TANZIA Askofu Chedieli Elinaza Sendoro, KKKT Dayosisi ya Mwanga amefariki kwa ajali

TANZIA Askofu Chedieli Elinaza Sendoro, KKKT Dayosisi ya Mwanga amefariki kwa ajali

RIP askofu, sote ni wageni kwenye uso wa dunia, tutembee kwa tahadhari sana tunapo ikanyaga ardhi.
Ni bahati mbaya sana ajili za vyombo vya usafiri vimekuwa sababu kuu ya kukatiza uhai, hivyo tahadhari iwe kubwa , heri kuchelewa kufika lakini ufike salama.
Wenyeji tupo-Mashahidi wa Yehova tutarithi majumba
 
Hiyo ya Arusha sioni shida yake sana..

Ukiwa mtu wa Safari sana utaona jinsi watu hasa Mabasi, magari binafsi na Serikali wanavyokimbia bila tahadhari.. mpaka unajiuliza huyu anafamilia kweli..?

Kuna sehemu za kumwaga moto na kuna sehemu za kunyata.. ktk 50 nenda na 50 walioweka wanamaana yao. Mstari upo straight usiovertake tulia..
Kwani huwa wanakimbilia wapi hasa? Kuzimu!!!? Haraka haraka haina baraka
Asilimia kubwa ya ajali ni uzembe
 
Kuna taarita ambayo sio nzuri.

Kuna ajali imetokea Barabara kuu ya Mwanga kwenda Same.

Taarifa zaidi kukufikia mapema

=====

Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chediel Sendoro amefariki dunia usiku huu, Septemba 9, 2024 baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

PIA SOMA
- Rais Samia atoa salamu za rambirambi kufuatia Kifo cha Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga

Chanzo: Gold FM
 
Ni sawa Mkuu ..lakini bado Barabara zimechakaa sana kwa hizo za Dsm-Arusha,Dsm-Mwanza,Dsm-Tunduma

Barabara hizo kuu zilizotajwa ni death traps...hasa ile ya kipande cha Dsm-Moro ni pa hovvyo mno.

Ni umaskini na maamuzi tu wa Nchi kuwa na 4 ways.Kutapunguza sana zile zinazoepukika.

Mtu akitoa nzima nzima huchomoki hata kama ulikuwa unatembea na 20Kms.

Jioni Mkuu utakuwa unajua Fuso zinavyotililka kwenda Mjini Dsm...plus na ubovu wa Barabara.
Ni kweli.. kiufupi Tanzania hakuna barabara nzima au yenye tija.. asilimia 90 ni mbovu na zisizo rafiki kwa vyombo vyetu.

Hiyo njia ya Moro sio kabisa haifai.. unaweza ukawekwa mtu kati na malori mawili mbele na nyuma ndugu zako wakaja kuokota nguo tu kuzika.
 
Kuna taarita ambayo sio nzuri.

Kuna ajali imetokea Barabara kuu ya Mwanga kwenda Same.

Taarifa zaidi kukufikia mapema

=====

Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chediel Sendoro amefariki dunia usiku huu, Septemba 9, 2024 baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

PIA SOMA
- Rais Samia atoa salamu za rambirambi kufuatia Kifo cha Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga

Chanzo: Gold FM
Imetengenezwa?
 
Labda alikua anachat..who knows...
Apumzike kwa amani
 
Ni kweli.. kiufupi Tanzania hakuna barabara nzima au yenye tija.. asilimia 90 ni mbovu na zisizo rafiki kwa vyombo vyetu.

Hiyo njia ya Moro sio kabisa haifai.. unaweza ukawekwa mtu kati na malori mawili mbele na nyuma ndugu zako wakaja kuokota nguo tu kuzika.
Mkuu kabisa.

Moja ya sehemu huwa na adabu iwe mchana au usiku ni hiyo Barabara.

Kiuhalisia Barabara zote zenye T01.....
Ni ziangaliwe ,haziendani na nyakati na zimekuwa death trap kwa mamia ya watu.

Tuna mifano hai mingi..kumbuka enzi za wami pale....
 
Kuna taarita ambayo sio nzuri.

Kuna ajali imetokea Barabara kuu ya Mwanga kwenda Same.

Taarifa zaidi kukufikia mapema

=====

Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chediel Sendoro amefariki dunia usiku huu, Septemba 9, 2024 baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kisangiro wilayani Mwanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

PIA SOMA
- Rais Samia atoa salamu za rambirambi kufuatia Kifo cha Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga

Chanzo: Gold FM
 
Attachments

Askofu alikuwa hana dereva? Mungu anachukua watumishi wema, alikuwa hataki kuchanganya siasa na dini kama Shoo na Kitima wa Chadema
Maaskofu wa aina hii ni wafia CCM! Askofu atakwepaje Siasa!
 
