Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo: Kunyamaza wakati mwingine ni hekima

Kumbe ndo maana kakosa maadili ya dini ya kushauri kwa staha yeye kahamia mitandaoni kutafuta uungwaji wa wananchi? Aludie maadili ya jinsi ya kuwashauli watawala kama mungu alivyosema, akishindwa ndo aje huku tena ayaseme kanisani kwake sio mitandaoni, kwa kuwa hao serikari wanasali humo kanisani mwake na pia wahalifu nao wamo. Wakiokoka kila kitu kitakuwa sawa.

Vipi hao wanaosifia wanaogopa kuhojiwa uraia wao,au makandokando yao ya upigaji kupitia misamaha ya kodi
 
Kama Askofu Munga anaona kunyamaza pia ni Hekima, kwa nini yeye hanyamazi kihele hele kila kukicha. Kwanza hana hadhi ya kumjibu Kardinali Pengo maana huyo si level yake
Musiba awatoshi mmeongeza na pengo ahalilishe nyekundu kuwa blue,uzuri watz si watoto wanamacho yote awahitaji kina pengo kuwaonyesha njia
 
BABA ASKOFU ,
KUMBUKA WOTE ULIOWASHUGULIKIA WALIPOKUTAKA KUKUREKEBISHA ....WOTE WALIPOTEZA NYADHIFA ZAO NA WENGINE KUSIMAMISHWA UCHUNGAJI)
MAMLAKA YA KUHOJI UNAYATOA KWA NANI KWA UTARATIBU UPI?MAANA MWENYE KUHOJI ANA MAMLAKA YA MAMUZI JUU YA MHOJIWA
KIMYA NI HEKIMA JE WW UMEKAA KIMYA?
WEWE NA KADINALI WOTE MNASAIDIA KUYUMBISHA WANANCHI NA VIONGOZI,CHUNGENI NDIMI ZENU
 
Pengo ni mjaalaana kama BASHITE. Wote wawili wamelaaniwa mbinguni na dunianuani.
Achana nao hao baba Askofu Munga.
M/Mungu akutangulie nabii wake wa kweli.
Asante kwa mawaidha yaliomema kabisa kabisa.
 
Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo

KUNYAMAZA WAKATI MWINGINE NI HEKIMA

Waungwana taifa la Mungu, someni hii kwa furaha na uvumilivu.

"Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi. Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu.

Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kwenda haja. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana. Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri. Lakini baadaye, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaruhusu kumshambulia Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake.

Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hadi chini, akamsujudia."
(1 Samweli 24:1-8).

Nimeleta maneno haya kutoka biblia ili niseme jambo muhimu kwa wakati wetu. Natumia maneno haya baada ya kusikiliza mazungumzo ya baadhi ya viongozi wa kiimani katika mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Ni baada ya kupokeo vipande vya video ( video clips) na kuvisikiliza pia mitandaoni.

Kama kawaida nilishikika na majukumu kwa hiyo sikuweza kufuatilia mkutano huo kwa karibu na hivyo nisemalo hapa si juu ya mkutano mzima bali ni juu ya "clips" nilizosikiliza. Nimemsikiliza kwa makini na kwa maoni yangu wenzetu walizungumza kupitiliza (they overstated matters). Ni mitazamo yao na kamwe sio mitazamo ya viongozi wote wa kiimani. Hata hivyo, niliyosikia yanasaliti ukweli wa mambo kama nitakavyoeleza.

Awali ya yote niweke wazi kwamba mashaka katika mazungumzo niliyoyasikiliza sio ya ama Mhe. Magufuli, Rais wetu au Comrade Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Shida ni waliozungumza kwa kujipendekeza na kupendezesha kwa maslahi binafsi. Najaribu kuwa mwaminifu katika hoja hii.

Nijieleze kidogo hapa. Niseme wazi kwamba kisera mimi nilikuwa mfuasi wa CCM. Uchungaji na Uaskofu ndivyo vimeninyang'anya haki hiyo. Nimemwita Mhe. Makonda Comrade kwa sababu mimi nilikuwa CCM mpaka nilipowekwa wakfu kuwa Mchungaji. Mimi nilikuwa ile CCM ya Mwalimu. Hata hivyo, baada ya hapo na hata kuwekwa wakfu kuwa Askofu nilishirikiana na makomredi Marais na Makatibu Wakuu na Makatibu wa CCM mkoani na wilayani kwangu.

