Askofu Gamanywa: Haki ni tunda la utii wa sheria vs Shehe Kishki: Haki ni tunda la uhuru wa binadamu. Ipi ni sahihi?

Askofu Gamanywa: Haki ni tunda la utii wa sheria vs Shehe Kishki: Haki ni tunda la uhuru wa binadamu. Ipi ni sahihi?

'Shehe' wako amesema amani ni tunda la nini?
 
Hawapo sahihi wote japo sheikh hayupo mbali sana, Uhuru ni moja ya haki ,na haki ipo kabla ya sheria hivyo haki hawezi kuwa tunda la utii wa sheria wala tunda la Uhuru kwa kuwa haki ndio mbegu ya huo mti uliozaa hivyo vitu...
Mungu wangu, askofu wangu kapatwa na nini jamani? Mbona anatumia nguvu nyingi hivi hadi kupotosha maandiko? Sio bure kweli kwa utawala huu kila goti litapigwa.
 
Naye shehe Kishki ametofautiana na askofu Gamanywa kwa kusema. Haki ni tunda la Uhuru ambao binadamu anapewa na Mungu tangu akiwa tumboni kwa mama yake.

~na kwamba hakuna binadamu anayezaliwa kuwa mtumwa bali utumwa ni maamuzi yafanyikayo ukubwani. Shehe Kishki amesisitiza kuwa Haki na Amani ni mapacha wanaofanana.

Source TBC


huyu Sheikh Kishki atakuwa amemuwakilisha Sheikh Mkuu wa Taifa Mzee Ponda...haweki unafiq,wala hatafuni maneno
 
Askofu Gamanywa ameitafsiri Haki kama tunda la utii wa sheria na kwamba Sheria ndio hutoa haki. Gamanywa amesema Amani ni muhimu kuliko haki kwa sababu Haki hubadilika badilika kulingana na mabadiliko ya sheria lakini Amani iko pale pale...
Labda nikueleze kisha nikuulize halafu uone kama huyo Gamanywa ameeleza hayo kwa utashi wake au kuna nguvu inamsukuma?
Gamanywa anasema haki ni matokeo ya utii wa sheria!

Haki ni neno pana linalojumuisha aina nyingi za sitahiki. Kuna haki ya kuishi, haki ya kupendwa, haki ya kupewa huduma za afya, Haki ya kusikilizwa, Haki ya kwenda popote unapotaka nk. Kati ya hizo ni haki ipi ambayo ni lazima kufuata sheria ili uipate?

Lakini pia kuna haki ya kukusanyika, haki ya kutoa maoni, haki ya kuchagua na kuchaguliwa nk. Hizi ni haki za kiraia ambazo kila nchi ina sheria zake kuzitekeleza! Kwa hiyo anapokuja mtu na kujumuisha kwenye kapu moja kwamba HAKI ni matokeo ya utii wa sheria ni kujitia umbumbumbu wa makusudi kwa maslahi binafsi.

Atueleze haki ya kuishi inatikana na kutii sheria gani? Kuishi ni haki ya msingi ya binadamu, ni haki anayozaliwa nayo binadamu. Ndo maana baada ya miezi 9 tumboni mwa mama mtoto huitafuta haki ya kuishi kwa kujitegemea kwa kulaIazimisha atoke nje, kulazimisha kwake ndo tunaouita uchungu/utungu kwa wanawake.

Haki hii ni yake tangu anazaliwa mpaka anakufa kwa mapenzi ya Mungu na hakuna mwenye uhalali wa kumnyang'anya na atakayelazimisha kuichukua atakutana na mkono wa Sheria. Huyu kweli ni Askofu? Au siku hizi hivi vyeo anapewa yeyote au anajipa yeyote anapojisikia?
 
Back
Top Bottom