Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Nimesikitishwa kwa kiasi kikubwa sana na huyu kiongozi ambaye pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la KAWE kwa kauli zake za kuligawa taifa. Ni kama vile mamlaka vinamchekea utafikiri yeye anatembea na pembe.
Huyu mtu anatoka hadharani na kudiriki kusema eti Marehemu JPM alimpigia simu na kusema waanzishe maombi kwa ajili ya kuomba taifa liondokane na janga la Corona, Marehemu hayupo who knows Kama maneno yake yana ukweli wowote nhamsingizii?
Askofu Gwajima anasahau kuwa kipindi cha JPM tumepoteza viongozi wengi waandamizi wa ngazi za juu kwa sababu ya Corona? Anaweza kutusaidia kutueleza ni kwanini taifa likipoteza viongozi wa juu mfululizo kwa sababu ambazo hatukuambiwa wazi na kweli? Kwanini anataka kupotosha watu kwa sababu ya ujinga wake? Anajua maneno yake yanagharimu maisha ya watu wangapi kwa wakati mmoja?
Mungu gani huyo ambaye anapenda taifa la watu wazembe wasiochukua hatua dhidi ya matishio ya majanga? Kipindi JPM Corona ilikuwepo nyingi tu tena huenda takwimu za vifo zilikua juu kuliko mataifa ya jirani ila tatizo sisi hatukutoa takwimu za vifo na ugonjwa kwa kuficha taarifa zake. Huu ujinga wanaolishwa watu na huyu Askofu hatutamvumilia katu.