Nilifanya hivyo kwa sababu katiba na sera za CCM zilisimama katika misingi ya haki na kuheshimu utu wa mtu. Zaidi ya yote ni CCM iliyoongoza mchakato wa utawala wa kidemokrasia na hivyo kufungua milango ya siasa za ushindani kwa kuruhusu kuanzishwa kwa vyama vingine vya siasa. Nakiri wazi kwamba nimekuwa karibu na viongozi wa juu wa CCM kwa muda mrefu na Comrade Makamba na Kinana ( schoolmate) ni mashahidi.

CCM imefanya mazuri mengi na makosa mengi katika nyakati tofauti lakini mtazamo wake wa nia ya kujisahihisha iliyorithi tangu Baba wa Taifa ndiyo uhai wake ulioleta matumaini. Kwa hiyo CCM ndiyo iliyozaa demokrasia ya vyama vingi.

Tena tukumbuke kwamba wakati ule kura za kukubali demokrasia ya vyama vingi hazikutosha lakini CCM ikachukua maamuzi magumu ya kuruhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Inakuwaje leo CCM inakula mtoto iliyomzaa kwa kukandamiza demokrasia?!

Someni vizuri "postings" zangu. Sijawahi kumsema neno lolote Mhe. Magufuli. Mimi ni nani hata nimseme mpakwa mafuta wa Bwana?! Mhe. Magufuli ni mtawala wa nchi ya Tanzania. Kwangu mimi yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.

Anafanya mazuri na anafanya makosa lakini hukumu yake imo mikononi mwa Mungu. Watanzania fahamuni kwamba alipoapishwa Mhe JPM mlimuweka mkononi mwa Mungu na kwamba Mungu ahukumu juu ya mambo yake. Nimejizuia sana kutosema neno juu ya Mhe. JPM hadharani kwa sababu ni mpakwa mafuta wa Bwana.

LAKINI LIKIWEPO NENO LA MOJA KWA MOJA LA KUMWAMBIA TOKA KWA BWANA NITAFANYA HIVYO NA KAMWE HAKUNA WA KUNIZUIA. Ila hapa namhoji Muadhama Pengo katika mkutano ulioitishwa na komredi Makonda, je, uliyoyasema na kuyatukuza yametoka kwa BWANA?!

Sasa nirudi kwenye somo. Wenzangu viongozi wa kiimani mliohudhuria mkutano ulioitishwa na Komredi Makonda na kupewa nafasi ya kuongea, kwa kweli mlijipendezesha. Sijui huko kwenu kiapo cha kichungaji kikoje. Huku kwetu kiapo hicho kinamdai Mchungaji aseme kweli hata kama amekaa mezani, akila chakula na Kaisari, kilichoandaliwa na Kaisari, lakini amwambie Kaisari mambo yake kwa kweli yote.

Huu ni mfano wa Yohana Mbatizaji aliyekaa chakulani na Herode, akila chakula cha Herode, lakini akimwambia Herode maovu yake. Yohana alimwambia Herode kwamba Herodia mke wake, si mke wake kihalali bali alitumia mamlaka yake kumnyang'anya Filipo (ndugu yake) mke wake. Kwa maneno mengine Herode alitumia vibaya mamlaka aliyopewa na Mungu kuwadhalimu mpaka ndugu zake. Ilimgharimu Yohana maisha yake lakini alitimiza utume wake.

Ndugu zangu viongozi wa kiimani, akiwemo mtumishi niliyemheshimu sana, Muadhama Pengo, mmesema kwa kusifu kulikopitiliza mipaka (you overstated the matters you stated). Tanzania ilikuwepo kabla ya Mhe. Magufuli na itakuwepo baada yake. Tanzania sio mali ya mtu awaye yeyote bali ni mali ya Mungu mwumbaji wa mbingu na nchi. Muadhama Pengo umetoa kauli tata zinazoweka utukufu kwa wanadamu na si kwa Mungu.

