Ni hali ya hatari kubwa kwa ugonjwa huu unaouwa (ambalo ni tatizo la kisayansi) unapoachwa kufanyiwa siasa au mzaha.
Ni hatari zaidi hali hiyo inapoachwa kuendelea, wakati serikali iliyo na dhamana ya kutulinda, ikiwa imechagua kuwa kama mpenzi mtazamaji tu.
View attachment 1868361
Haiingii akilini ni vipi serikali kutumia nguvu kwenye kongamano la Chadema kwa sababu za kudhihibiti Corona lakini si huyu anayehamasisha watu kutochukua tahadhari!
Kwa mwendo huu wa kuzikumbatia siasa uchwara zenye kuweka maslahi binafsi mbele tungali na safari ndefu sana.
-------
My take:
Uzi huu chini unaihusu sana serikali kwa sasa na hasa mheshimiwa SSH:
Itakuwa kujidanganya kama taifa kudhani kuwa tuko vizuri. Matumaini mapya yaliyoibuka baada ya SSH kuchukua nchi yamekwisha baada ya siku 100 ofisini. Kama taifa tunayumba tokea kwenye corona hadi kwenye mustakabala kama taifa. Taifa limegawanyika hisia kali na munkari juu: 1. Kuhusiana na...