Askofu Gamanywa: Haki ni tunda la utii wa sheria vs Shehe Kishki: Haki ni tunda la uhuru wa binadamu. Ipi ni sahihi?

Askofu Gamanywa: Haki ni tunda la utii wa sheria vs Shehe Kishki: Haki ni tunda la uhuru wa binadamu. Ipi ni sahihi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Askofu Gamanywa ameitafsiri Haki kama tunda la utii wa sheria na kwamba Sheria ndio hutoa haki. Gamanywa amesema Amani ni muhimu kuliko haki kwa sababu Haki hubadilika badilika kulingana na mabadiliko ya sheria lakini Amani iko pale pale.

Naye shehe Kishki ametofautiana na askofu Gamanywa kwa kusema Haki ni tunda la Uhuru ambao binadamu anapewa na Mungu tangu akiwa tumboni kwa mama yake na kwamba hakuna binadamu anayezaliwa kuwa mtumwa bali utumwa ni maamuzi yafanyikayo ukubwani. Shehe Kishki amesisitiza kuwa Haki na Amani ni mapacha wanaofanana.

Source TBC

My take; Wadau naomba maoni kuhusu tofauti ya Haki na Amani
 
Wewe usiye mchuuzi tupe maana ya Haki!
Haki ni usawa mbele ya sheria. Usawa huu ndio huleta amani. Kama kwenye jamii yenye sheria zake lkn kundi moja linavunja sheria hizo haliulizwi lakini kundi lingine likifanya sawa na kundi la kwanza linaandamwa, basi hapo usawa hakuna, hakuna haki na amani ni ngumu kupatikana
 
Tukishajua nani zaidi tukapige kura namna hii
 

Attachments

  • IMG-20201021-WA0002.jpg
    IMG-20201021-WA0002.jpg
    98.5 KB · Views: 2
Gwamanywa siku hizi simuelewi, akisema haki ni utii wa sheria hata zile sheria kandamizi tuzitii tu?!

Sheria zinazowabeba wengine na kuwaumiza wengine hizo hakuna sababu ya kuzitii.
 
Askofu Gamanywa Yuko Sawa!!

Hiyo Amani ni tunda la Uhuru, Nayo siyo mbaya kimtazamo, lakini tusisahau Kwamba, Uhuru ni Sawa na kitendo cha mtu kuhisi njaa

Kwamba Leo atataka Uhuru wa Aina hii, atapewa, na Kesho atataka tena Uhuru Fulani na mwisho wa siku atataka Uhuru wa kufanya mapenzi peupe pe

SASA Uhuru wa kuzingatia sheria ndio Amani haswaa!!
 
Hawapo sahihi wote japo sheikh hayupo mbali sana, Uhuru ni moja ya haki ,na haki ipo kabla ya sheria hivyo haki hawezi kuwa tunda la utii wa sheria wala tunda la Uhuru kwa kuwa haki ndio mbegu ya huo mti uliozaa hivyo vitu.

Haki inatakiwa uipate kwa kuwa ni mtanzania na sio kwa kuilipia kwa kutii sheria au kwa Uhuru. Mfano mtu anapoiba anakamatwa anahukumiwa jela lakini ataendelea kuwa na haki japo hakutii sheria wala hayupo huru.

Askofu kaiabisha PhD yake ya theology
 
Back
Top Bottom