Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Askofu Dkt. Bagonza amshukia Lugola kwa kumfananisha Magufuli na Yesu. Asema hii laana lazima itafune mtu na Taifa

Shida ya Mzee wangu Bagonza amejaa chuki, Chuki Imemjaa hata kwenye vitu vidogovidogo tu.

Unaweza kufafanua hili? How exactly?

Hii kitu ni ndogo? Kumfanya binadamu kuwa ni YESU/MUNGU ni ishu ndogo?

Bishop kaandika kwa lugha rahisi na yenye kueleweka na mifano kadha wa kadha. Lakini Bahati mbaya kwako hujaelewa lolote masikini wa roho wewe....

Maandiko matakatifu ktk Biblia 2KOR.10:3 - 5 yanatuonya na kutuelekeza wakristo kuwa; ".....vita vyetu sisi wakristo SI VYA KIDUNIA (kutumia maguvu ya mwili na damu) bali ni juu ya mashetani, roho wachafu na mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho...."

Ndo kusema kuwa, watu washukuru kuwa sisi wakristo huwa hatupendi ugomvi kama wenzetu wale.....

Maana mahali pengine ktk Biblia Takatifu, Neno (Mungu) anatuelekeza kusema;

"... vita hivi siyo vyenu, bali ni vya BWANA MUNGU mwenyewe...."

Kwa hiyo, laiti kashfa na dharau hii ya KANGI LUGOLA dhidi ya DINI na IMANI ya Kikristo ingekuwa imeelekezwa dhidi ya DINI na IMANI ya wenzetu waislamu, sijui kama ungeandika hivi, na naamini Kangi Lugola angekuwa anaomba radhi huku akilia machozi.....!!

Lakini ashukuriwe MUNGU baba mwenyezi katika YESU kristo kwa sababu hamlazimishi mtu kuamua atakacho yeye MUNGU...

MUNGU katupa utashi wa kuchagua JEMA ama BAYA; UZIMA ama MAUTI. Kangi Lugola ana utashi huo pia. Kama anadhani hakukosea, basi atakuwa kaamua kachagua fungu lake na hukumu yake....

Lakini kwa sasa, kama Bishop alivyosema, laana itamla muhusika taratibu sambamba na aliyefanywa kuwa ni YESU/MUNGU.....
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Absolutely correct Doctor.
Naona mapenzi ya wengine wangependa kuwa na dhehebu la mtu Fulani na awe Mungu na mtume wao.
 
Nimesikiliza mchango wa Mhe. Kangi Lugola kwenye Bajeti Kuu ya Serikali 2020/21 inasikitisha na imekosa focus.
Mhe. Kangi Lugola hakupashwa awe Bungeni huyu Fisadi mkubwa na mlarushwa aliyebobea. Neno la Mungu linasema: AMRLAANIWA AMTUMAINIYE MWANADAMU! Sifa zote alizoimba na mapambio yote kwa Rais Magufuli kiasi cha kumfananisha na Bwana Yesu Kristo hakika ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu na Kangi Lugola atavuna hichi alichopanda maana Mungu hadhihakiwi!
Msamaha wa Rais Magufuli kwa MAFISADI WA CCM ndani ya Jeshi la Magereza chini ya Adengenye na Kangi Lugola ndiko kumepelekea Lugola kumwona Magufuli Kama Mungu wake.....!

Amelaaniwa Kenge huyu.
 
Ndugu wana Jamii Forum. Naomba baadhi ya wachangia watambue sifa zamlokole;
1) Awe amempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
2) Awe na hofu ya Mungu (Kwamba Mungu ni mkuu kuliko mtu yeyote na mamlaka yeyote ya hapa duniani). Kwamba sifa na utukufu vyote anapaswa apewe Mungu muumba mbingu nchi.
3) Awe mtu mkweli kwamba ndiyo yake iwe ndiyo na hapana ya iwe ni hapana. Mlokole hawezi kuzungumzia jambo ambalo hana ushuhuda/ ushahidi nalo.
4) Awe ameachana na mambo ya kidunia kama vile kucheza au kuchezesha maungo yake kwa nyimbo zisizompa Mungu utukufu.
5) Awe na hekima katika kuongea na pia mwenye kuwa na kiasi cha maneno (kutunza maneno ya kinywa chake). Mfano; Kitu fulani kama hakiko hivi natavua nguo hadharani nk.
6) Awe na ushuhuda wa maisha na matendo yake kiasi kwamba jamii inayomzunguuka au jimii ikisikia chochote juu ya maisha wakiri kweli huyu mtu wa Mungu (yaani anawakilisha tabia na sheria ya Mungu ndani yake).

Sifa za mlokole zipo nyingi. Kwa hizi chache zitatoa vigezo vya mtu kuitwa mlokole.
 
Kuna mtu kasema hii kauli angeisema kuhusu waasisi wa dini fulani kungekuwa kumewaka
 
Yesu Ni binadamu kwa 100% sio mungu,MUNGU hawezi kufa.wala kuteswa
Kama unajua na kuaminini kuwa aliteswa na kufa kama base ya hoja yako( Nahisi umesoma kwenye Biblia ambalo ni jambo jema) basi endelea kuisoma na kuimani zaidi Biblia na usiache kusoma na kuamini kuwa Yesu alifufuka na ni Mungu. Ukipakosa mahali palipoandikwa hivyo niambie nikuelekeze.
 
Yesu kwa hiari yake mwenyewe aliruhusu uhai umtoke ili baadaye autwae tena, hili neno alilitoa kwa baba. Kwa hiyo mkata mauno anaweza kututhibitishia kwamba bwana yule alishawahi kuutoa uhai wake na akautwaa tena, au na yeye bado anapalilia kale kamsamaha ka bwana adwengenye..teh..teh..
 
