#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Ni wazo baya sana kuwachanja chanjo ya Corona askari wa majeshi yetu kwa sababu hatujui usalama wa hizo chanjo.

Baba Gwajima amesema anapinga kwa 100% vyombo vya dola kuchanjwa kwa sababu tunaweza kupoteza taifa. Askofu Gwajima amesema haya Kanisani kwake leo.

Askofu Gwajima amewataka wafuasi wake na wapiga kura wa jimbo la Kawe wakatae kabisa kuchanja kwa sababu watapata hasara kubwa sana maishani.

" Naikataa kabisa chanjo ya Corona " amesisitiza baba askofu.

Chanzo: Mtandao wa You tube!
Kwaiyo wachanjwe wanafunzi au wamachinga
 
Mm chanjo siwezi kuchanjwa
Hongera. Hiyo ni haki yako. Hakuna mwuungwana wa kukulazimisha, kukusikitikia wala kukushangilia.

Uamuzi ni wako, ila usipotoshe wengine wasiokuwa na uelewa kwa maslahi yako binafsi.

Hiyo ndiyo maana ya hiari:

IMG_20210720_094159_438.jpg
 
Kwa wenye akili finyu tu. Chanjo za ndui, pepo punda, kifua kikuu. Polio etc nazo zilizokwapuliwa kwa BEBERU huyo mpuuzi alizifanyia tathmini ili kujua kama ni salama kwa Watanzania!?
Gwajima ana hoja!
 
Mbunge wa bunge la JMT kupitia jimbo la Kawe mh Josephat Gwajima amesema ni balaa kubwa kuchagua Kigeugeu kuwa kiongozi katika jambo lolote lile.

Mkiwa na Kiongozi anayebadilikabadilika kulingana na maslahi yake binafsi basi mjihesabu " mmekwisha" maana yeye anaijua kesho yake tu na siyo kesho yenu, amesema.
Yupo sahihi, lakini

Atoe bolti iliyo jichoni mwake kwanza.
 
Kwa wenye akili finyu tu. Chanjo za ndui, pepo punda, kifua kikuu. Polio etc nazo zilizokwapuliwa kwa BEBERU huyo mpuuzi alizifanyia tathmini ili kujua kama ni salama kwa Watanzania!?
We dalali wa chanjo tuliza boga hilo!

Uwe na adabu ya kuufyata unapoona watumishi wa Mungu wanazungumza!
 
Mjinga huyo, hapo kanisani watajadili?

Yeye ni mbunge ana nafasi kubwa kuwawakilisha bungeni.

Hivi ilikuwaje Kawe nzima akapewa ubunge huyu mtu
Naamini alishinda kihalali japo wapo wanaoamini alipita kwa goli la mkono la uchafuzi mkuu wa 2020
 
Kwa kuwa Babaako ni boga kakufundisha nawe uwe boga ili mjiuze pamoja usidhani kila mtu anafanya huo ujinga dunya wewe!
Eti Gwajima mtumishi wa Mungu!!! Mungu yupi ZWAZWA wewe! Dikteta Magufuli!?
We dalali wa chanjo tuliza boga hilo!

Uwe na adabu ya kuufyata unapoona watumishi wa Mungu wanazungumza!
 
Una kiwango gani cha elimu?
Wewe pia tukuulize una kiwango gani cha Elimu? Kwa nini Elimu yako haikupi kushtuka kuona chanjo isiyokubalika Amerika, Canada, ulaya na aftika ya kusini ndio tupewe sisi!
 
Mm kwenye swala la chanjo, namwamini, serikali wanatudanganya kwa hili, huyohuyo waziri wa afya gwajima alikuepo kipindi cha mwendazake na alituhimiza kutokuchanjwa leo ndo anahamasisha baada ya mwendazake kufariki, hawana msimamo ni unafiki tu!!

Kuwa na msimamo hakuna maana ya kushikilia jambo hata kama ufahamu mpya unadhirisha awali kulikuwa na makosa.

Kama uliaminishwa watoto wadogo hununuliwa dukani, haina maana kuendelea kukomaa hivyo hivyo hata kama umekuja kufahamu kuwa kumbe huwa wanazaliwa.

Hata hivyo nakubaliana nawe kuhusu vigogo na nadharia za porojo za awamu ile:


Kwa hakika watajwa hapo juu hawatufai. Wanapaswa kuwajibishwa kwa vifo vyote vilivyotokana na ugonjwa huu.
 
