#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Huyu jamaa ni mpumbavu sana ná Serikali inamuacha tu asambaze ujinga wake.
Kama chanjo imekuja na ni salama,hofu ya nini kuwachanja wanajeshi na polisi, kwani hata wao wanaweza kuwa sehemu ya kusambaza maambuzi kwa wengine, kama wao hawafai kuchanjwa basi na wengine hawafai kuichanjwa,hili siyo taifa la wanajeshi na polisi ni taifa na watanzania wote.
 
K

Kwani ww unauhakika kilichofungwa humo ni chanjo ya corona kama corona!? Hauhitaji kujua nini hasa hiyo human genetic engineering vile itakufanya😜?
Maandiko ya kisayansi yapo yanayoelezea jinsi chanjo inavyofanya kazi na composition yake na hata majaribio yaliyofanyika kuweza kujiridhisha ufanisi wake....serikali kupitia vyombo vyake husika ndio ina uwezo wa kuhakiki kilichomo...wewe unafahamu chemical composition ya coca cola ?

Unafahamu hasa kiasi cha electromagnetic waves zinazotoka kwenye simu yako kama ni salama ?

Serikali ndio inayofanya kazi ya kujua kipi ni salama kwa wananchi wake, kama serikali na vyombo husika vikisema kitu ni salama, serikali za nchi nyingine zikasema ni salama, taasisi nyingine za kimataifa zikasema ni salama then who are you kupinga bila evidence ? Kama ukisema kisitumike basi weka ushahidi katika mfumo wa andiko la kisayansi ambapo wanasayansi wengine watajifunza kutoka kwako ama kukukosoa.
 
Wewe hata uandike vipi watz wachache sana watachoma...survival late ni 99.9% wagonjwa hawataki 1000 kati wa watu mil 60, kwann tu vaccinate watu without knowing the long term impact? Hapa wamenoa
Nilichofanya ni kujibu hoja zako, ili kama kuna mtu hajafanya maamuzi asome pande mbili za shilingi na afanye maamuzi.

Hiyo survival rate ya 99.9% umeitoa wapi ? Unafikiri survival rate ya covid kwenye Scandinavian countries itakuwa sawa na Brazil, Ecuador, Tanzania ?
Nchi kama Tanzania hata survival rate haijulikani, kwa sababu hata data za corona zina gaps zisizoeleweka

Moshi tu KCMC tunaambiwa wameelemewa na upungufu wa mitungi ya gesi👇

Sasa hivi tunasikia corona ikiongelewa kwa sababu tu Magufuli hayupo, tunaambiwa tupo wimbi la tatu lakini ni lini tulipita wimbi la pili ? Wanatuambia wimbi la pili lilituathiri zaidi lakini ni lini tuliambiwa athari zake.

Haijulikani hasa idadi ya wagonjwa waliopo Tanzania kwa sababu hatuna kampeni ya kupima watu kwa wingi na hatuna huo uwezo.

Wengi wanakimbilia kusema "long term impact" lakini ndio hao hao akipata mafua ananunua Antibiotics pharmacy anapona bila kuwaza long-term impact ya kitendo hicho, baadae anakuja kupata bacterial infection sugu anaondoka, wengine wanabugia panadol kila siku kichwa kikiuma kumbe anashida nyingine mwisho wa siku anakuta amechoma maini. Sarakasi zote za kupinga chanjo zimeletwa na utandawazi, hakuna kingine !
 
Kwani Gwaji anafahamu chemical composition ya panadol kweli? Mbona anahoji components za chanjo ya Corona? Hajawahi kutumia panadol?
 
Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
Huyu Bwana ni kama Mganga wa Kienyeji.

Yuko Negative tu kwa kila kitu.

Majeshi yetu yako juu kisayansi kuliko anavyofikiri.

Yeye ana mchanganyiko wa mawa zo ya kienyeji yanamtesa.

Mara Corona ni 5G
Mara Corona ni feki haiui
Mara Corona ni mambo Chungu nzima

Wewe kawalaletee Wananchi Wakawe zile Boti za Uvuvi hayo ya Corona mwachie Dada yako Dorothy kwa sababu kwa sasa anapiga kazi kitaalamu kabisa
 
