#COVID19 Askofu Gwajima na wewe umechangia kuligharimu taifa hili. Acha tabia hii!

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Nimesikitishwa kwa kiasi kikubwa sana na huyu kiongozi ambaye pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la KAWE kwa kauli zake za kuligawa taifa. Ni kama vile mamlaka vinamchekea utafikiri yeye anatembea na pembe.

Huyu mtu anatoka hadharani na kudiriki kusema eti Marehemu JPM alimpigia simu na kusema waanzishe maombi kwa ajili ya kuomba taifa liondokane na janga la Corona, Marehemu hayupo who knows Kama maneno yake yana ukweli wowote nhamsingizii?

Askofu Gwajima anasahau kuwa kipindi cha JPM tumepoteza viongozi wengi waandamizi wa ngazi za juu kwa sababu ya Corona? Anaweza kutusaidia kutueleza ni kwanini taifa likipoteza viongozi wa juu mfululizo kwa sababu ambazo hatukuambiwa wazi na kweli? Kwanini anataka kupotosha watu kwa sababu ya ujinga wake? Anajua maneno yake yanagharimu maisha ya watu wangapi kwa wakati mmoja?

Mungu gani huyo ambaye anapenda taifa la watu wazembe wasiochukua hatua dhidi ya matishio ya majanga? Kipindi JPM Corona ilikuwepo nyingi tu tena huenda takwimu za vifo zilikua juu kuliko mataifa ya jirani ila tatizo sisi hatukutoa takwimu za vifo na ugonjwa kwa kuficha taarifa zake. Huu ujinga wanaolishwa watu na huyu Askofu hatutamvumilia katu.
 
Ndio umezinduka leo?! Hizo episode tulishazipita kitambo hayo yashakua mambo ya kale lete mambo mapya.
 
Mkuu hao viongozi waandamizi ama wa juu wewe ulikua na ratiba zao za kufa hadi useme walikufa bila sababu? Kwa ratiba yako walitakiwa kufa lini na lini?

Jambo la pili, unaelewa maana ya uhuru wa kujieleza, askofu akitumia uhuru wake wa kujieleza wewe unaumia wapi?
 
Hivi ulitaka kuandika nini hasa? Mbona hukujenga hoja ya kueleweka? Jipange
 
Ameeleweka.

Gwajima asijidai mjuaji sasa hivi, kauli zake wakati ule wa mwendazake zilisababisha kuligawa taifa, kujidai kuanzisha kikundi cha wasukuma wakati vya makabila mengine vilipigwa marufuku ulikuwa ni ubinafsi uliopitiliza ambao haukustahili kufanywa na mtu anayejiita askofu.
 
Huyu mtu anatoka hadharani na kudiriki kusema eti Marehemu JPM alimpigia simu na kusema waanzishe maombi kwa ajili ya kuomba taifa liondokane na janga la Corona, Marehemu hayupo who knows Kama maneno yake yana ukweli wowote nhamsingizii?
Yani kweli katika hotuba zote za Magufuli wakati Corona inaanza wewe hukumsikia akituomba waumini wa dini zote na viongozi wa dini kuliombea taifa? Acha kutafuta sifa za kitoto hivyo.
 
Na Yule alituambia mitambo imetesitiwa yupo Sawa twende tukachanje unaushaidi gani Kama ni kweli
 
Hivi ulitaka kuandika nini hasa? Mbona hukujenga hoja ya kueleweka? Jipange
Hawa jamaa wanachekesha sana.

Kwanza wanapinga kila kitu alichofanya JPM!

Kisha wanampinga yeyote anayeamini katika aliloamini JPM!

Gwajima anaangukia hapo.

Wakikaa kwenye groups zao kila mtu anapangiwa cha kumshambulia Gwajima.

Ndiyo maana threads za kumshambulia Gwajima zinaongozona.

Wanashinda kwa uwingi wa threads na matusi lakini kwa uzito wa hoja wametupwa mbali!
 