Kama unajua na kuaminini kuwa aliteswa na kufa kama base ya hoja yako( Nahisi umesoma kwenye Biblia ambalo ni jambo jema) basi endelea kuisoma na kuimani zaidi Biblia na usiache kusoma na kuamini kuwa Yesu alifufuka na ni Mungu. Ukipakosa mahali palipoandikwa hivyo niambie nikuelekeze.
Kwani maandishi Ni Nini? Si wameandika tu watu
 
Bagonza anafikili anaweza kuchukua nafasi ya mungu? Hawezi ku finally hukumu ya mungu kwa binadamu hata siku moja, pia akumbuke kuna watu wanaitwa yesu hapa duniani kwa maana hiyo hao hawatasamehewa kwa vile wamejiita jina la yesu?

Pia lazima ajue mfano sio lazima iwe kitu halisi,
Ujuaji anaotaka kujifanya anao Bagonza unamuondolea hadhi ya kuwa Askofu.

Kuna wanasiasa wanasema uongo na anajuwa wanasema uongo na wengine ni waumini wake mbona hatujaona andiko kuwakemea ili waache uongo kwa kuwa vitabu vya dini vinasema usimsemee mtu uongo, pia uongo ni zaidi ya mchawi, sasa hilo halijui?

Mapenzi yake kisiasa hayamzuii kuacha uaskofu ili aje apambane kama mwanasiasa kwa kuwa yeye hatakuwa wa kwanza, kuna Dr slaa, kuna marehem rwakatale kuna msigwa na wengine wengi.
Yeye anashambulia upande wa CCM tu je huko Upinzani ni watakatifu?

Maaskofu wa hivi laana zao watazibeba wenyewe maana mungu anaiona mioyo yao inavyohangaika na maovu wanayowaza kika siku.
Bagonza ajitathimini.
Askofu Bagonza ni kweli kabisa umefika wakati kwake kuvua majoho ya uaskofu na kupanda jukwaani.
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___________
Kufuru haina kinga. Kwa Wakristo, dhambi isiyosameheka katika Agano Jipya ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Na katika Agano la Kale ni ibada ya sanamu (idolatry). Amri ya kwanza aliyopewa Musa inasema, "Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine" (Kutoka 20:3-6).
_
Kufuru haina kinga duniani wala mbinguni. Ghadhabu ya Mungu iko wazi katika vitabu vyake vyote.

Tuzitendee haki kumbukumbu zetu;

1. Mwaka 2005 mjinga mmoja alitumia uhuru wake vibaya huko Denmark. Akachora katuni yenye kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W). Dunia nzima iliwaka moto.

2. Mwaka 2010 mpuuzi mwingine huko Marekani akachoma moto Quran tukufu. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe.

3. Mwaka 2012 huko Mbagala utoto ukavuka mipaka. Msahafu ukakojolewa. Amani yetu ilitoweka kwa muda. Majivu yakawa majivu.

4. Huko Sumbawanga, msimu wa uchaguzi kama huu, ulimi wa mmoja uliteleza. Akaufananisha UTATU mtakatifu na mafiga matatu ya chama chake. Hapakutosha. Mzee Pinda (mtu wa amani), ana cha kusimulia mpaka leo.

Mungu wetu hafananishwi. Mungu wetu halinganishwi. Mungu wetu hashindanishwi. Ni ibada ya sanamu kupenda kitu kingine kuliko unavyompenda Mungu wako. Ni ibada ya sanamu kuchukia kitu kingine kuliko unavyomchukia shetani. Ni ibada ya sanamu kumlinganisha Muumbaji na uumbaji wake.

Hatumtendei haki Mungu kumlinganisha na aliowaumba. Hatuwatendei haki wale tuwapendao kwa kuonesha kuwa tunawapenda kuliko tunavyompenda aliyewaumba.

Walinzi na waangalizi wa imani (viongozi wa dini), kama hatuwezi kukemea hili (la Lugola) basi angalau tuchukie na tuonekane kweli tumechukizwa.!
Hatuwezi kunyamazia upuuzi wa wabunge kumfananisha mtu na Mungu kamwe hatuwez, hii ni kufuru ngoja tumwombe Mungu atajibu tu
 
Shida ya Mzee wangu Bagonza amejaa chuki, Chuki Imemjaa hata kwenye vitu vidogovidogo tu.
Siyo chuki, ni upendo na unazi alionao kwa CHADEMA! Yeye kwa mawazo yake anaona Chadema ndiyo inastahili kutukuzwa! Nina hofu siku CHADEMA ikifa (baada ya uchaguzi mwaka huu) Askofu anaweza akapata ugonjwa wa moyo.
 
Teteh!
Huyu ni askofu aliyemkabidhi kanisa shetani kipindi corona!
Na tumkubushe huyo askofusiasa kuwa Lugola alilenga zaidi matendo
 
Utatu mtakatifu ni mambo yaliyosukwa tu na wajanja! Kamwe huwezi kumgawa Mungu eti nafsi tatu!! Najibu swali! Alimlinganisha JPM na Yesu (nabii) kwa kuwa amejitoa mhanga kama Yesu alivyoteseka ili kuukomboa ulimwengu. Anaikomboa Tz kutoka mikononi mwa mafisadi. Ni hatari kwake ila amejitoa mhanga.
Wewe mpuuzi. Imani kitu kingine, wewe unayepiga foleni kuabudu jiwe uko sawa? Ile si imani yako?
 
Kwanza Yesu ana nafsi mbili "Umungu na Ubinadamu" JPM ni nafsi moja - Ubinadamu huoni JPM ni mkombozi wa Tz?
 
Back
Top Bottom