Askofu Benson Bagonza adai kuna wanaotaka kumdhuru, wamefika Karagwe

Ninavyojua Watu wakikuamulia hasa Kukumaliza huwezi kamwe kujua na hata wa karibu yako hakuna ambaye atajua. Sasa huyu Askofu anatuboa!
Lisu alijuaje? Sikia hakuna Siri chini ya Jua YESU ALISEMA YALE YALIONENWA KWA SIRI YATAHUBIRIWA JUU YA MAPAA YA NYUMBA.
 
Kama sifa ya ukristo ni kuona uovu na kuushangilia na kusapoti wanaoufanya Kwa sababu tu wanamamlaka.basi itakuwa ni dini kipumbavu kuliko dini zote duniani
 
An
Anae mlinzi mungu sasa anaogopa nini?
Pia kama hatapeleka taarifa police ni umbea tu kama wa wenzake.
Anataka kutengeneza picha kama la wenzake
Unaleta upuuzi wa kishetani anamwambia Yesu jirushe maana imeandikwa atakutumia malaika usijikwae mguu wako.
 
Chamsingi Askofu atulie kabisa, aachane na kuangaikia binadam wasio na shukrani, asije akapoteza maisha yake bure.
Chamsingi atulie kama wenzake, aendelee na maisha yake, habari za kutetea haki za watu wasiojitambua wala wasiokuwa na shukrani zimepitwa na wakati, kila mmoja apambane na hali yake.
NB: Askofu tulia, kula bata kama maaskof wenzako achana na mambo mengine, utauwawa bure ohooooooo!!!!!
 
Akitorekea Canada sisiem wanakuja kudaia kaenda jela ya kufikirisha. MATAGA ni janga la Taifa
 
Ndivyo anavyowadanganyeni 'Majuha' Wenzake nyie nawe ukiwemo? Sasa kama ana Ushahidi kwanini haupeleki Polisi au hata 'awaanike' tuwajue?
Kumbuka unamzungumzia mtumishi wa Mungu.. we unadhani yule ni Ngumbaru kama wewe mpinga Kristu?
 
A precedence has been set. Any thing is possible in our today's TZ. Achukue tahadhali. Nasi wakosoaji humu JF hatuko salama.
 
Bandiko lako refu linajichanhanya. Unamuunga mtu mkono iwapo umeona uchaguzi wa haki na sio vinginevyo. Iko siku utataka watu wauonge mkono serikali ya kijeshi. Kuingia madarakani kihalali kunakupa haki ya kutaka kuungwa mkono, na sio kinyume chake.
Nani amethibitisha kuwa uchaguzi haukua wa haki?

Ni mbunge yupi ameenda mahakani kupinga matokeo ya jimbo lake ?
Yani watu uchaguzi unakwisha hakuna hata diwani aliyekwenda mahakamani kupinga matokeo ili tupate uhalali wa kuwataja waliohusika kuvuruga uchaguzi!!

Wapinzani wanakua kama walinunuliwa ili wakubali matokeo mpaka ya udiwani na ubunge yanayohojiwa mahakamani!!
Kutoenda mahakamani kutafuta haki ni sawa na kukubali kuwa uchaguzi ulikua huru na haki.
 

Tumeona kwa macho yetu kilichofanyika, ni kweli walipaswa kwenda mahakamani, lakini mahakama zimekubali kutumikia siasa chafu. Hilo limesababisha wapinzani kupoteza imani na hizo mahakama.
 

Nawe kawe mkimbizi ulipwe hiyo $6,000.
 
Mtu mmoja aliacha kuwahubiria kondoo waliopotea na kujiingiza kwenye siasa huku akibaki kuwa na hofu wakati ana Mungu. Naanza kuwa na mashaka naye. Watumishi gani wa Mungu huwa wanaogopa kufa
 
Anatafuta Kiki kwa baiskeli, watu wamekuja kukudhuru na wewe mlengwa una taarifa, halafu umetulia unasubiri wakudhuru, yataka uwe msukule kweli kweli kama mwana saccos ndio uamini [emoji16][emoji23]
 
Tumeona kwa macho yetu kilichofanyika, ni kweli walipaswa kwenda mahakamani, lakini mahakama zimekubali kutumikia siasa chafu. Hilo limesababisha wapinzani kupoteza imani na hizo mahakama.


Hukumu za mahakama ni sheria inayoweza kutumika kwenye jumuiya za madola kutoa hukumu nyingine.
Unafiliri ni Juji gani atatoa hukumu kinyume na sheria iliyopo wazi kama hakuna Contradiction?

Unajua kwa muda mrefu mahakama zilikua zinatoa hukumu za kuilalia serikali. Hata wezi wengi walitegemea kuishinda serikali mahakamani . Kwa sasa mawakili wa serikali wapo makini zaidi .
Jambo la msingi ni ushahidi usio na shaka.

Mfano Lema badala ya kwenda mahakamani yeye amekwenda kuwa mkimbizi Canada.

Mihimili yote inatenda haki tatizo ni watu wanatembea naaamuzi yao mfukoni.

Mtu anasema amekamata kura feki halafu mtu huyo huyo, anachoma moto kielele hicho.
 
Tuko hapa hapa nchini boss, wanachokifanya mahakama tunakijua na kukiona. Kama umeamua kufanya utetezi wa haya yanayoendelea ni haki yako, lakini hilo haliondoi uhalisia wa kile kinachoendelea kwenye hizo mahakama, inapokuwa suala la kutenda haki kwa wapinzani. Kilichofanyika kwenye uchaguzi ule tumekishudia kwa macho yetu. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.

Nimecheka kwa nguvu hapo uliposema mawakili wa serikali wako makini. Sitaki kuharibu utetezi wako, nakushauri shikilia hapo hapo.
 
Askofu anastukia kivuli chake!!
kama kuna usaliti wowote kafanya, afanye toba mapema.

Saa inakuja ambayo kila mtu atalipwa kulingana na matendo yake.

Kofia ya uaskofu haitasaidia wakati ukiwadia.
Extremely well said.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…