Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza: Uchaguzi Mkuu au Utekaji Mkuu au Ujazaji fomu Mkuu?

Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza: Uchaguzi Mkuu au Utekaji Mkuu au Ujazaji fomu Mkuu?

Huyu naona kaishiwa sasa ya kuzungumza, hiki ndio nini sasa.
 
NEC ni kikazo sana kwa ustawi wa demokrasia.


Tumeliwa taifa la wizi wizi na udanganyifu.Tulipata katiba mzuri tutapona kama taifa
 
Fomu haigombei

Sisi tunamtaka mtu si fomu.

Miaka ya nyuma hatukuwahi kuona UCHUKUAJI FOMU MKUU

Basi haya ni maelekezo km ya UTEKAJI WA SM 2019

Usinibishie!!!!!
 
Nawasihi wanaopongeza, wanaokosoa, wanaofoka foka, wanaotafuta wasio raia, waliokwepa kodi na wachochezi, wasihangaike kutumia dawa ya bei mbaya. Dawa kuu ya kukomesha hayo yote ni UCHAGUZI MKUU, si UTEKAJI MKUU wala UJAZAJI FOMU MKUU.
UCHAGUZI MKUU uliofanyika kwa haki na kwa Uhuru unatibu magonjwa hayo.

Askofu Bagonza
Wewe askofu unastahili kupewa tuzo. Kila ukiikamata kalamu yako na kuandika kitu watanzania lukuki tunaelimika.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Jiwe hawezi kuwa na urafiki na maaskofu wanaojielewa kama hawa.

Ahsante Baba Askofu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Moja kati ya watu watamumia endapo Lisu atakatwa ni huyu Bagonza!

Jamaa ana mahaba kwa Lisu vibaya mno.
Akatwe kwa lipi hasa ? Halafu hayo mamlaka ya kukata wagombea mnayapata wapi ? Hana mahaba na Lissu , and mahaba na haki.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hawa watatu Bagonza, Mwamakula na Sheikh Issa Ponda ni Viongozi wa dini Nchini ninaowaheshimu sana na kuwapenda kwa kuwa mstari wa mbele kukemea maovu mbali mbali ya hii Serikali dhalimu ambayo yanaweza kuwa chanzo cha machafuko ya kutisha.

Jiwe hawezi kuwa na urafiki na maaskofu wanaojielewa kama hawa.

Ahsante Baba Askofu.
 
JESHI LA POLISI LIEPUKE KUWA CHANZO CHA VURUGU ZA KISIASA KATIKA MJI WA TUNDUMA NA NCHINI KWA UJUMLA!

Tumefuatilia habari hizi kutoka Tunduma! Ni tuhuma nzito kutolewa na Mgombea Urais wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini. Tuhuma hizi sio za kupuuza! Hali siyo nzuri kule Tunduma! Watu wa Tunduma wanahisia mbaya juu ya Jeshi la Polisi kuhusu hili tukio la kukamata Wagombea wa Upinzani. Wengi wao wanahisi kuwa hizo ni hujuma za wazi za kisiasa.

Tunaomba Wakuu wa Jeshi la Polisi watumie hekima katika jambo hili. Jeshi la Polisi lisiwe chanzo cha vurugu Tunduma na nchini kote kwa ujumla! Kuwakamata wagombea wa Chama Kikuu cha Upinzani katika ngome ya Upinzani na katika mazingira kama haya hakuleti afya. Jeshi la Polisi lina wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa weredi na haki na kwa mujibu wa sheria pasipo kutumika kisiasa na Chama chochote au kikundi cho chote.

Sisi tumetimiza wajibu wetu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate,

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
Huyu si aliambiwa na mkuu wake askofu Shoo kwamba wajitenge na siasa?
Hujaona wengine woote wakitumiwa na jiwe na genge lake Kila wakati?

Juzi kwny lile kongamano PM akiwa mgeni rasmi haikuwa siasa?
 
Back
Top Bottom