Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo: Kunyamaza wakati mwingine ni hekima

Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo: Kunyamaza wakati mwingine ni hekima

unajua serikali ya ccm inajua sana kucheza na akili za wananchi wake.

hapa tumamuona askofu mtu wa maana kishenzi.hasira zinapoa baada ya kuona kumbe kuna watu wa kutusemea upende wetu.

na hapa ndipo mnapopigwa.
Tema huo ugoro unaokula alafu tulia dawa ikuingie.
 
Mpigania Demokrasia anayetaka watu wote waone kama anavyoona, wafikirie Kama anavyofikiria yeye na watende Kama anavyotenda. Watu wa hivi ni watu wabinafsi na siku zote maisha yao huwa ni ya hovyo, chuki na sonono zisizoisha. So long sisi ni binadamu Basi ifahamike kuwa tunao utashi ambao unatuwezesha kufikiri na kuona tofauti, unachokiona kibaya siyo lazima watu wote wakione hivo, unachopaswa kufanya ni kubaki na msimamo wako lakini usiwachukie wala kuwalaumu wanaoona tofauti nawe.
Kama anavyokesha akikosoa Serikali ya JPM kwakuwa anaona haitendi vile angependa itende kiru ambacho kimsingi ni haki yake, Basi anapaswa aache na wengine wanaoona waisifie Serikali ya JPM wasifie, kwani wao wameamua kufanya hivo na wanasababu zao Kama vile ambavyo yeye ameamua kwa sababu zake kuwa mpingaji.
Katika Nchi yenye watu Million 60 yeye ni nani hadi ajipe usahihi, kwamba anachokiona, kuwaza na kutenda ndicho watu wote milioni 60 wanapaswa kuona, kuwaza na kutenda. By the way who is Steven Muga in this Country, to whom does he have Command, yes, Kuna wakati unaweza kukosa uhalali wa kuwafanya watu wafuate mawazo yako na maono yako kupitia ushawishi lakini ukaweza kwa kutumia nguvu ulizonazo kouchumi, kisiasa au kijamii. Muga Legitamacy yake ipo wapi, Kama Muasham Kardnal Pengo ameona tofauti na yeye, Muga ana nguvu gani ya kiushawishi dhidi ya Kardinal Pengo ya kumfanya aone kama yeye, maana hadi hapo nguvu ya hoja ameshashindwa ndio maana Kardinal Pengo bado anaona tofauti naye pamoja na maandishi yake ya kila kukicha kukosoa.
Yeye abaki na msimamo wake awaache wenye misimamo tofauti na yake nao wafanye kile wanachokiona!
Duh! Yaani kwako wewe kumkosoa na kuonesha dharau kwa Askofu Munga ni sawa.Lakini yeye Askofu Munga kumkosoa Pengo ni dhambi isiyosameheka. Hii ni ajabu sana.

Umeongea habari ya utashi kwamba binadamu tunao utashi wa kuchagua tunacholipenda. Ni kweli hujakosea. Sijaona mahali Munga amelazimisha mtu yeyote aone kile anachokiona ni sahihi kwake kiwe sahihi kwa kila mtu. Ametoa maoni yake kama vile na wewe unavyotoa yako kupingana naye.

Umeuliza Munga ni nani nchi hii, ana nguvu gani ya ushawishi, legitimacy yake iko wapi kulinganisha na Pengo?
Maswali kama haya ni ya watu wanaojiona bora kuliko wengine, wenye dharau na ambao hawana uvumilivu wa kuona wengine wakisema tofauti na wanachokiamini. Unaona Munga si kitu kwako lakini bado unasumbuka kuandika post ndeeefu ya kumkosoa. Ungempuuza tu kama aliyosema hayana maana kwako.

La mwisho ambalo nakubaliana na wewe umesema Munga abaki na msimamo wake na awaache wengine na misimamo yao. Uko 100% sawa. Na msimamo wa Munga ndio huu ambao umekupa shida wewe. Umesema jambo ambalo hata wewe limekushinda kutekeleza.
Tukubaliane kutokubaliana na maisha yaendelee.
 
Hakuna mtu au kitu chini ya jua au mbinguni kinachochukia kusifiwa, mtu akikusifu kuwa wewe ni tajili hata kama huna kitu utanyamaza au utatabasamu lakini akisema wewe masikini na unajua wewe ni masikini lazima utanuna na kuona kakukosea wakat kasema ukweli, sasa kusifu sio dhambi, ili kudhauliwa ndo dhambi, kwani hata mungu anapenda kusifiwa ingwa unaweza kuwa umempoteza mpendwa wako lakini bado utasifu tu kwamba ni mapenzi yake mungu, ulishawahi kuona mtu anamtukana mungu kwenye msiba?
Kusifiwa na sifa za kike na mtu aliyeruka stage.Mwanaume kamili akamilishwi kwa kusifiwa
 
Askofu Munga amepoteza mwelekeo

sasa Hajui ashike lipi kati ya dini na siasa
2019 Imeisha

-Soko la Korosho limeharibiwa

-Ajira Sekta rasmi na sekta binafsi zimeshuka

-Hali ngumu ya Maisha Maradufu

-Uchaguzi Serikali za Mitaa Umeharibiwa

-Kuna Hatari kutokea Janga la Njaa Kanda ya Kati

-Katiba Inavunjwa na kubakwa Mchana wa Jua Kali

Hiyo ndiyo 2019
 
Askofu Munga kamfanya Kadinali Pengo mbuzi wa kafara

au 'kill off’ kama sio 'care off' kufikisha Ujumbe wake kwa walengwa wake

..haya Bashite na Baba yako askofu ananungunika kwa namna mnavyoendesha Lori lenu
 
Inamhusu sana tu, tatizo uzi ukiwa mrefu hamsomi. Mnakimbilia ku- comment kwenye post za wachangiaji. Soma alichoandika huyu Askofu Munga halafu ndiyo ueleze ni wapi naye alitakiwa akae kimya.
Muda wenyewe ukwapi boss! Tunasoma heading, tunareply...
 
Back
Top Bottom