#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

Point yangu ni kwamba hizo takwimu za vifo vya magonjwa mbalimbali ambazo zipo kila mwaka ila ni kama kwamba sasa vimegeuka na kuwa vifo vya corona, lakini pia kama nilivyosema kipindi cha mwanzo mwaka jana watu wenye matatizo kama hayo ya moyo walikuwa wanaogopa kwenda clinic kwa kuogopa huko hospitali watapata corona,sasa hali ile ingekuwa inaendelea unadhani ingekuaje?
 
Mkuu ni sahihi mtu aliekutwa na virusi basi anaingia kwenye takwimu moja kwa moja. Nimeweka neno la kiengereza hapo kwenye machapisho yaliopita "cause of death is complications related to covid-19". Hii haimanishi umekufa na corona, labda kiswahili fasaha mtu amekufa na athari/changamoto zinazosababishwa na virusi vya covid-19.

Nimesema hapo awali uwe na maradhi ya aina yoyote au uwe na afya mzima, ukifa ukipimwa una virusi unaingia kwenye takwimu. Wapo watu hadi watoto wadogo waliokufa na covid-19. Kwani strategy yako ni ipi kukusanya hizo data za vifo vinavyohusishwa na haya maradhi ?
 
Kufanya hivyo inafanya tuwe na takwimu za vifo vingi vya corona hali ni kwamba kuna vifo ambavyo havikusababishwa na corona, lengo la kufanya hivyo ni lipi?
 
we have people who have been fully vaccinated against covid(Bill Maher etc) ,wanakuja kua re-infected against na hiki kirusi,,if that doesn't raise alarm bells ,I don't know what does?
 
Tangia lini aonaye akaongozwa njia na kipofu ambaye wala hana fimbo ya kukong'otea (vifaa vya kuhakiki ubora wa hizo chanjo)? Hoja ya Gwajima ni ya kusherehesha bunge tu.
 
Achana nao. Mwendazake kawakaririsha. Wanaimba kama kasuku.
 
Kufanya hivyo inafanya tuwe na takwimu za vifo vingi vya corona hali ni kwamba kuna vifo ambavyo havikusababishwa na corona, lengo la kufanya hivyo ni lipi?
Uwezekano wa kufariki ukakutikana na virusi vya covid-19, halafu sababu ya kufariki ikawa nyengine ni mdogo mno. Hususan kama umri wako uko juu au una maradhi mengine kama moyo, sukari, mapafu n.k. Kwa mtu mwenye afya yake labda hii inaweza kuwa tofauti kidogo tuu, lakini symtoms zinajulikana nyingi related to breathing system.

Labda kwa mtu asiefahamu huu ugonjwa unasumbua kiasi gani ndio ataweza kuleta mawazo mengine. Naishi kwenye nchi ambayo tatizo hili lipo kwa miaka takriban 2 sasa. Mwanzoni ilikuwa wengi wanaopokelewa emergency ni wazee baada ya wengi wao kupigwa shots. Data zinaonesha vijana wanaongoza (ambao ndio wanaanza kuchomwa vacine).

Data does provide light on how one should look into this subject. Without it we are doomed!
 
we have people who have been fully vaccinated against covid(Bill Maher etc) ,wanakuja kua re-infected against na hiki kirusi,,if that doesn't raise alarm bells ,I don't know what does?
Hakuna chanjo 100% ndio maana katika kila watu laki 1 lazima utakuta elfu 1 ambao chanjo haiwi effective kutokana na variation za miili na afya.

Mfano mtu mwenye UKIMWI can chanjo be effective? As compared tu mwenye kinga imara?
 
"Uwezekano wa kufariki ukakutikana na virusi vya covid-19, halafu sababu ya kufariki ikawa nyengine ni mdogo mno"

Kama hakufanyiki vipimo zaidi kujua chanzo cha kifo basi hiyo unaweza kuongea kauli kama hiyo, lakini pia takwimu za vifo ikoje kabla ya corona? kwa watu wenye matatizo kama hayo ya moyo sukari mapafu n.k na hata baada ya uwepo wa corona uangalizi wao ukoje kwa waru wenye magonjwa kama hayo? maana wanahitaji uangalizi wa karibu sana.
 
Sasa mtu alikuwa anaishi vizuri na maradhi yake ya moyo au sukari. Halafu ghafla kashindwa kupumua (symtoms related to covid-19) akafia hospitali. Wewe unataka tuseme amefariki na sukari. Tokea lini mtu wa sukari au moyo akawa na matatizo ya kupumua ? Naona bora tufunge chapter, au kwa mameno mengine tunakupa mji 😀
 
WHO wametoa muongozo na nchi zote duniani kasoro TZ, wamekusanya data kwa namna hii na zimewasaidia kuokoa maisha ya watu. Endeleeni kufukiza na kula miti shamba....wait pengine hata tatizo halipo maana hakuna test results kwa hio hatujuwi kama covid-19 ipo au haipo....🤷‍♂️
 
Tangu afe huyo mwendazake, mbona hatushuhudii tena vifo mfulilizo vya Viongozi? Au hiyo Corona ilikuwa ni kwaajili yake na Viongozi wenye misimamo kama yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Acha hizo, bhana! Ina maana wewe tofauti ya hivi vitu huioni? Mtu mmoja anakuambia, “possible side effects za ABC ni 1, 2, 3, et cetera” na mtu mwingine anakuambia, “possible side effects za XYZ hatuzijui, lakini bado tunaendelea na utafiti”. Are they talking about the same degree of risk?

Uamuzi wa kukubali chanjo ambayo short-term, medium-term and long-term side effects zake hazifahamiki ni reckless by any standard. Ni kama kukubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia!
 
Kwamba Radiotherapy haina madhara kwa above 20% ya watumiaji wake? Ila hampingi ila mnapinga chanjo ambayo risk ipo kwa 0.0001 ya waliodungwa wote? Duh
 
Kwamba Radiotherapy haina madhara kwa above 20% ya watumiaji wake? Ila hampingi ila mnapinga chanjo ambayo risk ipo kwa 0.0001 ya waliodungwa wote? Duh
Inakuwaje mtu ankubali risk ya kufukuzwa na watu wenye mapanga na kura bandia kisha baadae anakubali kuwa waliomfukuza na mapanga wameshinda na uchaguzi haukuwa na mapungufu?
 
Mzee Gwajima we utaalam wako ni kufufua misukule - huku kwenye chanjo na utatibuu ulikovamia waachie wenyewe.
 
Chanjo hizi zimeharakiswa mno hata waliozitengeneza hawajuwi madhara ambayo bado hayajajitokeza kwenye mwili wa mwanadamu.
Lakini wanaendelea kuzigombania!. Nimeona mahali Umoja wa Ulaya wameishtaki kampuni inayotengeneza chanjo ya corona kwa kushindwa kuwapatia idadi ya chanjo walizokubaliana,
Maana yake, pamoja na madhara yanayojitokeza na yanayoweza kujitokeza, wameona kwa sasa hiyo ndiyo njia iliyopo kwa kuwa haya madhara ni kidogo. Nilisikia kule Marekani kuwa kati watu milioni saba waliochanjwa chanjo hiyo, ni sita tu ndiyo walipata mgando wa damu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…