Wengine waliozungumza naweza kuwapuuzia mbali lakini wewe kutamka maneno yale sikutegemea! Mkumbuke Yesu Kristo aliyeungama maungamo mazuri mbele ya Pilato pasipo kuyumba. Huyu Kristo hakumpendezesha Pilato ili ahurumiwe na kupendelewa. Mtasimamaje mbele zake Kristo siku ya hukumu?! Kwa machozi baada ya kukusikiliza namwachia Bwana Yesu ahukumu juu yako.

Mimi kamwe sitasema neno lolote la hukumu. Wewe ni mtumishi na wakili wa siri za Mungu sina neno la kusema juu yako bali namwachia Kristo aliyekuita wewe na mimi katika utume huu. Wakati mwingine ni heri kunyamaza kuliko kusema na kupitiliza hata kukufuru.

Muadhama Pengo nitaendelea kukuheshimu kwa namna ile Daudi alivyomheshimu Sauli. Daudi alikuwa na nafasi ya kumuua Sauli lakini alitambua mipaka ya uwezo wake. Mimi sitakuhukumu na wala sitakujakaa nimhukumu Mheshiwa sana JPM kwa sababu najua dhahiri kwamba ni Mungu atakayemhukumu kwa mambo yote yanayotokea katika taifa hili la Mungu.

Nafanya hivyo kwa kukumbushwa na Daudi akiwa katika hali ngumu ya kuwindwa na Sauli aliyetaka kumuua Daudi. Lakini Daudi akawaonya watu wake akisema:

"Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA. Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaruhusu kumshambulia Sauli."

Nitaendelea kumheshime Rais wangu JPM na sina kibali cha kumhukumu lakini CCM inakandamiza vyama vya upinzani na yeye kama Mwenyekiti wa CCM arejee maamuzi ya CCM kuruhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Akisha kufanya hivyo aangalie faulu zilizofanyika katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Anapoyafanya hayo, yeye kama muumini wa kanisa katoliki aongee na Mungu aliyempa kibali kutawala nchi hii na kuona kama ametenda haki. Mungu ndiye atakayehukumu lakini kwa haya niliyoyasema damu yake haitadaiwa mikononi mwangu. Hapa nasimama, Mungu nisaidie.

+Askofu Stephen Munga
KKKT
Kunyamaza saa ingine ni hekima mbona wewe umesema na unataka wenzio wakae kimya, halfu wewe kila jambo unataka uwe unatoa maoni mbona huheshimu mawazo ya wengine.
 
Level yako Baba Askofu Ni ya chini sana. Kardinal Pengo huwezi kukaa meza moja naye. Na siku Zote jitahidi kutake things within the context. Pole kwa kuwa mropokaji kuliko huyo uliyemuandikia Gazeti hapa.
 
Kama Askofu Munga anaona kunyamaza pia ni Hekima, kwa nini yeye hanyamazi kihele hele kila kukicha. Kwanza hana hadhi ya kumjibu Kardinali Pengo maana huyo si level yake
Pengo ni Askofu tu kama maaskofu wengine, labda level anayowazidi wenzake yeye ni Agent wa kitengo.
 
