#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

Attack his points not him
You can't separate his points from himself. We shall pay the costs of bringing these nincompoops in our national assembly. Gwajima is so toxic and detrimental to our population. Whatever he preaches is a product of little education, consipiracy theories and lies. He is a clown who has succeded to brainwash thousands of followers under pretext of resurrection and healing church.
 
Aah wapi Covid imewapiga zaidi hao wazungu kuliko sisi waafrika, kwa hiyo wasitulazimishe tutumie hizo chanjo zao za majaribio. Ukilinganisha vifo vilivyotokea Afrika kwa sababu ya Covid haviwezi kufikia vifo vinavyosababishwa na Malaria.

Kwa hiyo changamoto yetu kubwa Africa bado ni Malaria siyo Covid. Wangekuwa wanatupenda wangeharakisha upatikanaji wa chanjo ya Malaria.
Ndo maana nasema hampendi kujifunza wala kufuatilia mambo,we bado ume stuck in first gear kuhusu covid 'imewapiga sana uk',ni kweli lakini hiyo ni ugonjwa ulipoanza na wakajipanga na kuji organize na leo hii covid haiui kama mwanzo,sidhani hata kama watano wanafika kwa siku.Wamejifunza na wakajikita na chanjo na sasa nchi imeanza kufunguliwa huku waki monitor na hali ikiendelea vizuri mwezi ujao wanarudi kama zamani.Corona itabaki lakini haitopeleka watu hospital kuwekewa ma oxygen wala kuua.Sababu watu watakuwa wana chanjo.
Nakubali sio vizuri kulazimisha chanjo kwa wasiotaka bongo,lakini elimu ya chanjo itolewe kwa wote ili watu wajue ukweli,tena waongeleaji wawe wataalamu sio watu wanaofikiri 5G ndo inaleta corona.
 
Sisi watanzania wabishi Sana na wagumu Sana wa kuelewa.basi Bora hizo chanjo zije kiasi kidogo kwanza.wanaotaka wapigwe,Ila wasilazimishe kupiga iwe hiari.
 
Point yako haina mashiko, chanjo ya homa ya manjano imekuwepo kwa zaidi ya miaka 70, na tafiti nyingi zimefanyika zikishirikisha nchi nyinyi Tanzania ikiwemo. Leo hii nionyeshe nchi ambayo inazalisha chanjo ya Corona walikubali kumshirikisha mtu au nchi yoyote ambayo inanunua chanjo ya corona. Unachopewa ni chanjo na kuambiwa tuambia hao uliowachanja wamepata madhara gani. kwa kifupi we are guinea pigs na mtu kama wewe unakubali tu. Nchi kama Kenya na Rwanda walikuwa wanashangilia walipopewa chanjo, soon after, side effects zikanaza kujitikeza kila kona. Leo hii wao wanahali mbaya kuliko sisi ambao we didn't care less.

Umesema vyema , Wizara isipuuze hoja za gwajima wazifanyie kazi
 
Kwanini kila siku kutolea makosa Vaccine za nchi zingine?
Kwanini mtu kama una wasiwasi usitengeneze Vaccine yako? Iran katengeneza Vaccine yake,Russia pia katengeneza Vaccine yake,hiyo ndio solution kama huamini vya wenzako.
Sidhani kama tatizo kuwa ni vaccine za watu wengine bali kinachotiliwa shaka ni vaccine zenyewe za corona kiujumla na sababu zinatolewa, vaccine za kuwa za wengine sio issue ndio maana hadi sasa zipo vaccine zengine ambazo hazijapingwa zinaendelea kutumika.
 
Wangekuwepo watu wasio na akili kama Gwajima wangepinga. Tena Bahati mbaya sana ana jina la kufanana na Waziri wetu wa Afya..

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Sisi watanzania wabishi Sana na wagumu Sana wa kuelewa.basi Bora hizo chanjo zije kiasi kidogo kwanza.wanaotaka wapigwe,Ila wasilazimishe kupiga iwe hiari.
Tatizo la wabongo unaweza kuona watu humu mitandaoni wengi tu wanasema hivyo zije wao watachanjwa ila ikitokea zikaletwa kweli hao watu watanyuti kusikilizia kwanza hadi wengine waanze wakati wao ndio waliyokuwa wanazililia huku mitandaoni, mambo haya ndio yapo hata kwenye maandamano unakuta humu mitandaoni kumechafuka ila siku ya tukio wananyuti wanasikilizia huko mtaani pakoje.
 
Wangekuwepo watu wasio na akili kama Gwajima wangepinga. Tena Bahati mbaya sana ana jina la kufanana na Waziri wetu wa Afya..

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
Kuita mtu hana akili kwa kutofautiana tu mawazo sidhani kama ni jambo sahihi, unajua tatizo inatumika nguvu kubwa kuzuia mawazo pinzani kwenye hili suala la covid 19 hata huko YouTube na Facebook ukiweka chochote chenye kupingana na WHO kinahesabika na upotoshaji na hufutwa.
 
Mtu katoa hoja, kwanini usijibu kwa hoja?

Yupi aliyetoa hoja na hakujibiwa kwa hoja?