Gwajima ana kinga ya ubunge na uaskofu....ndio chanjo yake🤣
 
Hahaaaaaa kwani ni lazima kuchanja jamani si tulikubaliana ni hiari ama! eti tuwaache mnao chanja mtambe tu sisi ambao hatuchanji tukae kimya ???Tuacheni na sisi tutambe hatuchanji nyinyi katestini na mitambo yenu na waume na wake zenu... sisi tuko fiti ile mbaya
 
Nimesikitishwa kwa kiasi kikubwa sana na huyu kiongozi ambaye pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la KAWE kwa kauli zake za kuligawa taifa. Ni kama vile mamlaka vinamchekea utafikiri yeye anatembea na pembe.

Huyu mtu anatoka hadharani na kudiriki kusema eti Marehemu JPM alimpigia simu na kusema waanzishe maombi kwa ajili ya kuomba taifa liondokane na janga la Corona, Marehemu hayupo who knows Kama maneno yake yana ukweli wowote nhamsingizii?

Askofu Gwajima anasahau kuwa kipindi cha JPM tumepoteza viongozi wengi waandamizi wa ngazi za juu kwa sababu ya Corona? Anaweza kutusaidia kutueleza ni kwanini taifa likipoteza viongozi wa juu mfululizo kwa sababu ambazo hatukuambiwa wazi na kweli? Kwanini anataka kupotosha watu kwa sababu ya ujinga wake? Anajua maneno yake yanagharimu maisha ya watu wangapi kwa wakati mmoja?

Mungu gani huyo ambaye anapenda taifa la watu wazembe wasiochukua hatua dhidi ya matishio ya majanga? Kipindi JPM Corona ilikuwepo nyingi tu tena huenda takwimu za vifo zilikua juu kuliko mataifa ya jirani ila tatizo sisi hatukutoa takwimu za vifo na ugonjwa kwa kuficha taarifa zake. Huu ujinga wanaolishwa watu na huyu Askofu hatutamvumilia katu.
Unahangaika Nini na Gwajima?
Wewe utamuweza?
Ameshawaambia Yuko tayari kwa lolote litakaloamuriwa isipokuwa kifo.

Unamulaumu kwa kufanya maombi badala ya kumpongeza?
maana Mungu kaliokoa taifa na hatukuwahi kuwa na lockdown.
Nchi zingine ambalo hawakufanya maombi walitegemea Sayansi hawakufa?
Watu zaidi ya 4m waliokufa ni wa Tanzania?

Nenda huko na upagani wako na Bwana akukemee.
 
Hahaaaaaa kwani ni lazima kuchanja jamani si tulikubaliana ni hiari ama! eti tuwaache mnao chanja mtambe tu sisi ambao hatuchanji tukae kimya ???Tuacheni na sisi tutambe hatuchanji nyinyi katestini na mitambo yenu na waume na wake zenu... sisi tuko fiti ile mbaya
Inawauma Watanzania wamegoma kuchanjwa.
Inawauma wasiochanjwa wanadunda mitaani badala ya kufa kwa sababu hawajachanjwa.
 
Unasemaje?
Hao viongozi waandamizi una uhakika walikufa kwa Covie 19
Na unatuambia kuwa pamoja na uongozi uanramizi wao uliousema walishikiwa akili na Gwajima, isipokuwa wewe?

Basi uwe Mwandamizi ili usife
 
Inawauma Watanzania wamegoma kuchanjwa.
Inawauma wasiochanjwa wanadunda mitaani badala ya kufa kwa sababu hawajachanjwa.
Hili nalo linaweza kuwa kweli.
Yaani tamanio lao nikuona wasio chanjwa wakifa.
Wasipokufa hasira zinawapanda hadi wanatetemeka midomo.
Mbona wasiochanjwa hawawaombei muwe Mazombie?
 
Back
Top Bottom