Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Buji mtata mtata kwema?Huyu huyu anayewatukana makadinali na kutaka kugeuza misikiti kuwa Sunday School ndio mwenye akili?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Buji mtata mtata kwema?Huyu huyu anayewatukana makadinali na kutaka kugeuza misikiti kuwa Sunday School ndio mwenye akili?
Huyu jamaa ana shahada ya saikologia kama anavyosema mwenyewe,ana kanisa lake ana waongopea Wafuasi wake kila sikuGwajima ni smart Sana alafu amezoea bunge Kama amekaa miaka 10 kumbe ndio Mara ya kwanza keep going Gwajima
Kwan Gwajima ndo alikuwa anagombea urais na Lisu nawashangaa kwanini mnachukia hvyo mtu ambaye hajawahi hata kukutana nawe chuki za nini eti Yan kumsifia Rais kwenu kero sasa mnataka nini yanUnamuwaza sana Lissu, sisi hapa tunamzungumzia Ngwajima...
Thread inamzungumzia Ngwajima na hotuba yake, Mimi nimechangia hilo, wewe unani comment unamtaja Lissu. Utakuwa una matatizo ama huenda we ni mchepuko wa Lissu uko obssessed nayeKwan Gwajima ndo alikuwa anagombea urais na Lisu nawashangaa kwanini mnachukia hvyo mtu ambaye hajawahi hata kukutana nawe chuki za nini eti Yan kumsifia Rais kwenu kero sasa mnataka nini yan
Kama kunamtu hafai kuigwa basi ni Lisu maana historia yake mwanzo mwisho ni ukorofi alafu Gwajima hakutupwa na Familia yake fuatilia Historia vzuri na kila jambo linalotokea kwenye maisha linasababu aliishi msikini kwa sababu pia hvyo usimuhukumu mtu kwasababu ya historia ya maisha yake we mwenyewe hajazaliwa mbinguni ni hapahapa dunianHuyu jamaa ana shahada ya saikologia kama anavyosema mwenyewe,ana kanisa lake ana waongopea Wafuasi wake kila siku
Sasa unategemea nini, Gwajima bin Rashid amezoea kuongea na watu,ni mzoefu wa kudanganya na kushifu watu..
Kutokana na stori yake mwenye kuwa alitupwa masikitini na wazee wake
Huyu jamaa hana malezi,huyu jamaa sio mfano mzuri kwa jamii..
Wanaomsifu itakuwa mtu kama wewe,hujijui hujitambui, mfano wa Mwafrika chini ya Jangwa la Sahara..sub human being..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Thread inamzungumzia Ngwajima na hotuba yake, Mimi nimechangia hilo, wewe unani comment unamtaja Lissu. Utakuwa una matatizo ama huenda we ni mchepuko wa Lissu uko obssessed naye
Vip nafaka unauza mazao nin tufanye biashara [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Thread inamzungumzia Ngwajima na hotuba yake, Mimi nimechangia hilo, wewe unani comment unamtaja Lissu. Utakuwa una matatizo ama huenda we ni mchepuko wa Lissu uko obssessed naye
Njoo jumapili uone mwenyewe kuwa wanapungua au wanaongezekaIla kanisani kwake wahumini wanapungua kwa kasi ya mwanga [emoji3577][emoji3577]
Ni kazi ya nin etiiLabda kama hamjui wajibu wa mbunge!! Kumsifia rais siyo sehemu ya kazi ya mbunge
Na export nje in mega tonnes, kama unaweza kununua kuanzia tonnes 500 za mahindi karibu.Vip nafaka unauza mazao nin tufanye biashara [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ushuzi Kabisa ndy huo u smartSalamu za Askofu Gwajima wa Jimbo la Kawe kwa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli alipoteuliwa na Mh.Spika kusalimia kwa niaba ya Wabunge wenzake, leo Bungeni Dodoma.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nikushukuru sana kwa kunipa fursa hii ya kusema maneno machache kwa niaba ya wabunge wenzangu. Ninajua kwamba leo kuna mabunge mawili humu ndani; upo wewe Mheshimiwa Spika lakini pia yupo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa sababu hiyo nimezingatia protokali.
Lakini tu niseme kwamba hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa overwhelming wazungu wanasema. Ni hotuba ambayo akili ya kawaida ya binadamu haiwezi kubeba unless umepata ufunuo kutoka kwa Mungu wa mbinguni. Na kwa sababu hiyo inanipelekea kutoa shukrani kwako wewe Mheshimiwa Spika kwanza, kwa jinsi ulivyochaguliwa kwa kura nyingi na bunge hili kuwa Spika wa bunge la 12; pokea hongera za waheshimiwa wabunge. Lakini pia nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa namna alivyochaguliwa kwa kimbunga cha kura nyingi na akaidhihirishia Tanzania na dunia kwamba muelekeo wake ni muelekeo salama.
Pia, nimpongeze sana kaka yangu, ndugu yangu, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kwa jinsi alivyowageuza wapinzani wake miguu chini kichwa juu kule Zanzibar na akatudhihirishia kwamba yeye ni nguli, ni jabali na hakika ni Daktari, si tu wa watu lakini ni daktari wa siasa pia. Asante sana Mheshimiwa Mwinyi.
