Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naimudu Kawe. Mimi sio kilaza, nilienda Marekani mwaka jana na nimeshaandika vitabu 5 kwa kijapani, vipo Amazon

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naimudu Kawe. Mimi sio kilaza, nilienda Marekani mwaka jana na nimeshaandika vitabu 5 kwa kijapani, vipo Amazon

Chadema hapo ndipo mko hovyo kabisa. Hivi mnapohubili maendeleo ya watu huwa mnaigizaigiza tuuu? Mbunge wenu toka awe kawe amepeleka amburance ngapi? Utajengaje maendeleo ya watu miundo mbinu ya afya ikiwa hafifu?

Hivi mnafaham faida ya haya magari hasa wakati na nyie mtakapokuwa mahututi? Acheni kubwabwaja, inawezekana nyie mnamagari yenu binafsi, ila tuachieni mbunge gwajima atuletee hayo magari ya kubebea wagonjwa sisi wa kipato cha chini.

Mjibuni Gwajima kwa hoja mbadala, sio kubwabwaja hapa.
 
Wewe ndio huna hadhi na huna akili. Video za kutengeneza ili kumchafua ndio unaziamini! Huna akili,usipoteze muda wako kujibishana na watu wenye hekima kama mimi.

Gwajima umefulia utapoteza fedha zako kuhonga na ubunge huupati!! Hilo ukae ukijua.
 
Chadema hapo ndipo mko hovyo kabisa. Hivi mnapohubili maendeleo ya watu huwa mnaigizaigiza tuuu? Mbunge wenu toka awe kawe amepeleka amburance ngapi? Utajengaje maendeleo ya watu miundo mbinu ya afya ikiwa hafifu?...
Lawama ni kwa kiongozi wetu Mbowe, amefuga wanachama ambao hawana ufahamu wa nini maendeleo ya watu.
 
Kwamba ambulance ndiyo we issue ya mtu kukupa kura? Ambulance ina umuhimu, lakini si kitu cha kumfanya mtu akupe kura simply kwa vile utaleta ambulance!
ALISHAWAHI PELEKA ATA BAJAJI KWENYE KATA IPI NDANI YA UTAWALA WAKE WA MIAKA KUMI?
MWAMBIENI ATUACHIE JIMBO HARAKA SAANAA.
 
Hayo unayasema wewe ambae unauhakika wa maisha. Kawe kuna masikini wengi sana ambao wanahitaji mbunge kama Gwajima. Halima aligeuka akawa mzee wa mahakama hawafai tena.

Kununua ambulance ni wajibu wa Serikali na sio wa mbunge kwa pesa zake za mfukoni. Kama Gwajima anataka kununua ambulance kutokana na umasikini uliopo kawe, sio lazima apewe ubunge ndio afanye hilo. Huko kijijini anakotokea Gwajima kuna hali mbaya sana kuliko kawe, angewasaidia huko. Mlimbambikia kesi Halima ili ikifika wakati wa uchaguzi mseme alikuwa ni mzee wa mahakama? Bado mnaamini kuwa watu wamelala hivyo kiasi hawajui lolote?
 
Unajidanganya, Kawe hatuhitaji ambulance. Kwanza ambulance zinatupeleka wapi na zitabeba wangapi kwa popln ya Kawe? Kila mgonjwa wa Kawe akiugua ataipata wapi? and by the way wanaugua wangapi a day in Kawe kuwa kipaumbele chao ziwe ambulance? In the first place, kwa foleni za Dar kwa mahitaji ya mtu wa kawaida wa Kawe, they are as useless as you are useless to us!

Umewaona wajinga kiasi hicho kuwa moved na ambulance? Zina umuhmu sawa, lkn haiwezi kuwa agenda ya mpiga kura kukupa kura yake simply umeahidi ambulance!

Make another attempt, this has failed!
Mkuu Mstaafu, The Retired, kwanza its good to know, kuwa wewe ni mwana Kawe mwenzangu na ni kweli Kawe ina changamoto nyingi na uhitaji wa ambulance sii miongoni mwa changamoto za Kawe. Ungelisaidia sana jukwaa hili kama ungezitaja hizo changamoto ambazo Gwajima hataweza kuzitatua.

