Askofu Benson Bagonza adai kuna wanaotaka kumdhuru, wamefika Karagwe

Askofu Benson Bagonza adai kuna wanaotaka kumdhuru, wamefika Karagwe

Sifikkri kama kukosoa ni makosa. Hata Mungu mwenyewe amekosolewa sembuse mwanadamu? Ila kwa utawala huu imekuwa ni kosa la jinai. Lakini tushamwambia Mungu ashughulike wote wanaotuharibia nchi yetu nzuri yenye maziwa na asali. Tunashukuru tushaanza kuona matunda. Ahsante Yesu!
 
Dikiteta magufuli atawamaliza wakosoaji wote hapa Tz, Bagonza omba hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa dikiteta magufuli hajawahi kuwa na huruma kwa wakosoaji!!
Alafu anajidai kuwaonea huruma waliohukumiwa kunyongwa huku mikono yake ikiwa imejaa damu
 
Sifikkri kama kukosoa ni makosa. Hata Mungu mwenyewe amekosolewa sembuse mwanadamu? Ila kwa utawala huu imekuwa ni kosa la jinai. Lakini tushamwambia Mungu ashughulike wote wanaotuharibia nchi yetu nzuri yenye maziwa na asali. Tunashukuru tushaanza kuona matunda. Ahsante Yesu!
Hayo matunda niyaone na mie.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Ona haka nako, huwezi kuvumilia wewe na nani? Na huyo muuaji ni nani? Kumbe unamjua sasa si mumfuate na risasi hata za kukodi mkampige aache kuua watu?

Umeanza tena kuleta mikwara yako kama ile ya wakati wa kampeni?

Bagonza inamtesa dhambi ya kumshabikia loser Lisu, na tulimuonya yeye kama kiongozi wa tasisi kama KKKT hapaswi kufanya vile. Unaona sasa tabu anayopata?

Haamini katika Mungu ndio maana mimi nasemaga hata tunguli atakuwa nazo lazima. Wakati wenzie wameungana kuomba kwa ajili ya corona yeye alifunga makanisa kwenye dayosisi yake ili kuwafurahisha kina Mbowe, yani tz nzima ni yeye pekeeake ndio alifunga makanisa kwa sababu yeye ana phd na ana akili sana, yani hata wapagani walimzidi kiimani huyu askofu,!
😁😁🤣🤣 wee dada wacha mbwembwe!
 
Leta kinyesi sasa ili kiwe mbolea.
Mnakosa lugha za kuwashawishi watu wema na hata waovu ili wawaunge mkono katika wema wenu au uovu wenu ndio maana hata mkiitisha maandamano hamuungwi mkono .

Fuatilia utagundua kuwa JPM anasoma sana mijadala kwenye Jamii Foram na anatoa majibu Chanya kwa wenye Mijadala sio matusi.

Kwa hivyo vijibu vya shoti kati mtaishia kulalamika tu. Unasoma ushuzi wa mtu halafu unabaki kutapika badala ya kusema kile unachoamini ili umshawishi.
Hivi nyie mnategemea kupata wapi watu wa kuwaunga mkono?
Au mnawategemea wazungu ? Wazungu hawana jibu kwa utawala wa Magufuli mana yupo siriasi kuleta maendeleo jambo ambalo linawapa wakati mgumu sana kupambana naye. Vatikani inamkubali JPM mana yupo kwa ajili ya wengi . Wezi wa chache hawana nafasi zaidi ya kutafuta vishirika vilivyochoka kuwaunga mkono ambao hauna tija. JPM sio kama akina Mugabe waliokuwa wameshachoka. Chuma kina uwezo wa kutosha sana. Lazima mje na mbinu nyingine ya kidemokrasia sio matusi. Watanzania ndio maana hawapigi kura mnabaki kusema mmeibiwa kura wakati watu wengi hawapigi kura kutokana na kukosa ladha ya siasa zenye matusi na kejeli tu. Nani akavunjwe mguu wake ili akaunge mkono matusi na kejeli.

Lazima mzungumzie maisha ya watu wengi sio wachache!. Lazima mjadili namna ya kuwafyeka waovu kwenye pato la taifa wasionekane kujipanga kutuibia tena.

Mnabahati akina Mdee na Maalim seif wameshtuka mapema na kwenda kuapishwa . Hivyo vyama vingejikuta nje ya orodha ya Msajili.
Empty verbosity! Trash.
 
Hii ndio Taarifa aliyoisambaza mitandaoni siku ya leo , kwamba kuna watu wabaya wamefika Karagwe kwa lengo la kummaliza , bali amejiapiza kwamba hatokimbia na anasubiri watekeleze Unyama wao...
Kabisa mkuu... Lisu alitaja hadi namba ya gari na aina, lakini kimyaa... CCTV zikabebwa, Kimyaaaa... Leo wansema hili kesho lile...

