#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Kuna watu wanawashambulia Gwajima na Ndugai ila wao kama sehemu ya Bunge wanatakiwa kupingana na rais bila kuvunja katiba ya nchi.

Lazima tujifunze kuwa na mawazo huru hoja ya Gwajima ila mashiko inatakiwa kujibiwa kwa hoja

Waziri wa Afya aliwaaminisha watu ujinga leo amegeuka anatakiwa kujibu hoja za chanjo kwa undani zaidi ili watu waondoe shaka.

Hoja ya Ndugai pamoja na kuwa sikubaliani naye ila ana haki ya kutoa maoni yake.

Mimi napingana na Mwigulu kubishana na Rais maana yeye ni sehemu ya Serikali ila Gwajima na Ndugai sina sida nao.
 
Jinsi wazindakaya wanavyoipigia kampeni hii chanjo,ndivyo sisi wengine tunzadi kupata wasi wasi nayo,ina ajenda ipi nyuma yake!!
 
Kumuamini Gwajima kwa kusema hoja yake ina mashiko halafu hapo hapo unagoma kumuamini waziri wa Afya kwasababu ya msimamo wake uliopita ni ujinga, mbona Gwajima wakati wa mwendazake nae aliwahi kusema Corona haitaingia Tanzania?
 
Si wamesema hii ni Hiari ?

Sasa kutumia muda wako kuwakataza / kuwa-convince watu hiari yao si ni kupotoka ?

Huu kama sio Uchochezi ni nini ?
 

Elimu yako tafadhali. Umebobea kwenye nini mkuu?



Kumbuka ujinga ni mzigo ambao kama ulivyo mzigo wa kuni nao hubebwa kichwani 😂😂😂😂😂!
 
Yohana Mbatizaji ,Ni kweli hayo Maneno ya Gwajima? Isije ikawa ni "BAUNSA" ndiye aliyeongea!!
 
Ngoja tuone hii movie itaisha vipi.....mpuuzi atajulikana tu siku ya mwisho...

kila mtu atumie utashi wake kufanya maamuzi...tuache kusambaza hisia za kikuda huku mtaani
 
Mbunge wa bunge la JMT kupitia jimbo la Kawe mh Josephat Gwajima amesema ni balaa kubwa kuchagua Kigeugeu kuwa kiongozi katika jambo lolote lile.

Mkiwa na Kiongozi anayebadilikabadilika kulingana na maslahi yake binafsi basi mjihesabu " mmekwisha" maana yeye anaijua kesho yake tu na siyo kesho yenu, amesema.
 
Huyu jamaa CCM mnamlea kweli...anapingana na Serikali yenu kuhusu chanjo, anapotosha watu na mnamuacha anarandaranda tu mitaanii..

Huyu anamuhujumu Mama Samia kwenye vita hii waziwazi...hawa ndiyo magaidi wenyewe hawa!!
 
Hamna wa kulia ndugu, Yesu yupo pamoja nasi!! Aliyetuvusha 2020 atakuwa na sisi pia

2020 hukuvushwa wave ilipita. Tambua kila wave ina wake:

Wave #1 - kina Mahiga, Nkapa mbunge wa Sumve, DC Mtwara nk, wapumzike kwa amani.

Wave #2 - kina Maalim, Kijazi, jiwe, nk wapumzike kwa amani.

Wave #3 - ndiyo hii inayo tusuka suka sasa hivi.

Utakuwa umetupia miwani ya mbao kama kimbembe cha wimbi hili wewe hukioni.

Ni ujinga kudhani kuwa umevuka kwa wimbi moja kupita wakati tufani lingalipo na mawimbi mengine makubwa zaidi yangali njiani yaja 😂😂!
 
Tuanze naye, alituambia Corona haitaingia Tanzania, ikaingia, sasa hivi anatuambia tumuachie Corona apambane nayo, nani atamuamini?

Kama anajiamini anafufua wafu aanze kumfufua yule alietangulia mwezi wa tatu, kinyume na hapo aache kusema wenzake wakati na yeye ni msanii tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…