Na kwasababu hiyo niseme maneno machache ambayo waziri mkuu wa zamani wa uingereza, Sir Winston Churchill aliwahi kusema, “If you have a destiny and you stop everywhere throwing stones to the dogs that are barking at you, you won’t arrive to your destiny.” Maana yake ni hii kwa wagogo labda hawatanielewa nifafanue, “Ukiwa unasafiri halafu ukawa unasimama kila mahali kumtupia mawe kila mbwa anayebweka, hutafika safari yako.” Mheshimiwa Rais waache mbwa wabweke, tuendelee na safari yetu ya kutimiza ilani ya kurasa mia 303. Waziri mkuu Winston Churchill alisema, “Let them bark for their own enjoyment but keep your course.” Maana yake ni kwamba, “Waache wabweke kwa raha zao lakini wewe kaza mwendo.”
Lakini pia kwa projection hii ya hotuba yako Mheshimiwa Rais ni muhimu niseme na nikiri wazi kwamba, hakuna beberu atakayekupenda kwa projection hii uliyoipanga kwa ajili ya nchi yetu. You have just made a blueprint kwa ajili ya nchi yetu na ni kwa mara ya kwanza kwenye historia ya nchi yetu kuweza kujitegemea kufinance uchaguzi wake na kuzuia fedha inayotoka nje inayotupa masharti ya mambo ya kufuata kinyume na tamaduni zetu za kiafrika. Mheshimiwa Rais is a blueprint not only for Africa but for the whole world as well. Umefanya jambo ambalo dunia yote imestaajabu na mabeberu wote umewaacha mdomo wazi. Asante sana Mheshimiwa Rais.
Umeongea mambo ya ajabu katika hotuba yako. Wakati unazungumza uliposema kwamba maduka yafunguliwe na dawa za kienyeji zianze kuuzwa, Mheshimiwa Nape hapo akawa ananikonyeza ananiambia inawezekana na nyungo za kuruka za wachawi zitaanza kuuzwa, nikamwambia hapana. Mheshimiwa Rais, nikwambie wewe ni muafrika na umetufanya sisi waafrika dunia yote tusione aibu kusema Rais wetu ni John Pombe Magufuli.
Wakati Mheshimiwa Spika anawakaribisha wageni jana hapa; alipowakaribisha wageni wa Mheshimiwa Mpina, akasema kwamba, ninajua wasukuma ni washamba kwa hiyo angalieni msigongwe na magari lakini sasa Mheshimiwa Spika, nikakumbuka ule usemi wa mwalimu mwaka 1978, alipokuwa anasisitiza watu wapanue mashamba, alipofika hapa Dodoma akawaambia wagogo panueni mashamba, wakashindwa kumuelewa na badala ya kupanua mashamba wakapanua masikio. Jamani Mheshimiwa Spika ni mtani wangu kwa hiyo msiwe na shaka, msiogope.
Kwa hiyo ninataka niseme kwa dhati, sisi wabunge tulioingia bungeni kwa mara ya kwanza, pamoja na wabunge wengine ambao wamekuwepo hapa bungeni kwa muda mrefu, tunachukua nafasi hii kukushukuru Mheshimiwa Rais. Performance yako ya miaka mitano iliyopita imetubeba wabunge wote kwenye majimbo yetu na bila shaka tumepata kura kupitia wewe. You have just become a beacon for our victory; you became a reference for our victory. Ulikuwa ndio tofali la ushindi wetu.
Kuna sehemu zingine Mheshimiwa Rais hatukuhitaji kupiga kampeni, tulihitaji kutaja jina lako tu na kura zikapatikana, asante sana Mheshimiwa Rais. Pia, kwa niaba ya wabunge wenzangu kwa sababu nimepewa nafasi ya kutoa shukrani; nikushukuru sana Mheshimiwa Rais, nishukuru pia halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi kwa namna ilivyochagua wabunge wote majabali! Mheshimiwa Rais, wabunge wako wote ni majabali na hakuna mbunge mnyonge hata mmoja hapa. Kwa namna hiyo umejipa urahisi sana wa kutengeneza serikali yako, hauhitaji vetting kubwa sana, chukua yote Mheshimiwa Rais utafanya vizuri. Umewapeleka likizo isiyo na malipo watu wa vetting kwa sababu kutoka kaskazini mpaka kusini mashariki mpaka huko, wabunge wote wanafaa kwa ajili ya kuitumikia serikali yako na kwenda na mwendo wako Mheshimiwa Rais.
Nimalizie kwa kusema, umetupa heshima kubwa sana hasa sisi wabunge ambao ni mara yetu ya kwanza kuingia katika bunge hili. Umetupa heshima kubwa sana na ushindi wako wa kimbunga, umeonyesha dhahiri kwamba kesho yako inang’aa kuliko jana yako na kwa namna hiyo nikushukuru sana na kusema maneno machache kwamba tufani imekoma katika nchi, sasa ni majira mapya! Asante sana Mheshimiwa Rais.
Sawa sawaNa export nje in mega tonnes, kama unaweza kununua kuanzia tonnes 500 za mahindi karibu.
KabisaWatu wa kawe tumepigwa[emoji16][emoji16]hakuna mbunge pale kuna ujinga ujinga tu
Hahaha ni wivu tuUshuzi Kabisa ndy huo u smart
Wachungaji 7 walishajitoa waliobaki misukule iliyofufuliwaNjoo jumapili uone mwenyewe kuwa wanapungua au wanaongezeka