IMG_20210512_105300_905.jpg

Unaongelea mavi ukijibiwa kama ulivyokuja unaanza kulia lia kujaribu kuwalagai ambao hawakujua ulianza je na eti sasa ghafla wataka hoja?

Hoja gani uliyo nayo wewe ili ujibiwe?

Waliosema Garbage In Garbage Out hawakukosea.
 
Yupi aliyetoa hoja na hakujibiwa kwa hoja?

View attachment 1781765

Unaoungea mavi ukijibiwa kama ulivyokuja unajaribu kuwalagai ambao hawakuja ulianzaje kudai ujibiwe hoja?

Hoja gani uliyo nayo wewe ili ujibiwe?

Waliosema Garbage In Garbage Out hawakukosea.
Gwajima katoa hoja, ni kwanini tu usijibu kwa hoja?
 
Huyu Gwajima hana sifa ya kuwa mtumishi wa Mungu, ni kigeugeu kila siku.

Sijui ni mwepesi kusahau anayoyasema au anahisi watu tunasahau anayoyasema.

Kipindi Corona inaingia Afrika akiwa madhabahuni akaiapisha na kusema haitaingia Tanzania waumini wake wanashangilia.

Mara inaingia, akageuza kibao kusema anataka akaikomeshe Corona kwa kuruhusiwa kwenda hospital kuwaombea wagonjwa waumini nao wanashangilia.

Sasa anaongea mengine asiyojulikana.
View attachment 1781691
Sawa ni kigeugeu tumekubali, na hana sifa ya kuwa mtumishi, tumekubali. Haya sasa, jibu hoja zake.
 
Nlisali Kwake akiwa pale ubungo maji nkatafakari sana mahubiri yake hayakuniingia nliona ni walewale wapanga madeal na waumini wao ili wajinga waamini miujiza stakagi kuskia porojo zake.....alishindwa kuzuia kifo cha jiwe atatuambia nn kipya
Sawa kashindwa kuzuia kifo, ila jibu hoja zake kwa hoja sasa
 
Gwajima katoa hoja, ni kwanini tu usijibu kwa hoja?

Gwajima hana ufahamu wowote wa chanjo, microbiology, viruses wala mutations za viruses.

Gwajima ni mtalaamu kidini mwenye kipawa cha kufufua wafu.

Wataalamu waliobobea kwenye chanjo, microbiology, viruses na mutations zao ni hawa hapa:

"Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara."

Tokea kwenye chapisho lao hili hapa:

Nitamsikiliza Dr. Manyahi kuhusu masuala ya virusi vikiwamo vya Corona.

Nitamsikiliza Askofu Gwajima hasa kwenye eneo lake la ufundi - kufufua wafu.

Simple logic. Tusilazimishane kumeza hata kama ni utopolo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hivi unaelewa kweli ulichoandika? Kwa hiyo hoja uliyoandika inapingana na mawazo ya Gwajima?

Ninaelewa 100% ya nilichoandika. Nichukue wasaa huu kujiuliza pia:

"hivi na wewe unaelewa kuwa kuna watu wanasomea na kubobea kwenye virusi kama fani na kuwa Gwajima siyo mmoja wao?"

😂😂😂😂😂😂😂!
 
Tupe basi wewe hayo unayosema kwani inahitaji PhD kujua tu side effects za dawa na inavyofanya kazi?
Aliekwambia kila dawa unazo tumia kila siku hazina effect ni nani mbona hujaacha kutumia, tunaangalia kiwango Cha effect, Hata wakati chanjo za pcv13 ,rota, wakati tunaanza zitumia kwenye mwaka 2012/ 2013 zipo batch zilikua na shida KWA leta reaction, but mpaka Sasa Zinafanya vizuri ,so usitegemee utapata dawa chin ya jua ambayo haina side effect, chanjo ije asietaka kuchanja Basi anaetaka achanje leo tz ndo tunajifanya tu wajuvi wa Mambo ya tiba too shame ,
 
Gwajima hana ufahamu wowote wa chanjo, microbiology, viruses wala mutations za viruses.

Gwajima ni mtalaamu kidini mwenye kipawa cha kufufua wafu.

Wataalamu waliobobea kwenye chanjo, microbiology, viruses na mutations zao ni hawa hapa:

"Akizungumza na Mwananchi, Mtaalamu wa maicobaolojia na virusi kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (Muhas), Dk Joel Manyahi alisema aina hiyo ya kirusi kina tabia ya kujibadilisha mara kwa mara."

Tokea kwenye chapisho lao hili hapa:

Nitamsikiliza Dr. Manyahi kuhusu masuala ya virusi vikiwamo vya Corona.

Nitamsikiliza Askofu Gwajima hasa kwenye eneo lake la ufundi - kufufua wafu.

Simple logic. Tusilazimishane kumeza hata kama ni utopolo.
Hayo yote sijabisha, ila jibu hoja zake, kwanini usijibu hoja kwa hoja?
 
hawa jamaa si huwa wanafnya miujiza kila siku si watusaidie tu hili janga liondoke au hii miujiza haiwez kufanyika kwe ngazi ya kitaifa?
Kuongea vile alivyoongea nao ni muujiza.Kwa sababu hapo mwanzo kulikuwepo na neno nae neno alikuwa ni Mungu.
 
Back
Top Bottom