Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naweza kufanya kazi yoyote ambayo haijakatazwa kibiblia, Mungu alijitambulisha kwa majina tofauti!

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naweza kufanya kazi yoyote ambayo haijakatazwa kibiblia, Mungu alijitambulisha kwa majina tofauti!

Naomba na mimi nichangie kwenye mada hii! Askofu huyu ni mpumbavu, hakuna tafasiriya hivyo kwenye Biblia. Tena Biblia imekataza kabisa huwezi kuwatumikia mabwana wawili! Yeye kama ameamua kumtumikia Mungu abaki huko huko!! Ila ukweli ubaki pale pale bila mbereko ya polisi hawezi kushindana na Halima!
Na akisaidiwa na polisi maana yake lazima kuwepo na ukiukwaji wa haki za binadamu na hata wizi wa kura.

Maana yake ni kuwa atakuwa mbunge aliyeshinda kwa wizi ilhali yeye ni askofu
 
Kwahiyo hata ya kufanya movie naona anaweza kama alivyo dakwa anavunja amri ya 6, huyo hana sifa ya kuingia kwenye jengo la kutunga sheria
Askofu Gwajima amesema Mungu anayemtumikia alijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kulingana na nyakati na jukumu husika.

Alijiita Jehova, Niko ambaye Niko, Mungu Mwenyezi, Bwana wa Majeshi nk.

Hivyo mtumishi wa Mungu unaweza kufanya kazi yoyote ilimradi tu kazi hiyo siyo katazo la kibiblia.

Askofu Gwajima ametangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe Wilayani Kinondoni.

Maendeleo hayana Vyama!
 
Muda utaongea. Tunayo takribani miezi 3, hadi uchaguzi mkuu. Mbivu na mbichi zitajulikana
 
Sasa nyie watu mnaamini katika demokrasia ipi? Akiwa mbunge Mch. Msigwa sawa. Mch. Israel yule wa Karatu sawa. Ila akiwa Gwajima inakuwa nongwa! Acheni ubaguzi. Kila mtu anayo haki ya kugombea na kuchaguliwa. Ikiwa anastahili atashinda na ikiwa hastahili atashindwa. Muache kujiona mnajua kila kitu.
Gwajima alisema hawez gombania ubunge nafasi aliyokua nayo ni kubwa ni Zaid ya ubunge
 
Mkuu haya ndiyo yalikua mahubiri yake kanisani leo???
Aliposema hawezi kujishusha kuwa diwani, mbunge au waziri alimaanisha nini au dili zimeisha kanisani sasa anajishusha ili apige dili siasani?
 
Gwajima alisema hawez gombania ubunge nafasi aliyokua nayo ni kubwa ni Zaid ya ubunge
Amejisahaulisha na anadhani watanzania wote ni wasahaulifu kama wa chama chake au waumini wake waliotetea ule ufuska wake kana kwamba ndio utakasifu wenyewe!!
 
Askofu Gwajima amesema Mungu anayemtumikia alijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kulingana na nyakati na jukumu husika.

Alijiita Jehova, Niko ambaye Niko, Mungu Mwenyezi, Bwana wa Majeshi nk.

Hivyo mtumishi wa Mungu unaweza kufanya kazi yoyote ilimradi tu kazi hiyo siyo katazo la kibiblia.

Askofu Gwajima ametangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe Wilayani Kinondoni.

Maendeleo hayana Vyama!
Mathayo 6:24
“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili. Maana atamchukia mmoja na kumpenda huyo wa pili; au ataambatana na mmoja na kumdharau huyo mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja
 
Ni sawa ana wajibu wake kiroho huko kanisani kwake lakini yeye ni mtanzania ana haki sawa na watanzania wengine.

Tunaweza kuhoji dhamira na integrity yake lakini hatuwezi kuhoji haki yake ya msingi ya kiraia. Marehemu Rwakatare na Mchungaji Msigwa wote walikuwa wabunge hatukuwahi kuhoji haki zao.

