#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Kuna watu wanawashambulia Gwajima na Ndugai ila wao kama sehemu ya Bunge wanatakiwa kupingana na rais bila kuvunja katiba ya nchi.

Lazima tujifunze kuwa na mawazo huru hoja ya Gwajima ila mashiko inatakiwa kujibiwa kwa hoja

Waziri wa Afya aliwaaminisha watu ujinga leo amegeuka anatakiwa kujibu hoja za chanjo kwa undani zaidi ili watu waondoe shaka.

Hoja ya Ndugai pamoja na kuwa sikubaliani naye ila ana haki ya kutoa maoni yake.

Mimi napingana na Mwigulu kubishana na Rais maana yeye ni sehemu ya Serikali ila Gwajima na Ndugai sina sida nao.
 
Jinsi wazindakaya wanavyoipigia kampeni hii chanjo,ndivyo sisi wengine tunzadi kupata wasi wasi nayo,ina ajenda ipi nyuma yake!!
 
Kumuamini Gwajima kwa kusema hoja yake ina mashiko halafu hapo hapo unagoma kumuamini waziri wa Afya kwasababu ya msimamo wake uliopita ni ujinga, mbona Gwajima wakati wa mwendazake nae aliwahi kusema Corona haitaingia Tanzania?
 
Si wamesema hii ni Hiari ?

Sasa kutumia muda wako kuwakataza / kuwa-convince watu hiari yao si ni kupotoka ?

Huu kama sio Uchochezi ni nini ?
 
Sawa covid ipo, na variants zake and whatever waves we are expecting in the future, hata lije wimbi la 40, ni hivi tutahimiza watu wasichanjwe... hawa watu wametengeneza tatizo ku create fear ili wachome watu masindano(chanjo) bila kuwa na uhakika na content ya hizo chanjo? Kachome wewe na familia yako... wanaopinga sio wajinga kama unavyofikiri, we are well informed and we know exactly what is goin on huko duniani... Tumesoma na kujifunza mambo mengi sana kuhusu hizi chanjo. Wajinga pekee ndio watachoma hizo chanjo.

Elimu yako tafadhali. Umebobea kwenye nini mkuu?

Screenshot_20210625-093839.png


Kumbuka ujinga ni mzigo ambao kama ulivyo mzigo wa kuni nao hubebwa kichwani 😂😂😂😂😂!
 
Yohana Mbatizaji ,Ni kweli hayo Maneno ya Gwajima? Isije ikawa ni "BAUNSA" ndiye aliyeongea!!
 
Ngoja tuone hii movie itaisha vipi.....mpuuzi atajulikana tu siku ya mwisho...

kila mtu atumie utashi wake kufanya maamuzi...tuache kusambaza hisia za kikuda huku mtaani
 
Mbunge wa bunge la JMT kupitia jimbo la Kawe mh Josephat Gwajima amesema ni balaa kubwa kuchagua Kigeugeu kuwa kiongozi katika jambo lolote lile.

Mkiwa na Kiongozi anayebadilikabadilika kulingana na maslahi yake binafsi basi mjihesabu " mmekwisha" maana yeye anaijua kesho yake tu na siyo kesho yenu, amesema.
 
Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
Huyu jamaa CCM mnamlea kweli...anapingana na Serikali yenu kuhusu chanjo, anapotosha watu na mnamuacha anarandaranda tu mitaanii..

Huyu anamuhujumu Mama Samia kwenye vita hii waziwazi...hawa ndiyo magaidi wenyewe hawa!!
 
Hamna wa kulia ndugu, Yesu yupo pamoja nasi!! Aliyetuvusha 2020 atakuwa na sisi pia

2020 hukuvushwa wave ilipita. Tambua kila wave ina wake:

Wave #1 - kina Mahiga, Nkapa mbunge wa Sumve, DC Mtwara nk, wapumzike kwa amani.

Wave #2 - kina Maalim, Kijazi, jiwe, nk wapumzike kwa amani.

Wave #3 - ndiyo hii inayo tusuka suka sasa hivi.

Utakuwa umetupia miwani ya mbao kama kimbembe cha wimbi hili wewe hukioni.

Ni ujinga kudhani kuwa umevuka kwa wimbi moja kupita wakati tufani lingalipo na mawimbi mengine makubwa zaidi yangali njiani yaja 😂😂!
 
Tuanze naye, alituambia Corona haitaingia Tanzania, ikaingia, sasa hivi anatuambia tumuachie Corona apambane nayo, nani atamuamini?

Kama anajiamini anafufua wafu aanze kumfufua yule alietangulia mwezi wa tatu, kinyume na hapo aache kusema wenzake wakati na yeye ni msanii tu.
 
Back
Top Bottom