#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni jambo baya sana kuwapa Chanjo ya Corona Wanajeshi, Polisi na watu wa Usalama

Juzi MBUNGE wa Kawe Askofu Gwajima Alitoa Kauli ya kuwa Walioruhusu CHANJO kutoka NJE kwa Watanzania WAMEHONGWA na Mabeberu ili Kuruhusu Chanjo pia Akawataka Watanzania Waikatae Chanjo hiyo Je Watu hao Waliohongwa ni KINA NANI?
 
Mimi simsikilizi mtu ambaye anaongea mambo ya hewani. Ningeweza kumskiliza kama angekuwa na ushahidi wowote kuonyesha jinsi hiyo chanjo iliyoletwa isivyo salama. Otherwise, hizi ni porojo tu.

Hana justification yoyote ya kile anachokisema. Kwa hiyo, kwa mtu kama huyu natumia 'methodical doubt' ya mwanafalsafa wa Kifaransa René Descartes kutupilia mbali maoni yake.
 
Mkuu, umesoma ukaelewa nilichoandika?

Mbona nimeshaeleza kuwa, Huyo Gwajima Kwa nini asiwe na wasiwasi kwenye madawa mengine au Chanjo zingine isipokuwa Chanjo ya Corona yeye ndio kaiona?

Nani alimuambia Dawa zinazoletwa TANZANIA hazifanyiwi uchunguzi mbali na hiyo Chanjo ya Corona??

Au kihere here cha mdomo wake?

Yeye ni vitu vingapi anavitumia yakiwemo madawa yanathibitishwa na Wataalamu wa kitanzania pasipo kelele wala Matangazo?
Nadhani pia tycon wa fasihi hujapata bahati ya kunielewa.

Nimekwambia mbona hayo madawa mengine vilivyomo ndani na utendaji kazi wake upo wazi?

Corona ni issue mtambuka ndio maana kila mtu anatoa mawazo yake.

Unaona hoja unayotumia kumzuia asihoji inatosha? Eti mbona madawa mengine unatumia?

Je, hayo madawa mengine yamepitishwa kwa emergence pia?
 
Mimi simsikilizi mtu ambaye anaongea mambo ya hewani. Ningeweza kumskiliza kama angekuwa na ushahidi wowote kuonyesha jinsi hiyo chanjo iliyoletwa isivyo salama. Otherwise, hizi ni porojo tu. Hana justification yoyote ya kile anachokisema. Kwa hiyo, kwa mtu kama huyu natumia 'methodical doubt' ya mwanafalsafa wa Kifaransa René Descartes kutupilia mbali maoni yake.
Kwani hao wanaosema ipo salama wana ushahidi wowote kwamba ipo salama? au kwa kuwa mzungu kasema ipo salama.

Wasomi wa bongo trash tupu, sana sana ukikutana na wale waliosomea nje ya nchi wanamuamini mzungu kama baba mungu, mzungu hata akisema mavwi ya mbwa chanjo ya Corona wasomi wa bongo wote wataanza kufuga mbwa. Bora hata nliishia form 4...... shwain
 
Habari za majukumu ya kujenga taifa!

Watu wote wanaoonekana kumpinga, hawaji na majibu mahususi ya hoja za maana za kupinga msimamo wake. Zaidi wanashambulia personality yake badala ya hoja alizotoa.

Wanasema Mchungaji feki, mara mcheza. Mara Sukuma gang, ana maumivu ya kukosa kitu fulani.

By the way huo ni msimamo wake. Cha muhimu hoja alizowasilisha zijibiwe kwa hoja, na kuelezewa kitaalamu kwa wananchi waelewe na kushawishika kwenda kuchanjwa kwa hiari yao bila wasiwasi.

Wakishindwa kuwashawishi wananchi na kuanza kuwashambulia wanaopinga. Maana yake ni kwamba Heshima yuko sahihi.

Ni jukumu la Serikali na wote wanaomwamini chanjo, wafanye juhudi kuhakikisha watu wanaelewa kuhusu umuhimu wa chanjo na kuweza kuchanjwa bila Tashwishi.

Tusishambulie utu. Tushambulie hoja.
 
Kuna kile kijikamati kiliundwa hivi majuzi, kikaja na mapendekezo kwamba wanajeshi wote wadungwe chanjo kwa sababu ati wako kwenye mstari wa mbele wa maambukizi.

Kutokana na ufinyu wa maarifa wa hao wanaoitwa madaktari na wanasayansi wa Tanzania; mpaka sasa hawajaweza kutoa taarifa kamili ya kisayansi kuhusu madhara marefu na mafupi ya chanjo hizo.

Madaktari wetu wanategemea maarifa kutoka ulaya na nchi zingine za magharibi. HAWAJIWEZI.

Ndio maana kabla ya kudungwa chanjo, unapewa fomu ujaze ambayo inasema kwamba SERIKALI HAITAWAJIBIKA KWA MADHARA YOYOTE YATAKAYOKUPATA BAADA YA WEWE KUDUNGWA CHANJO.

Kwa vyovyote vile, chanjo hii haina ithibati ya usalama.

Ni gunia lililotoka ulaya wakalibwaga nchini halafu tunaambiwa tulifakamie.

Kuwadunga chanjo wanajeshi na vyombo vingine vya usalama bila kujiridhisha usalama wake ni jambo ambalo hata fyatu hawezi kulielewa.

Ni vyema serikali iachane na haya machanjo ya ajabu ajabu ya mwendokasi hayafai yataliangamiza taifa.
 
Sio wanajeshi tu bali watanzania wote wanatakiwa wapewe elimu kuhusu madhara ya hizi chanjo zinazopigiwa upatu.

Nikichanjwa naweza kuambukizwa? Ndio 🤣🤣

Nikichanjwa naweza kuambukiza? Ndio 🤣🤣🤣

Nikichanjwa napaswa kuvaa barakoa? Ndio 😂😂😂😂

Nikipatwa na madhara ya hiyo chanjo serikali itawajibika? Hapana 🤣🤣🤣

Watanzania tukatae kwa nguvu hizi chanjo kwa wakati huu wa majaribio! Kataa kutolewa kafara
 
Back
Top Bottom