Shehullohi
JF-Expert Member
- Jul 21, 2020
- 3,751
- 3,698
Mpelekeeni ujumbe baba askofu huwezi kutumikia mabwana wawili, "Mungu na Lissu" Mtumishi wa mshahara katika ubora wake.
Unataka kupanuliwa wapi?Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Kwani utofauti WA yeye na huyo gwajima kwa ulichokizungumza kina utofauti gani?tunamzungumzia huyu hatujamzungumzia Gwaji boy fungua uzi na wewe tuchangie kuhusu Gwaji
Unawafahamu WAAMUZI kwenye Biblia??Mpelekeeni ujumbe baba askofu huwezi kutumikia mabwana wawili, "Mungu na Lissu" Mtumishi wa mshara katika ubora wake.
Dogo kazaliwa juzi juzi huyo, hawezi mfahamu hata.Desmond Tutu UNAMUELEZEAJE?
wanatusumbua sana hawa watoto wa LumumbaDogo kazaliwa juzi juzi huyo, hawezi mfahamu hata.
Nchi kadha baada ya pande hasimu kuvuruga nchi imebidi wakimbilie kwa viongozi wa dini kupoza mambo. Huyu baba anajaribu kuzuia watanzania wasivurugane kama wote tujuavyo kinga ni bora kuliko tiba. Hopefully hii imepunguza ujinga wako (LoL) kwenye hili jambo.Hakuna mtu mjinga katika watumishi wa dini ila huyu tu maana haeleweki ni mtumishi wa kanisa au ni mwanasiasa achague moja dini au siasa aache ujinga wake hapa.
Unawafahamu WAAMUZI kwenye Biblia??
Wapo wengi zaidi ha wao ila hoja ni kwamba walivaa kofia mbiliSamson wa Delila au Gideon yupi mmoja wapo? Kuna ukweli kipindi cha Einstein mawani yalikuwa bado kugunduliwa? Na yeye alihitaji pair kwa ajili kuonea?
Mkuu inawezekana ni kweli kacheki.Hata wewe utakuwa huju
Ijui kama ni chizi au la maana huyo anajifanya anajua sana kila kitu hata hiyo phd yake itakuwa ya kufoji abaki sehemu moja tu ili aeleweke mbona yule padri alitangaza nia ya kugombea akafukuzwa upadri nao hawana akili? Jistukie utakuwa huna akili vizuri wewe.
Anaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
Taifa letu limekumbwa na virusi viwili vya hatari. Kimoja kinaitwa LISSUPHOBIA na kingine kinaitwa LISSUPHORIA. Inaonekana viliingia nchini tarehe 27/7/2020 kupitia jiji la DSM.
Madaktari wanadai dalili za LISSUPHOBIA ni hizi:
1. Hofu ya vyombo vya habari
2. Hofu ya mikusanyiko
3. Hofu ya matumizi ya mitandao ya kijamii
4. Kirusi kinashawishi kupindisha sheria na taratibu za kawaida
5. Hudhoofisha uwezo wa kutenda kwa haki
6. Hudhoofisha uwezo wa kukumbuka yaliyopita
7. Huzuia uwezo wa kujifunza kwa majirani na kinaongeza uwezo wa kujipendekeza kwa vyombo vya dola
8. Dalili mpya hujitokeza kwa mgonjwa kila wakati na kuhitaji kupimwa kila wakati
9. Kirusi kinamsukuma mgonjwa kuwa karibu na Mungu kinadharia na kumkimbia Mungu anapomkaribia mgonjwa
Dalili za kirusi cha LISSUPHORIA ni hizi:
1. Ujasiri uliopitiliza
2. Kuhisi kuonewa kila wakati
3. Kujiona ni tiba ya LISSUPHOBIA kwa sababu ndiye amesababisha LISSUPHORIA
4. Kuamini kuwa kinatibu kukosekana kwa ajira, na kuleta utawala bora
5. Kumfanya mgonjwa ajione ana uwezo wa kutibu kila ugonjwa ikiwemo kukosa "nguvu za kiume"
6. Mgonjwa kuamini anaanza na Mungu na kumaliza na Mungu
7. Kumfanya mgonjwa aamini kirusi hiki kinastawisha uzalendo
8. Kinamfanya mgonjwa kupoteza uwezo wa kutunza siri zake
9. Kinamfanya mgonjwa amshuku kila mtu aliyewahi kuwa karibu na mgonjwa wa LISSUPHOBIA
Virusi hivi viwili visambaa kwa kasi hapa nchini. Madaktari wanashauri wagonjwa wa virusi hivi viwili vya hatari, kutumia dawa moja inayofanana na wakiishapona wadungwe chanjo ili wasiambukizwe tena.
Dozi ya dawa hiyo ni:
1. Matumizi sawa ya vyombo vya habari kutwa mara tatu.
2. Matumizi ya hoja mara 12 kwa siku
3. Kuheshimu sheria mara 24 kwa siku
4. Kula upendo mara 2, kunywa uvumilivu mara 3 na kujipaka mafuta ya umoja mara 6 kwa siku.
Wakati wote wa kutumia dozi hii, wagonjwa waepuke:
1. Matusi na kejeli
2. Matumizi ya vyombo vya dola
3. Kutumia raslimali za nchi kwa masuala ya kiitikadi
4. Kutumia dini, kabila, au ubaguzi wa namna yoyote
5. Wote wajiepushe na imani ya kuwa mwisho wa dunia ni siku ya uchaguzi mkuu wa 2020. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Wamwogope Mungu na Teknolojia.
Ukijua kweli nayo kweli itakuweka huru kweli kweliAnaandika Baba Askofu Rev. Dr. Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.