Mimi nilikuwepo pale Bunju, hiyo ya ambulance ni moja tuu kati ya mengi, Gwajima amezungumzia changamoto nyingi ikiwemo ya barabara, ajira kwa vijana, mikopo kwa vikundi vya vijana, kinamama na walemavu, amezungumzia kufungua chuo cha veta cha ufundi. Amezungumzia mambo mengi, makubwa mazuri

Kwa faida ya wengi, huyu hapa Gwajima msikilizeni



Kwa kumalizia, maadam wewe ni mwana Kawe na unazijua changamoto za Kawe, sasa kwa vile kuna mtu amekaa miaka 10 Kawe na anataka kuendelea, hebu utueleza amefanya nini Kawe kwa miaka yake yote 10 ili kustahili kuongezewa?

Uchaguzi 2020 - Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Ujumbe kwa wana Kawe, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Kawe tumefanya sana makosa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi kufanya kweli na kamwe tusirudie makosa!

P
 
  • Thanks
Reactions: Ccc
Hahaha kwanza ni wapi Tanzania hii mmewahi kusikia au kuona Ambulance imemfuata mgonjwa nyumbani?!

Nani alimwambia sisi ni wagonjwa?!

Gwajima boy acha maigizo.
 
Angekuwa amenunua ambulance kabla ya kugombea ubunge halafu safari hii akasema atajenga hospital bila shaka ungekuja kuuliza kwanini hakujenga hospital kabla kuwa mbunge. Gwajima hazuiliki

Hazuiliki kwa ahadi ya kununua ambulance, kwani anagombea kuwa mganga mkuu wa hospitali?
 
Jamaa ana akili copywright kama Bashite na kama kuna tofauti basi ni ndogo ndogo sana lakini naamini ukipima DNA zao nafikiri zitakuwa chain moja
 
Hazuiliki kwa ahadi ya kununua ambulance, kwani anagombea kuwa mganga mkuu wa hospitali?
Hapana hagombei kuwa mganga mkuu wa hospital. Anagombea nafasi ya ubunge ambayo mpaka sasa njia ni nyeupe ya kushinda.
 
Chadema inavowapa ahadi kemkem wananchi huku ruzuku wakipata kale ka ofisi ka ufipa hawakakumbuki nao ni akina Gwajima tu, una ahidi makubwaa wakati kibanda chako kinakutoa jasho

Jifunze kuelewa hoja, cdm wanaahidi kufanya hayo iwapo watapewa dola na sio kwa fedha zao. Gwajima yeye anasema akipewa ubunge atanunua kwa fedha zake. Usiwe kilaza wa hoja za wazi kama hizi.
 
Hapana hagombei kuwa mganga mkuu wa hospital. Anagombea nafasi ya ubunge ambayo mpaka sasa njia ni nyeupe ya kushinda.

Sema njia ni nyeupe, na sio kwakuwa kaahidi ambulance, maana haendi kuongoza wagonjwa.
 
Kamanda mwenzangu unaniaibisha,Ambulance hazina umuhimu! Tuache kupinga kila kitu.
Lazima kuwe na proportional kwenye kila kitu, hizo ambulance kwa kila kata zitakuwa zinapeleka wapi hao wagonjwa.

Kabla ya kufikiria ambulance lazima kufikiria haya kwanza
Elimu ya afya kwa watu wa eneo husika
Vituo vya afya vyenye wahudumu qualified
Vituo vya afya vyenye vifaa tiba vya kutosha

Kumbuka ambulance sio taxi na gari maalum za kubeba wagonjwa wa dharura hivyo inatakiwa kuwa na mahitaji yote maalum pamoja na wahudumu wenye ujuzi husika.

Sasa kila kata ambulance zitakuwa zinapaki wapi kwa usimamizi wa nani? Zitakuwa zinahudumiwa na nani?

Ambulance sio ving'ora na maandishi makubwa ubavuni ile ni EMERGENCY LIFE SAVER TOOL, Sio tax kuwa unaweza kupaki hata kona bar
Hawa wanasiasa uchwara wanapotoa ahadi kabla ya kuzikubali muwe na tafakuri, that's why nikasema he is moreless a pumpkin
 
Sema njia ni nyeupe, na sio kwakuwa kaahidi ambulance, maana haendi kuongoza wagonjwa.
Kinachompa ushindi Gwajima ni ahadi zake kwa sisi wakazi wa kawe ikiwemo ambulance comrade
 
Hahaha kwanza ni wapi Tanzania hii mmewahi kusikia au kuona Ambulance imemfuata mgonjwa nyumbani?!

Nani alimwambia sisi ni wagonjwa?!

Gwajima a.k.a UNO boy acha maigizo.
Unajua watu hawana tafakuri wanadhani ambulance ni gari ya kawaida kama daladala au tax.
Ambulance handling yake ni tofauti kabisa na magari mengine
 
Back
Top Bottom