Hivi ni kwa nini ma layman ndio wamekuwa vinara wa kuongelea mambo ya kitaalam?
 
Safi sana gwajima!! Hawa wachumia tumbo wanafiki wakubwa!! Wanatudanganya tuchanjwe na kuvaa barakoa, wavae wao na familia zao sisi tuna jina la Yesu lipitalo majina yote
 
Kwa hio Gwajima ana maanisha kwamba Rais Samia ni kigeugeu, si ndio hivyo. Ila yeye hajioni alivyo kigeugeu na alivyo muongo (Waumini wanasubiri ile treni aliowaahidi kununua).


Hongera zake Gwajima kwa kumrushia mawe SSH na kumuita kigeugeu, kweli naamini maneno ya wana CCM kwamba SSH ni dhaifu sana.
 
Kwa kuwa Babaako ni boga kakufundisha nawe uwe boga ili mjiuze pamoja usidhani kila mtu anafanya huo ujinga dunya wewe!
Eti Gwajima mtumishi wa Mungu!!! Mungu yupi ZWAZWA wewe! Dikteta Magufuli!?
Hizo chanjo utazinywa na mashoga wenzio.

Watanzania wamesema hawazihitaji.

Kwa sasa wako bize wanachapa kazi [emoji818][emoji818][emoji818]
 
Asili yake yeye ni Mungu

Israel alikozaliwa Yesu wanaongoza duniani kwa kiwango cha % ya watu wake waliopata chanjo.

Ugonjwa na vifo vimepungua sana huko na maisha yamerudi kuwa kawaida.

Israel wenye vinasaba vya damu na Yesu wanazingatia tahadhari sembuse wewe na gwajima?

Hiiiiii bagosha!
 
Njia zilizotumika kumpatia Ubunge anajua hazikuwa sahihi na haki haikutendeka lakini Leo hii hajawahi popote kuukataa ubunge wake Wala japo kuukubali lakini kutumia kanisa kukemea pale ambapo hakukuwa na haki

Amekywepo kwenye utawala wa awamu iliyopita ambapo tulishuhudia na kusikia watu wakipoteza uhai na kutekwa na watu wasiojulikana, tulishudia risasi adharani lakini hakuna siku amewahi kutoka adharani kukemea uvunjivu wa sheria na katiba ya nchi

Alikuwepo BUNGENI juzi wakati tozo kandamizi zinapitishwa hakuna siku tulimsikia akipinga na kura alipiga ya ndiyo. Hata hao waoumini wake hajawahi kuwaonea huruma, mshahara wake alipi Kodi na hatumsikii akikemea.

Leo anaibuka anaanza kumjadili JPM kwamba wakati wake hakuna aliyeleta chanjo. Je wakati wa JPM wakati watu wanabambikiwa kesi yeye hakuwepo? Alitusemea? Wakati watu wanakufa kwa corona alisema? Wakati tunaficha data alisema? Leo ametoa wapi ujasiri wakutumia nyumba za ibada kutaka kujifanya yeye ni daktari?

Tunaporuhusu watu wa aina ya Gwajima waongoze jamii ndipo tunapozalisha mawazo mgando. Yeye anaamini JPM alikuwa Mungu na kwamba maarifa ya JPM lazima yaheshimiwe hata Kama yalikuwa hayafai, kwamba Leo badala atueleze Mungu anasemaje anatulazimisha tufuate nyayo za binadamu ambaye ana mapungufu mengi ya wazi. Hii dini gani yakuelekeza watu wamwabudu mtu?

Leo ndipo amekuwa na msimamo, mbona huo msimamo upo kwa mambo ya mwendazake haupo kwa wengine?

Huyu mtu apuuzwe, siyo kiingozi wa dini Bali ni Kiongozi wa walafi wa madaraka. Kwenye siasa anataka, kwenye dini anataka na kwenye ushirikina anataka. Yeye Nani wakuombea watu wafe kisa awakubaliani naye? Unasiamama madhabauni unabiri kuua watu unadhani waumini wako wanajitunza Nini? Kwamba wanaokwenda kinyume na mtizamo wako na JPM wafe? Nani kakwambia ninyi ni miungu? Kwamba wewe utokufa?

Nadhani huyu mtu kwa kuwa tu Ni mwana ccm anayo haki yakutumia kanisa anavyojisikia yeye Tena kwa mambo ya hovyo kinyume kabisa na imani yake. Ila ipo siku ataadhibiwa
 
Back
Top Bottom