Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naimudu Kawe. Mimi sio kilaza, nilienda Marekani mwaka jana na nimeshaandika vitabu 5 kwa kijapani, vipo Amazon

Kanisani kwake kaweka Ambulance ngapi?
Sina majibu ya swali lako comrade. Ila anaenda kununua ambulance kwenye kila kata kwa ajili yetu wakazi wa kawe.

Unajua jimbo kawe lina kata ngapi?
 
Hapo pana maswali ya msingi;
1. Hivi kuongea kijapani au lugha nyingine iwayo ni jambo la kujisifu majukwaani?

2. Je hajui kinga ni bora kuliko tiba? Kwanini asizungumzie uboreshaji elimu ambao ungepunguza maradhi yanayoweza kuzuilika?

3. Je kwanini baadhi waumini wake ikiwa ana huo uwezo anaojinadi nao kwa wana Kawe ni maskini sana na wasio na ajira?

4. Je nini majibu yake kuhusu "kugeuza misikiti kuwa sunday school Je aliropokwa? Je alipata wazimu wa muda? Je alikuwa anajifurahisha au kuwahadaa waumini wake?

5. Ikiwa jambo dogo la kuleta ushahidi kuhusu Bashite alishindwa kuuleta anayo haki gani ya kupewa dhamana na wana Kawe? (Hili linaaminisha kwamba maneno yake sio ya kweli na ni uzushi "sijasema ni mwongo na mzushi!")
 
Sawa ,

Kama atakuwa na watu wa karibu yake au team yake ya Campaign basi bila shaka watamfikishia huu ushauri wako naona ni mzuri na kufaa!
 
Sina majibu ya swali lako comrade. Ila anaenda kununua ambulance kwenye kila kata kwa ajili yetu wakazi wa kawe.

Unajua jimbo kawe lina kata ngapi?
Kuamini maneno ya Gwajiboy unahitaji kujitoa ufahamu kwa kiwango cha PHD je alifanikiwa kumfufua Amina Chifupa RIP?
 
Kuamini maneno ya Gwajiboy unahitaji kujitoa ufahamu kwa kiwango cha PHD je alifanikiwa kumfufua Amina Chifupa RIP?
Kwa kweli uyo Gwajiboy unayemzungumzia simfahamu na sijui kama alifanikiwa kumfufua.
Mimi namzungumzia Gwajima nadhani umeniquote kimakosa.
 
Unachotaka kusema ni kuwa kwa sababu Kawe ni mjini kwa hiyo Ambulance haina umuhimu sana? Unadhani Kawe hakuna akina mama ambao wanakosa usafiri wa kuwawaisha kwenda kujifungua? Mwananchi wa Kawe na Ukerewe wana utofauti gani pale inapohitajika Ambulance kwa ajili ya msaada wa dharula?

Kupoteza jimbo la Kawe kusiwafanye mkapoteza uwezo wa kufikiri na kutambua mambo sahihi.
 
Ambao mko karibu na Gwajima mshaurini awe na utulivu halafu aepuke campain za mipasho mfano kumuita Halima bi Kidude mimi naona si sawa!

Gwajima anapaswa kuonesha kuwa matured enough na kustaarabika!

Halafu awe prudent aepuke ahadi ambazo hataweza kuzitekeleza!

Awe na utulivu na kuwa prudent Mbona Safari hii ushindi ni wake tu!
 
Huku jengo la kanisa likiwa nimemshinda kujenga anatangatanga. Lakini angeanza na kuboresha miundombinu ya shule ingefaa kuliko hayo magari.
.....au ndo baada ya matokeo hayo magari yatahitajika......
 
Kwa kweli uyo Gwajiboy unayemzungumzia simfahamu na sijui kama alifanikiwa kumfufua.
Mimi namzungumzia Gwajima nadhani umeniquote kimakosa.
Umeshanunua kitabu chake Amazon?

 
Kwa kuwa wao sio wananchi hao waumini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…