Askofu Dr Stephen Munga amuonya Kadinali Pengo: Kunyamaza wakati mwingine ni hekima

Umetimiza wajibu wako BABA ASKOFU na DKT. Umevitendea haki vyeo vyako vyote, cheo cha elimu ya Udaktari (PhD) na cheo cha UTUME (Uaskofu). Ombi langu ni kwamba endeleeni kujitolea kuomba rehema kwa Mungu maana vinginevyo hasira ya Mungu atawaka juu ya nchi hii na maangamizi yapo mlangoni. Kuna maovu ya kutisha yanafanyika katika nchi hii kwa mkono wa huyu mhe
Umenena vema Baba Askofu. Umevitendea haki vyeo vyako vyote. Cheo cha Utume (Uaskofu) na Elimu yako ya Udaktari wa Falsafa. Ombi ni moja kwako na kwa wengine wenye ufunuo kama huo. Ni kuomba rehema usiku na mchana kulinusuru taifa hili. Kuna unyama wa kutisha unafanyika, dhuluma kubwa, umwagaji damu, uonevu, na mengine mengi. Bila ninyi watu wa Mungu wenye maono kama haya kusimama kwa nafasi yenu, hasira ya Mungu itawaka wakati wowote katika nchi hii. Ni hasira kali! Mungu hadhihakiwi. Tusijisahau tukafikiri wale walioangamizwa siku zile kabla yetu walifanya mabaya zaidi yetu, la hasha. Imeibuka hali ya kujisahau sana hata kwa viongozi wa Kiroho.Kiimani na kuona kama vile wanamtumikia binamu yao vile. Hadi unashangaa. Watu wako tayari kumsifia shetani mbele ya wenye mamlaka eti wanaona wapo salama sana wakiwa na uhusiano wa kujipendekeza kwa wakubwa wa dunia hii. Baba, thawabu yako ipo mbele. Songa mbele ukimtetea kristo kama wale Mitume wa zamani. Mwanadamu ni nani hadi umwabudu? Ee Mungu uturehemu.
 

Aya yote yanatoka wapi tatizo letu sisi watanzania tunapenda kusikiliza kile tunachopenda kusikia

Kifupi kila mtu ana haki ya kusema ama kutoa mawazo yake binafsi sio kazi yako wewe unayeyapokea haya mawazo kulazimisha yanane na ya kwako

Sikubaliani sana rafu za kisiasa zinazofanywa na CCM ila tujenge utamaduni wa kuheshimu mawazo ya watu wengine japo hayatupendezi

Kusema sema huku na kutuma nyaraka ndefu kwenye mitandao ya kijamii hazisaidii simameni kwenye mimbari muwafunze waamini wenu otherwise kinachofanyika sasa ni kutaka umaarufu tu
 
Askofu Munga amepoteza mwelekeo

sasa Hajui ashike lipi kati ya dini na siasa

Huna akili na wewe MUNGU aishivyo ata kuhukumu, yeye ni mtumishi hujui siasa na dini na uongozi wa viongozi wa dini.
 
Mhashamu Baba Askofu Munga unavizia wengine waseme kwanza ndio uwajibu? Huna mawazo yako binafsi?
 
Ina maana kwa akili za Mkuu wa dini wa zamani anaona ccm haitawahi kuondolewa madarakani?
Sifa za mkuu za kawaida zenye kasoro za wazi, kuua wapinzani kuua uhuru, kujenga miundo mbinu isiyo na faida kwa uchumi wa nchi tena akitumia mikopo na kuongopa.
Ipo siku wewe mkuu wa dini utatoa hesabu ya maneno yako.
Hawa watu wanaendaje makanisani kwenda kuomba nini kama wana matatizo haya yote?
Mioyoni mwao hata hawajisikii vibaya?
 
Mbele za Mungu hakuna cha mapengo wala cha nani, binadamu wote ni sawa tu hata Pope Fransis mbele za Mungu ni wale wale tu!
Kama Askofu Munga anaona kunyamaza pia ni Hekima, kwa nini yeye hanyamazi kihele hele kila kukicha. Kwanza hana hadhi ya kumjibu Kardinali Pengo maana huyo si level yake
 
Keywords hapo ni Waziri na kufumania! Hakuna namna maoni yangu yangeweza kutoka nje ya mstari, kama ningechangia. Hivi vitu hata shule vinafundishwa, halafu tukimaliza tunalalamika havina application...
Acha kupingana na mantiki. Basics za lugha kwako ni sifuri. Ndo nyie ukimuonà mtu amevaa miwan bas amebukua sana. Hoja ya msingi ni kupata maudhui sio keywords
 
Wasi wasi wangu hata hunaelewa chochote kwenye hiyo comment. Kunywa maji, then soma upya Tena taratibu!
 
Kama kunyamaza ni hekima mbona yeye hajanyamaza? Au hekima hizi hazimuhusu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…