Hii taarifa si ya kupuuzwa kabisaa
 
Hii ndio Taarifa aliyoisambaza mitandaoni siku ya leo , kwamba kuna watu wabaya wamefika Karagwe kwa lengo la kummaliza , bali amejiapiza kwamba hatokimbia na anasubiri watekeleze Unyama wao...
Na yeye sijui kachagua nchi gani ya kwenda maana hapa tutabaki wawili tu wengine naona wanachagua nchi hahaa
 
Bagonza yeye atakuwa kachagua kwenda kuishi ujerumani
 
Bagonza yeye “afunge na kuomba” na awateketeze kwa nguvu ya Mungu. Huu ndio muda wa hawa viongozi wa dini kupractice kile wanachotufundisha sisi kila siku

‘Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA’ (Yer 1:19)
 
Sifikkri kama kukosoa ni makosa. Hata Mungu mwenyewe amekosolewa sembuse mwanadamu? Ila kwa utawala huu imekuwa ni kosa la jinai. Lakini tushamwambia Mungu ashughulike wote wanaotuharibia nchi yetu nzuri yenye maziwa na asali. Tunashukuru tushaanza kuona matunda. Ahsante Yesu!
Kikosa hakukataliwi iwapo mkosoaji anatumia hekima au staha kwenye kauli zake.

Lakini wakosoaji wengi ni tofauti wenyewe ni kumdharirisha na kuhamasisha uasi.
Sasa watu wa namna hiyo dawa yao ni kuwapelekea moto tu.
 
Pale mtu wa Mungu anapogoma kumpa heshima Kaisali na huku akijitapa kumpa heshima Mungu wakati kufanya hivyo anajua kabisa anamfanyia utovu wa nidhamu Mungu! Mungu ameishaagiza, ya Kaisali mpe na Ya Mungu ampe tena kwa heshima.
 
Nasoma kwenye mitandao lakini sijui hasa katika nchi ni chombo gani au mtu gani anayetoa uamuzi wa kuwa "mtu fulani aondolewe duniani".Wengi tunawasoma Mossad ambao kila baada ya fanikio la kumuondoa adui yao kuna wakati wanaweka sababu za kuhalalisha hilo lakini kwa hapa kwetu kwa kweli sijui.

Kinachoonekana katika matishio haya na matendo ya kuua au kuteka hapa kwetu ni uwezekano wa kuwa na kikundi chenye nguvu ya kufanya lolote bila kuwajibika kwa yoyote.

Tuiangalie mifano michache tu ifuatayo:
  1. Miaka iliyopita mgomo wa madaktari ulisababisha Dr.Ulimboka akaonja jahanamu.Binafsi niliupinga mgomo huo lakini kitendo kile cha kuteswa Ulimboka kiliniacha hoi.
  2. Hebu tuangalie sinema ya kutekwa Mo Dewji
  3. Tuangalie kushambuliwa kwa Lissu.
Mifano ipo mingi lakini tuangalie katika hayo machache uwajibikaji wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mahakama.
Tukirudi nyuma tuangalie nini kilifanya Mwinyi ajiuzulu Uwaziri,Waziri wa ofisi ya Rais,Maafisa usalama na maofiasa wa polisi katika mauaji ya Shinyanga. Dhahiri serikali kama serikali ilihakikisha ya kuwa inajisafisha na uchafu huo.

Sina uhakika kama Bagene angefungwa maisha ingekuwa wale wafanya biashara wa madini wangeuawa kipindi hiki na pia sina uhakika kama viongozi wetu wakubwa ambao ni Wacha Mungu wanaweza kubariki haya.
 
Hii ndio Taarifa aliyoisambaza mitandaoni siku ya leo , kwamba kuna watu wabaya wamefika Karagwe kwa lengo la kummaliza , bali amejiapiza kwamba hatokimbia na anasubiri watekeleze Unyama wao .

Binafsi siwezi kupuuza taarifa hii ya kiharamia kutokana na ukweli kwamba sasa tuko kwenye Tanzania mpya ambayo wote waliotoa taarifa za kuwindwa hawakulindwa hadi wakaumia ama kupotea , Lissu na Ben Saa Nane ni mifano halisi , mpaka leo Polisi hawana maelezo yaliyonyooka zaidi ya kumung'unya maneno tu .

Mungu mbariki Baba Askofu Bagonza

Muda mwengine ya serekali achia serekali ya kkkt achia kkkt.bora achague nini kati ya hapo
 
ila kiukweli katika dhambi amabayo imefanya huu utawala kitendo cha kummaliza saanane na lissu kumvunja viungo na wengine kuwamaliza kabisa haitasahaulika wafanye wafanyavyo..hili magufuli ulikosea sana tena sana.
 
Back
Top Bottom