PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hilo lisikupe faraja.
Endelea kuwa na matumaini hayo, hata kama hayana msaada wowote kwenu.

Haya yote mmeyatengeneza wenyewe; kwa bahati mbaya sasa hamna uwezo wa kuyazuia yasiwafyekelee mbali.
Lissu hana uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike. hizi ni siasa za kwenye magazeti na instagram huwa zinawafikia wachache sana sio zaidi ya watanzania milioni 5.

Kuna hao milioni karibu 60 walio mbali kabisa na uanaharakati wa kwenye media.
 
Wasalaam
Kuna msemo usimao ngoma ikivuma sana hupasuka.
 
Attachments

  • b660f87522cd9c342408f4f1704f8d17_1748858793062.mp4
    4 MB
Lissu hana uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike. hizi ni siasa za kwenye magazeti na instagram huwa zinawafikia wachache sana sio zaidi ya watanzania milioni 5.

Kuna hao milioni karibu 60 walio mbali kabisa na uanaharakati wa kwenye media.
Nani kasema "Lissu anao uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike"? Umesoma mahali popote nimeandika hivyo mimi?
Kila mara unageuza geuza maneno; mtindo ule ule unaotumiwa na Samia, wewe, Tlaatlaah... Huu utamaduni mmeurithi toka wapi?
Hao waTanzania milioni 60 mnawafuga nyinyi, ni mifugo yenu?
 
Ukishakula nyama ya mtu katu HUWEZI acha RIP Mdude damu yako haitoenda bure itajibu kama ya Azory
Inauma sana kuona mwanamke anaejiita Rais ndie anahamasisha mauaji ya Watanzania..... Ila ajue hata yeye atarudi mavumbini
 
Mwanaharakati ambaye nguvu yake inaanzia na kuishia humu humu mitandaoni, pole sana.
 
Mwanaharakati ambaye nguvu yake inaanzia na kuishia humu humu mitandaoni, pole sana.
Sasa pole ya nini, wakati tupo wote humu?
Utatambua tu ndani ya muda hayo unayotaka kuyaona mitaani.
Inashangaza sana uduni wenu wa akili, kudhani kwamba mtaifanya Tanzania kuwa eneo lenu la kufanyia uchafu.
 
Uduni wa akili mnao nyinyi mnaodhani kuwa mnaweza kuupata uongozi wa Tanzania kwa hizi siasa nyepesi za mitandaoni.

CCM wapo kila kona ya nchi hii wakiwa karibu kabisa na maoni pamoja na mahitaji ya wananchi, hizi siasa zinazoishia kwenye majiji manne tu haziwezi kuwapatia hii nchi.

Watanzania hawahitaji kufanyia majaribio masuala nyeti ya kiuongozi.
 
Hao CCM mnaowatanguliza mbele kama pambo la kuwahadaa watu nalo mnadhani watu bado hawajui kinachoendelea?
Mnaitumia CCM kufanya uovu wenu, halafu mnaendelea kutegemea kuwa itawalinda mbaki madarakani?

Nyinyi wenyewe mnaiogopa CCM, ndiyo maana hamkuwa tayari apitie taratibu za miaka yote kuteuliwa kuwa mgombea wa chama hicho; halafu unakuja hapa kama huna akili kichwani kuzungumzia CCM?

Mnacho kitegemea kukitumia chama hicho ni kuhalalisha uvurugaji wa kura za wananchi kwa kutumia muundo wa chama hicho. Hili nalo safari hii haitawezekana.

Ungekuwa na akili kidogo kichwani ungeelewa kwa nini Samia anaogopa sana kuwepo kwa marekebisho ya taratibu za uchaguzi ili wananchi wawachague viongozi wao kwa uhuru na HAKI. Lakini hata ukijuwa haya, bado unajizima akili ukidhani kufumba macho ndiko kutazuia Samia kukataliwa.
 
Hata ukibadilisha hizo kanuni za uchaguzi hakuna namna Lissu au yoyote wa upinzani anaweza kumshinda Samia kwenye sanduku la kura.

Samia kaigusa nchi nzima, hawa wanaharakati siku zote wanaishia kwenye malalamiko na mbwembwe nyingi za humu mitandaoni.

Kosa lenu ni lile lile la miaka yote, kushindwa kwenda sambamba na mahitaji mapana ya watu walio wengi.
 
Hata ukibadilisha hizo kanuni za uchaguzi hakuna namna Lissu au yoyote wa upinzani anaweza kumshinda Samia kwenye sanduku la kura.
Sasa ni kipi anachokiogopa yeye?
Akubali hizo taratibu zirekebishwe, ili kuepusha kumwaga damu ya waTanzania kwa sababu tu ya yeye kutaka kubaki madarakani kwa nguvu.
Huoni thamani ya maisha ya binaadam mwenzako?

Huna lolote la ziada hapa, unabaki kuimba tu ngonjera zilezile kama ilivyo kawaida yako.

Hii tabia siyo ya kawaida, inawezekana ni athari inayotokana na umwagaji wa damu za watu wasiokuwa na hatia. Nimejaribu sana kukusoma vizuri siku za hivi karibuni. Hali yako ya afya ya akili inazidi kuzorota siku hadi siku.
 
Baada ya kanisa kufungwa, hatayumba na msimamo wake kweli! Kanisa ndio maokoto yenyewe!
 
Mnapokosa hoja mnakimbilia kuandika hisia za kusadikika.

Kuna vyama vingi vipo tayari kuingia kwenye uchaguzi mkuu kwa kutumia hizi hizi kanuni zilizopo.
 
Mnapokosa hoja mnakimbilia kuandika hisia za kusadikika.

Kuna vyama vingi vipo tayari kuingia kwenye uchaguzi mkuu kwa kutumia hizi hizi kanuni zilizopo.
Lakini huwezi kueleza kwa nini hizo kanuni kwenu zinakuwa ni msahafu.
Huko ndiko kukosa hoja kwenyewe. Mtu kama wewe huwezi kulielewa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…