Uchaguzi 2020 Askofu Benson Bagonza: Wote Hawaamini

Uchaguzi 2020 Askofu Benson Bagonza: Wote Hawaamini

[emoji23] [emoji23] [emoji23] Katika watu wanaumia katika haya matokeo ni huyu Askofu wangu! Maana yeye alishajichagulia upande toka siku nyingi sana.
aendelee kubip atapigiwa soon kisha akaandike utombolo wake huko atapelekwa
 
Siyo kukubishia baba askofu.

Ni kukuambia kuwa uliyemtaka hajawa, na kwa hili ulikuwa kipofu.

Sisi tuliopiga kura na kupata ushindi tuna furaha kwa kuwa tulichokuwa tunakitaka kimekuwa!
 
Kuna haja ya kupima akili za watu kabla ya kuwapa madaraka makubwa hapa nchini.
Watanzania tumepatikana safari hii, sijui Jakaya anajisikiaje, Mkapa ameshaondoka haya yanayotokea hata hajui pengine angekuwepo angesema neno.
 
Sheikh Ponda na Askofu Bagonza Mungu awapunguzie njaa ili muwaze kwa kutumia ubongo na siyo matumbo, Ameen!
 
Maoni yake tunayaheshimu. Ndo democrasia. Ila ajue tupo tulio amini, tuliofurahi na tunasherehekea.
 
Huwezi kuamini maana kila kitu huwa kina logic yake! Hata mgonjwa anapofariki kwa ugonjwa flani huwa kunakuwepo na historia flani ya kujiridhisha kuwa amekufa kwa ugonjwa husika, otherwise ni kifo cha kutatanisha!

Mwanafunzi anayepa marks chini ya 30% katika mitihani ya kawaida hawezi kuja kupata 98% kwenye mtihani wa taifa, Otherwise ameiba paper!

Vivyo hivyo mwanafunzi anayepata 75% katika mitihani ya kawaida hawezi kuja kupata 0% katika mtihani wa taifa, hili halipo!
Historia ya upinzani inaonyesha kuwa idadi ya wabunge na kura za upinzani imekuwa ikiongezeka kila chaguzi mpya zinapokuja.

Hivyo si rahisi hata kidogo eti chama kilichokuwa na wabunge zaidi ya 40 eti leo kimekosa wabunge kwenye majimbo yote? Mbona wale waliogombea kupitia CHADEMA muhula uliopita kama akina Silinde,Mwambe,Waitara na wengine waliogombea kupitia CCM wamepita?

There are must be something insecret!
 
Maoni yake tunayaheshimu. Ndo democrasia. Ila ajue tupo tulio amini, tuliofurahi na tunasherehekea.
SHEREHE za muda mfupi,kinachokuja ni kilio na kusaga meno.Weka akiba ya maneno.
 
Inashangaza!
tumetulia tulii
tunawasubiri Marekani waje watuamulie watusaidie kupinga matokeo why
Ndivyo mlivyoambiwa na huyo mbelgiji msubiri marekani na huyo beberu lake Amsterdam watakuja kuwapa hi nchi nyie Wana saccos.
Kwa hiyo subirini tuu Lissu ataapishwa kwa lazima iwe isiwe baada ya kichapo kwenye sanduku la kura.
 
Sikia nikwambie, ni ujinga kusema mmeibiwa.

Na hata kama ni kuibiwa basi mnaibiwa kuanzia madiwani, ubunge mpaka Urais tena nchi nzima kila kata?

Na kama ni kweli mmeibiwa basi nyinyi ni wapuuzi, kwanini mnaibiwa kila uchaguzi ilhali mawakala wenu wapo na wanafatilia kila hatua ya upigaji kura?

Kama kweli kila mwaka mnaibiwa na mnakubali kushiriki uchaguzi wa wizi, viongozi wenu wanaakili timamu kwenye vichwa vyao, kukubali kushiriki kwenye uwizi?

Kama kweli mnaibiwa basi mnaibiwa kizembe sana hata mkipewa nchi rasilimali za nchi pamoja na hazina ya nchi itaibiwa kizembe sana kwakuwa hamko makini.

CHADEMA piteni kushoto mtupishe.
CCM tuna jambo letu la kuapishwa kwa Rais JPM.
Mkuu huu utumbo ulio nao akilini kwako utagharimu maisha ya kizazi chako cha kwanza mpaka cha nne, kweli kwa akili yako unaona ni sahihi kwa CCM kukaa bungeni peke yake..
 
WOTE HAWAAMINI...

Na Askofu Benson Bagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe

Waliopiga kura hawaamini,
Waliogoma kupiga kura hawaamini,
"Walioshinda" hawaamini,
"Walioshindwa" hawaamini,
Walioshuhudia hawaamini,
Waliohesabu kura hawaamini,
Wasimamizi hawaamini,
Waangalizi wa ndani na nje hawaamini,
Walinzi wa amani hawaamini,

Kwa nini lakini?

KWA sababu mwaka 2019 baada ya Uchaguzi wa serikali za mitaa,

"Walioshinda" hawakuwa na furaha,
"Walioshindwa" hawakuwa na furaha,
Waliopiga kura, ambao hawakupiga kura, waliohesabu, waliotangaza na waliosikia, WOTE hawakuwa na furaha. FURAHA alipotea, hajarudi. Sasa na IMANI ametoweka.

Usinibishie kwa sababu ubishi ni hulka ya watu waliopoteza furaha na Imani.

Nani anafuata kuwafuata FURAHA na IMANI?

Haiwezi kuwa bora kuliko hii. Kwani hata aloiba haamini.
 
Mkuu huu utumbo ulio nao akilini kwako utagharimu maisha ya kizazi chako cha kwanza mpaka cha nne, kweli kwa akili yako unaona ni sahihi kwa CCM kukaa bungeni peke yake..
Ni bora wakae pekeyao maana wenzao walidai Bungeni kuna Corona.
 
Ni kweli hawaamini bali wanaelewa kilichofanyika.
Wapiga kura wanaelewa
walioshinda wanaelewa japo huenda walioshindwa hawelewi
Tume ya uchaguzi inaelewa
Wananchi wanaelewa japo si wote na si wote wanaweza kuelewa wakati wapo wanaotegemea kuamini badala ya kuelewa
Hapa issue si kuamini bali kuelewa. Kuelewa ni kukidurusu kitu au jambo na kulielewa vilivyo tofauti na kuamini ambako ni kuwa na uhakika wa jambo usilojua kana kwamba unalijua. Hapa ndipo lilipo tatizo. Wanaweza kuamini kumbe wanaamini uongo. Ila wakielewa kikweli kweli, hawana haja wala sababu ya kuamini.
Nadhani hata kuku wanaelewa kila kitu japo hawana uwezo wa kueleza wakaeleweka
Cha mno, wakati ndiyo unaoelewa na soon utasema sijui kama mtaelewa.
 
Back
Top Bottom