Kati ya watu ambao nikiwa napita zangu nikaona wamepata ajali na mimi nawapita na kuwaacha wafe ni askari jeshi la polisi na wanajeshi wote , madereva wa magari ya serikali na madereva wa mabasi hao nita waacha wafe tuu kwakweli
Sio kwamba polisi wote ni wabaya, au wanaunga mkono ubaya unaotendwa na polisi wenzao hasa wakubwa. Polisi wengine wengi nao ni raia wema, ingawa kuna polisi majambazi na wauwaji. Ni kama wanaccm wapo wema pia, ingawa wengi ni wabaya sana.
 
Katika siku za karibuni, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), haswa katika dayosisi ya Kaskazini, ambapo Askofu Dr. Shoo amepata ugumu wa kutatanisha. Baada ya kumaliza mihula miwili ya kikatiba, sasa ameongezewa muhula maalumu wa miaka sita. Hali hii imeibua maswali mengi miongoni mwa waumini na wachungaji, ambao wanashangaa ni kwa namna gani mchakato huu umepita bila kupingwa.

Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba sheria za kanisa zinapaswa kufuatwa ili kudumisha uwazi na haki katika uongozi. Kila kiongozi anapaswa kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, na waumini wanapaswa kuwa na sauti katika mchakato huu. Uamuzi wa kuongeza muhula wa Askofu Dr. Shoo unachukuliwa na wengi kama uvunjifu wa sheria na kanuni za kanisa. Hii inatoa picha mbaya kuhusu uongozi wa kanisa na inachangia kukosekana kwa imani miongoni mwa waumini.

Ufisadi huu unadhihirisha jinsi ambavyo mifumo ya uongozi inaweza kutumika kwa faida ya mtu mmoja badala ya jamii nzima. Taarifa zinaonyesha kuwa Askofu Dr. Shoo alihonga Halmashauri kuu ya dayosisi ili kuzuia uchaguzi wa wazi na kumpa nafasi ya kuendelea. Hii ni dalili ya wazi ya kukosekana kwa maadili katika uongozi wa kanisa, ambapo viongozi wanatumia mbinu zisizo za haki ili kudumisha madaraka yao.

Wachungaji wengi hawakujitokeza kugombea nafasi ya uaskofu, na hali hii inaweza kuwa ni matokeo ya hofu na kukosa ujasiri. Kutojikita kwa wachungaji katika uchaguzi huo ni kielelezo cha udhaifu wa mfumo wa uongozi wa kanisa. Wanaposhindwa kujitokeza, wanatoa nafasi kwa watu wachache kuamua mustakabali wa kanisa bila ushirikiano wa waumini. Hii inasababisha kukosekana kwa uwakilishi wa kweli wa waumini katika maamuzi makubwa yanayohusiana na uongozi wa kanisa.

Katika mazingira haya, ni muhimu kwa waumini kuchukua hatua. Wanapaswa kuhimiza uwazi katika mchakato wa uchaguzi, kuhakikisha kwamba viongozi wanachaguliwa kwa njia ya haki. Haki na uwazi ni nguzo muhimu katika kudumisha uaminifu na kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na waumini. Hivyo, ni jukumu la kila mwamini kuhakikisha kwamba wanajitokeza na kuleta mabadiliko yanayohitajika.

Kuhusiana na masuala ya maadili, viongozi wa kanisa wanapaswa kuwa mfano mzuri kwa waumini. Kila hatua inayochukuliwa inapaswa kuwa ya manufaa kwa jamii nzima, na si kwa maslahi ya mtu mmoja. Viongozi wanapaswa kutambua kwamba wanawajibika mbele ya waumini wao na kwamba kila uamuzi wanaofanya unapaswa kuwa na faida kwa jamii nzima.

Katika kuangalia mustakabali wa kanisa, ni muhimu kwa waumini kujiuliza: Je, tunataka kuendelea na mfumo huu wa uongozi? Je, hatutachukua hatua kuhamasisha mabadiliko? Ni wakati wa kuanzisha mjadala wa wazi kuhusu uongozi wa kanisa, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata nafasi ya kujieleza na kushiriki katika maamuzi yanayohusiana na uongozi.

Kwa kuzingatia yote haya, ni wazi kwamba kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ili kurejea kwenye misingi yake ya awali ya uwazi na haki. Waumini wanapaswa kuwa na sauti katika mchakato wa uchaguzi na kuhakikisha kwamba viongozi wanawajibika kwa vitendo na maamuzi yao. Hakuna sababu ya viongozi wa kanisa kuendelea kutawala kwa mifumo ya kifalme, ambapo mtu mmoja anakuwa na nguvu za kupitisha maamuzi bila ushirikiano wa waumini.

Kwa kumalizia, ni wajibu wetu sote, kama waumini, kuhakikisha kwamba tunasimama kidete dhidi ya vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu uhusiano wetu na Mungu na kuathiri ustawi wa jamii. Ni muhimu kutafakari kuhusu mustakabali wa kanisa letu na kuchukua hatua zinazohitajika ili kurudisha imani na uaminifu katika uongozi wa kanisa. Kwa pamoja, tunaweza kujenga kanisa linaloheshimu sheria na kanuni, na ambalo linajali waumini wake kwa dhati.
 
Back
Top Bottom