Habari wakuu!
Jana Askofu Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama tawala na ametoa sababu nyingi tu kwa nn yy ni Askofu na anataka kuingia kwenye siasa! Mm kama mtumishi wa Mungu pia na mchambuzi wa Biblia natoa sababu kwa nini askofu gwajima hatakiwa kuwa kwenye siasa.
1: Neno asikofu kibiblia ndo Kazi njema kuliko kazi nyingine zote, kuwa Askofu maanake ww unaongoza makanisa mengine, na umeitwa na Mungu kwa ajili ya Kazi hiyo, maana nyingine unamwakilisha Mungu hapa duniani, na unalipwa na Mungu.
2: Askofu Gwajima ni kiongozi wa kiroho anayeongoza watu wote wa vyama tofauti sasa anapoingia kwenye siasa ataweza kkuwa na ujasiri wa kukemea mabaya yatakayofanywa na chama chake?? Lakini pia Kanisani kwake ataweza kuhubiri bila kuwa na itikadi ya chama?
3: Kazi kubwa ya Askofu Gwajima ni kuwaleta watu kwa Yesu, he! Hiyo Kazi kaimaliza??? ( Rejea kwenye Biblia mavuno ni mengi watenda Kazi ni wachache) bado maasi yanaongezeka duniani huu ndo muda ambao angeutumia kuihubiri injili kwa kila kijiji na kabila watu waache dhambi, hii Kazi hajaimaliza bado anaenda kwenye majukumu mengine ya kaisaria.
4: Mifano aliyoitoa yote haina mashiko ukilinganisha na wito wake, kwanza lwakatare bila shaka alikuwa ni mbunge wa vyiti maalum maanake wa kuteuliwa, na madhara yake tuliyaona hana rekodi ya kuhubiri injili mikoani tofauti na Kanisani kwake!, lakini mchungaji Msigwa au mtikila baada ya kuingia tu kwenye siasa wote tunajua lina baki jina tu uchungaji lakini ule wito kamili unaondoka!
6: Huwezi kuwatumikia mabwana wawili ni lazima umchukie mmoja na umpende mmoja.
7:Kugombea ubunge na ww ukiwa mtumishi wa Mungu sio dhambi lakini madhara yake ni makubwa kwenye ulimwengu wa roho.
8: Kama ni swala la kumsaidia Rais hata hapo alipo uwezo huo anao sana sio mpaka uwe mbunge!
9: Kuwa mbunge ni kujiongezea majukumu ambayo sio ya lazima kwako ili hali kondoo bado wanahitaji malisho yako.
10: Gwajima alianza vizr ila kwenye siasa ungewaachia wenyewe ww uwe mshauri tu:
Note: Nia ya mwili ni mauti lakini nia ya Rohoni ni uzima wa milele, Mungu anaangalia mwisho mwema wala sio mwanzo, gwajima ww huwezi kutolea mfano wa papa wa Italia! Huko ni kuwafurahisha wanadamu ili hali ukweli unaujua tofauti ya makanisa ya kidini na makanisa ya kiroho! Labda kama unataka kuwa mwanadini sawa!
Ili kuelewa jambo hili unashauriwa kusoma mada hii
=> Uchaguzi 2020 - Askofu Gwajima atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe