Askofu Bagonza: Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA

Askofu Bagonza: Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA

LUKA 6:26 haiongelei wakuu wa dola, wafalme, askari, watoza ushuru nk. Bali inaongelea manabii: wachungaji, wahibiri, na wengine wote wenye kujiita watumishi wa Mungu.
hii nukuu yako inahuikaje hapa au mmeanza kulewa sifa kama Belshaza,
DANIEL 5:
25Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. 26 Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. 27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. 28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. 29Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme. 30 Usiku huo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. 31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.
 
Maandiko haya hayana uhusiano na suala linaloongelewa
 
Nime zoom hiyo picha ya Askofu uso umejaa mapele kulikoni isije kuwa gonjwa lileeeeeeeee

Akina mama kaeni mbali
 
Hili jiwe naona wale wanaosema
"Bontwe ngali bontwe ngali"

Jiwe liko hewani wenye vichwa vikubwa litawaangulia
 
Ujumbe huu ni muafaka kabisa kwa wote, ila ukiwa na kibri utaudharau na mguu utaota tende.
 
Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Aisee hujui ulisemalo. Kwenye mataifa mengine machafuko yakitokea wakuu wa dini ndio unapoonekana umuhimu wao
 
Anaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA. Inaonekana viliingia nchini tarehe 27/7/2020 kupitia jiji la DSM.

Madaktari wanadai dalili za LISSUPHOBIA ni hizi:
1. Hofu ya vyombo vya habari
2. Hofu ya mikusanyiko
3. Hofu ya matumizi ya mitandao ya kijamii
4. Kirusi kinashawishi kupindisha sheria na taratibu za kawaida
5. Hudhoofisha uwezo wa kutenda kwa haki
6. Hudhoofisha uwezo wa kukumbuka yaliyopita
7. Huzuia uwezo wa kujifunza kwa majirani na kinaongeza uwezo wa kujipendekeza kwa vyombo vya dola
8. Dalili mpya hujitokeza kwa mgonjwa kila wakati na kuhitaji kupimwa kila wakati
9. Kirusi kinamsukuma mgonjwa kuwa karibu na Mungu kinadharia na kumkimbia Mungu anapomkaribia mgonjwa

Dalili za kirusi cha LISSUPHORIA ni hizi:
1. Ujasiri uliopitiliza
2. Kuhisi kuonewa kila wakati
3. Kujiona ni tiba ya LISSUPHOBIA kwa sababu ndiye amesababisha LISSUPHORIA
4. Kuamini kuwa kinatibu kukosekana kwa ajira, na kuleta utawala bora
5. Kumfanya mgonjwa ajione ana uwezo wa kutibu kila ugonjwa ikiwemo kukosa "nguvu za kiume"
6. Mgonjwa kuamini anaanza na Mungu na kumaliza na Mungu
7. Kumfanya mgonjwa aamini kirusi hiki kinastawisha uzalendo
8. Kinamfanya mgonjwa kupoteza uwezo wa kutunza siri zake
9. Kinamfanya mgonjwa amshuku kila mtu aliyewahi kuwa karibu na mgonjwa wa LISSUPHOBIA

Virusi hivi viwili visambaa kwa kasi hapa nchini. Madaktari wanashauri wagonjwa wa virusi hivi viwili vya hatari, kutumia dawa moja inayofanana na wakiishapona wadungwe chanjo ili wasiambukizwe tena.

Dozi ya dawa hiyo ni:
1. Matumizi sawa ya vyombo vya habari kutwa mara tatu.
2. Matumizi ya hoja mara 12 kwa siku
3. Kuheshimu sheria mara 24 kwa siku
4. Kula upendo mara 2, kunywa uvumilivu mara 3 na kujipaka mafuta ya umoja mara 6 kwa siku.

Wakati wote wa kutumia dozi hii, wagonjwa waepuke:
1. Matusi na kejeli
2. Matumizi ya vyombo vya dola
3. Kutumia raslimali za nchi kwa masuala ya kiitikadi
4. Kutumia dini, kabila, au ubaguzi wa namna yoyote
5. Wote wajiepushe na imani ya kuwa mwisho wa dunia ni siku ya uchaguzi mkuu wa 2020. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Wamwogope Mungu na Teknolojia.

When you know..You know
 
Kanisa lake liko wapi wakuu na mimi jumapil nikapokee upako wake huyu baba askofu, kiukweli amenibariki sana na kuinua hali yangu kiroho.
 
Back
Top Bottom