PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askofu gwajima asema CCM si chama cha utekaji, na kinapinga kwa nguvu zote kama yeye anavyofanya. Asema utekaji si sera ya CCM, ataendelea kuipenda CCM lakini kwenye utekaji atakataa milele.

Asema ukiona anaongelea utekaji na watu wanampinga basi wapo watu wanajua hiyo itakuwa inamaanisha nini.

Kenge hatuhitaji D2 kuelewa si ndio?🌚
Yani leo lijamaa limenyooka. Lazima Samia atoe mlio tena.
 
Kuna haka ka kenge kanajiita lucas mwashamba

IMG_1486.jpeg
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=NhpB9Zh2_6Y

Askofu Gwajima ameanza kwa kuwaambia waumini wasimame na kuimba wimbo wa 'Tanzania Tanzania', na kuongeza japokuwa tuna makabila tofauti tofauti lakini Tanzania ni yetu sote.

--
Gwajima anawaelezea waumini kuhusu mkutano wa waandishi wa habari aliofanya kuhusu suala la utekaji nchini lakini pamoja na mapendekezo aliyotoa kuhusu uteuzi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Anasema baada ya kuongea, Sheikh Jabiri huko Zanzibar alitekwa juzi tarehe 28 na mwili wake kupatikana ukiwa umetelekezwa. Watekaji wanateka MwanaCCM na watu wengine.

Chama cha Mapinduzi hakikubali utekaji, na mimi ni mwanachama wa CCM, hivyo naungana na waasisi na waliowahi kutangulia uongozi kuwa hatukubaliani na hili. Anayeteka watu ni kwa malengo yake mwenyewe. Yeyote anayepingana na mimi wenyewe mtajua mtamuitaje.

Gwajima ameongezea mifano ya watoto wa viongozi (Mwinyi, Kikwete, Majiliwa, Magufuli) ikiwa watatekwa na kung'olewa macho wazazi wao watajisikiaje?

Baada ya kukemea mauaji na utekaji, imezaliwa terminology ya Gwajimanization.

Kwenye hili suala sitayumba, nitahakikisha kila aliyetekwa yuko wapi na anafanya nini. Vaeni silaha kamili za Bwana ili kushindana na pepo wabaya na tutashinda.

Kwa CCM, Gwajima ni hazina yenu, mnaye mtu ambaye hamjamjua bado. Ni mtu wa Mungu wa watu wote. Natetea waislam waliotekwa, Wakristo waliotekwa bila kujali chama. Kama mtu amekosea si apelekwe mahakamani. Vyombo vya ulinzi na usalama hawateki, bila shaka kunaweza kuwa na kakikundi ka utekaji na ndiko nakatumia ujumbe.

Naishia hapo, ila mtu akinichokoa chokoa, nitaitisha press. Na nikiitisha ya pili moshi utafuka hutoweza kufumbua macho.

Tutashusha maombi, ili damu ya mtu anayetekwa imrudie yule anayeteka.

Tunaomba iliyorekodiwa yale makombora yake ya awali kanisani.
Live streaming nimeshindwa kuwa na kumbukumbu.
 
Back
Top Bottom