna vitu wanafanana.Mbowe ni mtu mwenye kifua na mnaweza fanya compromise ila sio mtu kama Lisu,ni dizaini ya Mwendazake wote waropokaji tuu.
Nakubaliana na wewe mia kwa mia ,wewe ndio mtu mwenye akili zaidi kuchangia mjadala huu.Lissu amefanya vile ili kusiwepo na aina yoyote ya kukasalitiana. Ikumbukwe leo Rais alitakiwa kukutana na uongozi wa EU hivyo kikao na Lissu ni turufu kwa serikali ya SSH kuliko kwa Lissu.
Kwa vyovyote, Rais alitaka kujenga hoja ya kuwa na nia njema ya kuanzisha mjadala na upinzani hususani Lissu ambaye yupo ukimbizini alikokwenda kupitisha bakuli.
Kwa Lissu kutoka hadharani na kusema yale, Rais anafungwa na hawezi kumgeuka Lissu kwenye zile hoja, labda atashindwa kutekeleza makubaliano kwa shinikizo la chama chake lakini dunia itajua hakuwa mkweli katika mjadala. Lissu asingetumia ile fursa, hoja zingepitishwa kinyemela katika meza ya mazungumzo na viongozi wa EU alafu rais akirudi nchini anaamua kupotezea, hapo tayari Lissu anakuwa ametumika.
Bora kushangilia kuliko kusifia ata ujinga.Maana kamwe huwexi kushangilia jambo ambalo halikufuraishi ila unaweza kusifia ata mambo ya kijinga.Sasa wewe kama una akili timamu jiulize uko upande gani kati ya hayo mambo mawili.
Hivyo ndivyo alivyo Lissu wala hata sio kwa sababu ya lile tukio alilofanyiwa.Sometimes Lissu ni wa kumsamehe tu, madhira aliyofanyiwa hata ingekuwa mimi au wewe tusingekuwa sawa kisaikolojia muda wote.
All in all, ilikuwa ni vyema wamekutana na kuwa na kikao, mengine yote ni yatokanayo tu
Ulitaka nani aseme?.Mwenye agenda zakumwambia rais alikua Lissu sasa ulitaka rais ndiye aje aseme kua niliongea na lissu na kaniambia kesi ya mbowe ni kesi ya mchongo..Rais hana sababu yoyote yakuelezea umma mazungumzo ya lisu yalivyokua maana yaye yuko kwenye upande wa kutekeleza hoja alizoletewa ila lissu ana sababu kwasababu mazungumzo yale yanafaida kwake,chama chake na hali ya kisiasa kwa ujumla.na amefanya vyema kueleza ili wananchi tujue na tumsubiri rais aamue atakalo amua.sasa sijui vichwa vyenu vinatakaje.Kasema kwa faida ya nani?? In protocol hii imekaaje ukutane na Rais halafu Rais asiseme mmezungumza nini na wewe ukaenda kubwabwaja? Sio sawa!
Rais hajaumizwa kwa lolote ila nyie kajamba nani na roho zenu za kutu ndio mnajifanya mmeumia.kwendeni uko.hopeles kabisa.Ni kweli na hii inaonyesha hafai kuwa kiongozi mkubwa.
Rais kamheshimu amemfuata unless wangaitisha press ya pamoja.
Mh.Rais next time achana na Hawa wajinga wasio na adabu wala wasiojoelewa.
Hilo lijamaa limezoea kuropoka ropoka. Sijui linaogopa nini kurudi ilhali liligombea urais na kupoteza viti kibao vya wabunge na hakuna mtu aliligusa.
Hilo swali waulize misukule ya ufipa....Bora kushangilia kuliko kusifia ata ujinga.Maana kamwe huwexi kushangilia jambo ambalo halikufuraishi ila unaweza kusifia ata mambo ya kijinga.Sasa wewe kama una akili timamu jiulize uko upande gani kati ya hayo mambo mawili.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app