Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Askofu Gwajima ambaye ni Mbunge wa Kawe kasema nchi imekosa maono kwa kuwa kila Rais akiingia madarakani anaachana na ya mtangulizi wake, kuongeza hilo kamwe halitaweza kutuletea maendeleo
Gwajima amesema nchi inatakiwa kuwa na mikakati yake ya muda mrefu na kila rais anayeingia madarakani anaongozwa na mikakati na maono hayo na sio kuleta vitu vyake vipya, ama sivyo anaweza akaja Rais wa ajabu ambaye atavuruga kila kitu na hakuna atakeyeweza kumbana kwa kuwa hakuna maono.

Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima amesema ni muhimu Tanzania kuwa na Dira ya Taifa ili kila Rais anayeingia Madarakani asimamie maono ya Nchi na si yake binafsi
Akiwa Bungeni amezungumzia kila Rais anayeingia Madarakani kuanza na lake akisisitiza hakuna Nchi inayoweza kuendelea ndani ya Utawala mmoja
Ameeleza, "Alipoishia Nyerere, Mwinyi hajaendelea pale. Alipoishia Mwinyi, Mkapa hajaendelea. Alipoishia Mkapa, Kikwete hajaendelea pale na Magufuli naye hajaendelea. Kila Rais anayeingia Madarakani anaanza chake"