Watanzania tusome zaidi siasa hata kama hatutaki kuwa wanasiasa ili tunapojadili tujadili mambo kwa kufuata misingi badala ushabiki.
Rwakatare na Msigwa hakuna mahali waliukana udiwani, ubunge au uwaziri kama gwajiboy aliyesema ana cheo kikubwa kuliko hivyo na havihitajii...
Atoe majibu tu "...ameona nini katika siasa hata akakengeuka?" Au kala maharagwe ya wapi askofu yule...?
 
Kama aliwahi kukataa madhabahuni kuwa hajawahi kuunga mkono UKAWA huku video zake zote akiwa kwenye vikao vya UKAWA viko online tutamwaminije huyu mzinzi, muongo na msahaulifu?
 
Attachments

  • 2445530_Mwambie_Gwajima_Ukiwa_muongo_jitaidi_uwe_na_kumbukumbu.._rolling_on_the_floor_laughing...mp4
    694.2 KB
Kama aliwahi kukataa madhabahuni kuwa hajawahi kuunga mkono UKAWA huku video zake zote akiwa kwenye vikao vya UKAWA viko online tutamwaminije huyu mzinzi, muongo na msahaulifu?
Makaburi yote yatafukuliwa.
Mungu hawezi kudhihakiwa.
Halafu sijui waumini wake akili zao zikoje.
Watamuunga mkono ktk hili pia.
 
Anatuona sisi sote ni kama wale waumini wake kila anachoropoka hushangilia
Hawa wanaojiita manabii, mitume mara maaskofu wenye makanisa yao sijawahi kuwaamini.

They are shopkeepers waiting for desperate customers to come and buy the "holy ghost"
 
Askofu Gwajima amesema Mungu anayemtumikia alijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kulingana na nyakati na jukumu husika.

Alijiita Jehova, Niko ambaye Niko, Mungu Mwenyezi, Bwana wa Majeshi nk.
Inabidi Akasome Tena Bible kwa Umakini; Watu ndio waliokuwa wanamtambulisha Mungu kulingana na Matendo yake; Mungu habadiliki; ni yeye yule Miaka Hiyo, Jana Leo na Milele yote.
 
Mkono wa baunsa aka Gwajiboy aache kujidharirisha kwenye mambo ya siasa.. awaachie wakina kasheku huko na lema,yeye aendelea kutafuna sadaka.za waumini.
 
Gwajima Jiunge unufaike na elimu ya kupitia tovuti ya Tigo kisha utaanza kulipia tsh100/siku. Tuma neno CLICK kwenda 15313 sasa.

Itakusaidia kupunguza ujinga.
 
Askofu Gwajima amesema Mungu anayemtumikia alijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kulingana na nyakati na jukumu husika.

Alijiita Jehova, Niko ambaye Niko, Mungu Mwenyezi, Bwana wa Majeshi nk.

Hivyo mtumishi wa Mungu unaweza kufanya kazi yoyote ilimradi tu kazi hiyo siyo katazo la kibiblia.

Askofu Gwajima ametangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe Wilayani Kinondoni.

Maendeleo hayana Vyama!
Huna lolote mzee mbona kunayaliyo katazwa kwenye biblia unafanya?
 
Askofu Gwajima amesema Mungu anayemtumikia alijitambulisha kwa majina tofauti tofauti kulingana na nyakati na jukumu husika.

Alijiita Jehova, Niko ambaye Niko, Mungu Mwenyezi, Bwana wa Majeshi nk.

Hivyo mtumishi wa Mungu unaweza kufanya kazi yoyote ilimradi tu kazi hiyo siyo katazo la kibiblia.

Askofu Gwajima ametangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Kawe Wilayani Kinondoni.

Maendeleo hayana Vyama!

Hivi kuna mwenye Klip yake aliyesema kazi ya Ubunge ni ndogo sana kuliko hiyo ya utumishi wa Kanisa? Na akasema hatarajii kugombea Ubunge. TYafadhali iwekeni hapa tuone jinsi alivyokuwa Mtumishi Muongo.
 
Back
Top Bottom