Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima amlaumu Halima Mdee kwa mafuriko ya Dar-es-Salaam siku ya leo

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima amlaumu Halima Mdee kwa mafuriko ya Dar-es-Salaam siku ya leo

Unataka kumchafulia Gwajima lakini kawe tunataka maendeleo na mabadiliko kwahiyo usituambie huu ujinga wako

Suala la mafuriko Dar es Salaam ni tatizo la serikali kwa ujumla. Serikali na wenye maamuzi wote wamekuwepo DSM miaka yote wanajionea kwa macho yao na kushuhudia adha zote miaka yote. Halihitaji mbunge kuikumbusha serikali ingawa CCM imekuwepo serikalini miaka yote.

Tafiti zimefanywa na kujadiliwa sana tangu miaka ya 80 lakini kumekuwa na uvivu wa kuwekeza kikamilifu kwa vile miundombinu inayotakiwa inataka hela kubwa kwa kazi ambayo haitaonekana kirahisi machoni: mitaro mikubwa ya chini kwa chini na barabara nyingi kuinuliwa juu kwa juu mithili ya madaraja marefu. Halafu ujenzi wa kingo za mito mikubwa km Msimbazi, n.k. Ile jeuri ya kutamka “kilomita elfu ...” haipo. Ni hela inazikwa chini kwa chini na kwenye zege zito. Wanasiasa hawataki hiyo. Wanataka kukosha wanyonge na kujibakizia 10% ya uhakika.

Safari hii, it’s even worse. Serikali za mitaa zimehamishiwa kwa Rais (Serikali kuu) na mapato yao yote yanapelekwa Hazina. Wakurugenzi wa Halmashauri ni makada wa CCM na wateule wa Rais. Wana sauti juu ya mbunge. Halafu kuna watu wanadiriki kusema Halmashauri hazifanyi kitu. Ukweli ni kuwa HAKUNA SERIKALI ZA MITAA AWAMU YA TANO.

Kazi ya miundombinu ya Dar es Salaam ni kubwa sana; inahitaji mkono wa serikali kuu kuwekeza mabilioni na juhudi kubwa. Gwajima asidhani hii ni sawasawa na mazingaombwe ya kufufua “misukule”.
 
Sasa nani wa kulaumiwa kama si mbunge wa Kawe kazi kwenda kupigana bungeni Kama sisi ndio tumemtuma hicho
 
Mara hii umeshasahau mkuu wa maraika alivyojiapiza hapeleki maendeleo sehemu aliposhinda mpinzani? Na kwani CHADEMA ilishawahi kushika dola na kuwa na uwezo wa kukusanya kodi?
Uislam umekatza kubagua kabisa
 
Duh!

Mkuu Kwanza Gwajima anapotosha ukweli makusudi! Kamwe kisheria sio jukumu la mbunge kuleta maendeleo ya umma!

Kazi ya mbunge ni bungeni na kuisimamia serikali bungeni na katika halmashauri yake. Maendeleo kwa umma ni jukumu la serikali, ndio maana uliona haya Makonda juzi akimbana mkurugenzi fulani hilo! Sio mbunge!

Mbunge hana bajeti ya maendeleo, mfuko wa jimbo upo simply kumfacilitate mbunge kusikiliza maoni na kero za wanajimbo ili aziwasilishe bungeni au halmashauri.

Kama anadai mwenzake hakufanya basi yeye Gwajima aoneshe alichofanya mpaka sasa ndani ya miaka 4 katika jimbo lake.

Waumini wake waone matango pori ambayo wamekuwa wakibugua! Kwa hili naanza kuamini ule mkono wa baunza ulikuwa wa kwake! Ule ubuyu wa clouds ulikuwa wa kweli!

Huyu ni muongo zaidi ya TB Joshua!
 
Mara hii umeshasahau mkuu wa maraika alivyojiapiza hapeleki maendeleo sehemu aliposhinda mpinzani? Na kwani CHADEMA ilishawahi kushika dola na kuwa na uwezo wa kukusanya kodi?
Wachana na hao vichwa maji wa Lumumba
 
Tatizo tutamaliza kwaaa......kimya,
Haliishi hilo tatizo,mwongo tu huyo.
 
Back
Top Bottom