Mpigania Demokrasia anayetaka watu wote waone kama anavyoona, wafikirie Kama anavyofikiria yeye na watende Kama anavyotenda. Watu wa hivi ni watu wabinafsi na siku zote maisha yao huwa ni ya hovyo, chuki na sonono zisizoisha. So long sisi ni binadamu Basi ifahamike kuwa tunao utashi ambao unatuwezesha kufikiri na kuona tofauti, unachokiona kibaya siyo lazima watu wote wakione hivo, unachopaswa kufanya ni kubaki na msimamo wako lakini usiwachukie wala kuwalaumu wanaoona tofauti nawe.
Kama anavyokesha akikosoa Serikali ya JPM kwakuwa anaona haitendi vile angependa itende kiru ambacho kimsingi ni haki yake, Basi anapaswa aache na wengine wanaoona waisifie Serikali ya JPM wasifie, kwani wao wameamua kufanya hivo na wanasababu zao Kama vile ambavyo yeye ameamua kwa sababu zake kuwa mpingaji.
Katika Nchi yenye watu Million 60 yeye ni nani hadi ajipe usahihi, kwamba anachokiona, kuwaza na kutenda ndicho watu wote milioni 60 wanapaswa kuona, kuwaza na kutenda. By the way who is Steven Muga in this Country, to whom does he have Command, yes, Kuna wakati unaweza kukosa uhalali wa kuwafanya watu wafuate mawazo yako na maono yako kupitia ushawishi lakini ukaweza kwa kutumia nguvu ulizonazo kouchumi, kisiasa au kijamii. Muga Legitamacy yake ipo wapi, Kama Muasham Kardnal Pengo ameona tofauti na yeye, Muga ana nguvu gani ya kiushawishi dhidi ya Kardinal Pengo ya kumfanya aone kama yeye, maana hadi hapo nguvu ya hoja ameshashindwa ndio maana Kardinal Pengo bado anaona tofauti naye pamoja na maandishi yake ya kila kukicha kukosoa.
Yeye abaki na msimamo wake awaache wenye misimamo tofauti na yake nao wafanye kile wanachokiona!
 
hahaha dogo unanitahidi kupost ila nikukumbushe waliwahi kuwepo wenzio wanapost zaidi yako yaani ilikua balaa but leo hawapo, so take care, njaa mbay vidole vitaota kutu
Kweli kabisa hivi akina Lizabon walikwenda wapi
 
Level yako Baba Askofu Ni ya chini sana. Kardinal Pengo huwezi kukaa meza moja naye. Na siku Zote jitahidi kutake things within the context. Pole kwa kuwa mropokaji kuliko huyo uliyemuandikia Gazeti hapa.
Pengo ni Àskofu sawa na wengine usijitowe akili, ukadinali na nafssi tu ya kupiga kura kwenye conclave. Hats padre au shemasi anaweza kuteuliwa kuwa kadinari, umeelewa wewe kilaza?
 
Nimemkumbuka kadinali kwenye issue ya mahakama ya kadhi!!!
Mimi ni nani hata niwaamulie waamini wangu.................................................................
 
Wewe kigori VP kumuita mtu dogo wakati humfahamu ni kielelezo cha ujinga na sonona ilikomaa

Siku ukivunja ungo ndio utafahamu mm ni zaidi yako

State agent
Dogo wewe mwendawazimu kweli, hapa ndio nimetambua huna akili na waliokupa kazi ya kuposti humu mnafanana.
 
BABA ASKOFU ,
KUMBUKA WOTE ULIOWASHUGULIKIA WALIPOKUTAKA KUKUREKEBISHA ....WOTE WALIPOTEZA NYADHIFA ZAO NA WENGINE KUSIMAMISHWA UCHUNGAJI)
MAMLAKA YA KUHOJI UNAYATOA KWA NANI KWA UTARATIBU UPI?MAANA MWENYE KUHOJI ANA MAMLAKA YA MAMUZI JUU YA MHOJIWA
KIMYA NI HEKIMA JE WW UMEKAA KIMYA?
WEWE NA KADINALI WOTE MNASAIDIA KUYUMBISHA WANANCHI NA VIONGOZI,CHUNGENI NDIMI ZENU

Baba askofu usomapo uzi huu rudi jukwaa hili ukanushe kama kweli uliwashughulikia na kuwapokonya watu nyazifa zao baada ya kukurekebisha? Na kama ndio basi huna haki ya kukosoa serikari maana wewe pia hukutumia busara kuwasamehe au kujibu walicholalamikia hao uliowapokonya nyazifa zao kwani hata wewe ni binadamu tambua hao wana familia pia. Niliwahi kuuliza je wewe upo tayari kuulizwa maswali juu ya utendaji wako pamoja na matumizi ya sadaka? Kama ndio rudi hapa utwambie ulishafanya mara ngapi kuwapa waumini wako nafasi ya kukuhoji?
 
Back
Top Bottom