Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo: Kunyamaza wakati mwingine ni hekima

.... wameanza tabia ya kukimbilia mitandaoni kila siku, haswa huyu Munga, sijui ana shida gani haswa!, maana kama Pengo kwa mtazamo wake ndio uliomlazimu kusema vile, huyu Munga ni nani mpaka aingilie uhuru wa mwingine kutoa maoni yake!, au mpk aongee vile unavyotaka ndio uone ameongea vizuri?!, hekima ni kukaa kimya, mimi kwa upande wangu niko na wale wanaokaa kimya, vinginevyo hapa itageuka ukumbi wa taarabu na hilo kanisa litadharaulika, vyema kuwa makini sn tusichotwe na matakwa na utashi wa wengine kwa mapenzi yao binafsi.
 
Munga ni nani hadi azuie watu kutoa maoni yao ??
Kuna maoni gani waliyoyatoa pale? Upofu wa akili huzuia kichwa kufikiri na badala yake tumbo huchukua nafasi ya tumbo! Huo ni ulemavu ukiokithiri na hauna dawa! Yaani hujui tofauti ya kusifu na kutoa maoni? Kata huo m-bichwa uutupiwe nguruwe!
 
Huyu pengo anatuharibia kanisa. Baba mtukufu tunaomba utuondolee mapema huyu mnafiki.
 
Haki huinua taifa
 
Niliwahi kumnukuu humu Lord Thatcher, mume wa Margaret Thatcher..."ni bora kukaa kimya watu wakakuona mpumbavu kuliko kuongea na watu wakathibitisha kweli wewe ni mpumbavu" (ni tafsiri yangu isiyo rasmi). Viongozi wa dini hata kama wamestaafu wawe waangalifu na maneno yao.
 
..... hawa maaskofu wa mitandaoni hawa!, Asante Mungu wengine hawawajibu.
 
Mungu ambariki sana huyu Askofu. Katika huu ujumbe inapatikana hekima ya pekee.

Shukrani na utukufu umrudie Mungu wetu.
 
Bavicha akili zenu zinajua kupiga deki barabara
Mbona kawaida tu! La kushangaza hapo ni lipi? Kwani lami nauhitaji kusafishwa kwa maji? Au wewe unaishi mavumbini? Karibu mjini ushangae!
 
..... kama Munga kashindwa kuheshimu maoni ya wengine kwa nini maoni yake yaheshimiwe?, hayo maneno aliyotumia ukaona ni dharau au kiburi yamesababishwa na huyo Askofu kila siku kushinda mitandaoni kusema wengine, huyo ulie m_quote wala hana kosa, chanzo ni huyo Askofu wenu mjuaji, kila siku kusema sema wengine tu!
 
Mimi naona wanaheshimiana. Lugha aliyotumia Askofu Mungu inaonesha kabisa kwamba anamheshimu.
.... huyo Munga ni mnafiki, nikimsoma kwenye andiko lake kasema.. "ndugu zangu viongozi wa dini akiwemo Askofu NILIYEMHESHIMU sana Pengo" halafu mbele anasema NITAENDELEA kumuheshimu!, hii maana yake nini? niambie matumizi ya maneno NILIYEMHESHIMU na NITAENDELEA kumheshimu ni sawa?

...Kuna lake amelificha moyoni, bahati nzuri kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake, muache kumtetea atawapeleka wote gizani!
 
Natamani nikushike mkono ila ukombali nami, itoshetu kusema manano yako yataishi katka taifa hili, hata yule asietaka kuyakubali mwache andelee kushupaza shingo yake.
 
Duuh huyu ndiyo yule anayewashitaki kondoo wake mahakamani??
 
....juzi Askofu wa Katoliki katoa maoni yake, akatokea tena mwingine upande huo huo anapinga, hivi nyie ni nani mnaotaka kufunga midomo wengine nchi hii, jifunzeni kukaa kimya, msitake kufanya wengine wajinga na mitandao yenu.
 
Aisee! Hivi ukikosoa maoni yangu maana yake ni kwamba umeyadharau/umeshindwa kuyaheshimu? Ni kweli hatuwezi kutofautisha kati ya kuheshimu na kukosoa. Askofu Munga amekosoa hayo maoni kwa lugha ya unyenyekevu mno. Hakuna sehemu ktk bandiko lake nimeona lugha ya dharau.
 
....Munga sio Mungu!, lugha ipi ya kinyenyekevu inayojichanganya changanya, fungua macho yako vzr soma andiko la askofu wako!
 
....Munga sio Mungu!, lugha ipi ya kinyenyekevu inayojichanganya changanya, fungua macho yako vzr soma andiko la askofu wako!
Nimesoma vizuri, na nimeona hayo maneno, "niliyemheshimu" na " nitaendelea kumheshimu"
Bado sijaona dharau hapo. Ur making a mountain out of a molehill.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…