Askofu Gamanywa ameitafsiri Haki kama tunda la utii wa sheria na kwamba Sheria ndio hutoa haki. Gamanywa amesema Amani ni muhimu kuliko haki kwa sababu Haki hubadilika badilika kulingana na mabadiliko ya sheria lakini Amani iko pale pale...
Nakubaliana na Sheikh. Huyo Gamanywa hicho cheo cha uaskofu feki alichojibandika anasababisha hata hilo neno 'askofu' watu waanze kulichukulia for granted.
Haki ni zaidi ya sheria. Watunzi wa sheria wanaweza kutunga sheria inayonyang'anya haki, katika mazingira hayo sheria haiwezi kutoa haki. Utunzi wa sheria unapaswa kuongozwa na Haki, kwamba haki ndiyo izingatiwe katika kutunga sheria, kwamba sheria zote zijengwe juu ya haki.
Na watu wote watakapotendewa kwa haki na kutendeana haki wao kwa wao, na utawala wa nchi ukazingatia haki, ndipo amani itakapokuwepo na kudumu.