Tusikimbilie kujibu hoja kabla ya kutafakari kwa kina na kunwelewa mtoa hoja.
Binafsi namuunga mkono 100% Askofu Gwajima kwa sababu nimeielewa hoja yake ya msingi.
Kumbukeni, hata ile Tume ya Corona haikuleta majibu yoyote yatokanayo na watu kuhofia usalama wa chanjo.
Miongoni mwa mambo ya msingi waliyotakiwa kutueleza bayana ni na:-
(1) Chanjo hiyo ina madhara(side effect) gani kwa binadamu?
(2)Je, ukipata hiyo Chanjo huwezi kuambukiza au kuambukizwa Corona?
(3) Je, tangu Chanjo ianze kutolewa katika Nchi mbalimbali Duniani, ni Nchi ngapi mpaka sasa hazina Corona kabisa kutokana na Wananchi wake kuwa wamepata Chanjo?
Hayo ni machache tu, ingawa hata hayo machache hawakuweza kuyatafutia majibu.
Swali la msingi la Askofu Gwajima ni, kwa nini Corona inapigiwa debe sana wakati huu tofauti na wakati wa JPM?
Kuna nini nyuma ya pazia?
Tunataka majibu ya maswali hayo kwanza kabla ya kutulaghai kutumia Chanjo.
 
No zezeta tu anayeweza kupuuza kauli ya Gwanjima,kwani ni Nani anayejua long term side effects ya hizi chanjo!
Kwanini Serikali imejitoa kuwajibika ikiwa mtu atapata madhara! Kama zipo salama?
Watu weusi unafikili tuna akili, watu hawataki hata kujifunza kwa historia tu. Kitu hakijafanyiwa clinical trials za kutosha kujua long term effects lakini mi mtu inashadadia tu
 
Yeye ametoa hoja kwa nini uchanjwe then ufate taratibu ambazo mtu asiechanjwa anafata? Inakuwaje upewe chanjo ya Ukimwi then unaambiwa utumie condom kunyanduana??
Hiyo hoja ni ya msingi, haiwezekani ww umepata kinga alafu uendelee kuvaa barakoa.
 
Umeandika pumba tu kachajwe huko,tuache sis tusikuwa na akili hatujanjWI
 
No zezeta tu anayeweza kupuuza kauli ya Gwanjima,kwani ni Nani anayejua long term side effects ya hizi chanjo!
Kwanini Serikali imejitoa kuwajibika ikiwa mtu atapata madhara! Kama zipo salama?

Sintu uzezeta yaan inahitaji ukosefu wa akili timamu kabisaaa kumpinga Gwajima MB
 
Samahani. Wewe ni mjinga ingawa unaona umeelimika.
 
Kwani Gwaji anafahamu chemical composition ya panadol kweli? Mbona anahoji components za chanjo ya Corona? Hajawahi kutumia panadol?

Unauliza swali shallow sana hata mtoto mwenye akili aliye darasa la tano hawezi kuuliza hivi. Sorry
 
Maandiko ya kisayansi yapo yanayoelezea jinsi chanjo inavyofanya kazi na composition yake na hata majaribio yaliyofanyika kuweza kujiridhisha ufanisi wake....serikali kupitia vyombo vyake husika ndio ina uwezo wa kuhakiki kilichomo...wewe unafahamu chemical composition ya coca cola ?

Unafahamu hasa kiasi cha electromagnetic waves zinazotoka kwenye simu yako kama ni salama ?

Serikali ndio inayofanya kazi ya kujua kipi ni salama kwa wananchi wake, kama serikali na vyombo husika vikisema kitu ni salama, serikali za nchi nyingine zikasema ni salama, taasisi nyingine za kimataifa zikasema ni salama then who are you kupinga bila evidence ? Kama ukisema kisitumike basi weka ushahidi katika mfumo wa andiko la kisayansi ambapo wanasayansi wengine watajifunza kutoka kwako ama kukukosoa.
Acha upuuzi ww! Tangu lini coca cola imetiliwa shaka! Ndio ninyi mnao kariri na kupita madarasa na kupoteza kitu cha maana kupita vyote kwa msomi...kuhoji/kudadisi!
Ingetokea sintofahamu hii kwenye coca cola tusingeendelea kuitumia!
Unajifanya unaamini sayansi kuliko hata sayansi yenyewe! Unayaelezeaje matukio ya wadungwaji kuganda damu na wengine hata kufa! Unaelezeaje waliochanjwa full dose kuambukizwa na kulazwa tena hospitalini na wengine kufa pamoja kuwa walichanjwa! Au hata hufuatilii yanayojili UK na keingineko ww msomi uchwara!?
Au hufuatilii ukweli kwamba hao virusi wa mafua hujibadilibadili na hivyo hata ukidungwa vichanjo uchwara hivyo vya majaribio vyenye vina7 baada ya muda mfupi virusi vitabadirisha na kuvaa suti nyingine na kuja kusababisha maafa kwenu mliochanjwa kana kwamba hamkuchanjwa!
Ww kama umelishwa mlungula kula kimya kimya ila usituletee hadaa zako hapa pungu1!
 
Back
Top Bottom