Auto-Marvelt
JF-Expert Member
- Jul 13, 2019
- 2,661
- 5,583
Mwenye List ya waliompinga tafadhali
View: https://www.youtube.com/watch?v=NhpB9Zh2_6Y
Askofu Gwajima ameanza kwa kuwaambia waumini wasimame na kuimba wimbo wa 'Tanzania Tanzania', na kuongeza japokuwa tuna makabila tofauti tofauti lakini Tanzania ni yetu sote.
--
Gwajima anawaelezea waumini kuhusu mkutano wa waandishi wa habari aliofanya kuhusu suala la utekaji nchini lakini pamoja na mapendekezo aliyotoa kuhusu uteuzi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Anasema baada ya kuongea, Sheikh Jabiri huko Zanzibar alitekwa juzi tarehe 28 na mwili wake kupatikana ukiwa umetelekezwa. Watekaji wanateka MwanaCCM na watu wengine.
Chama cha Mapinduzi hakikubali utekaji, na mimi ni mwanachama wa CCM, hivyo naungana na waasisi na waliowahi kutangulia uongozi kuwa hatukubaliani na hili. Anayeteka watu ni kwa malengo yake mwenyewe. Yeyote anayepingana na mimi wenyewe mtajua mtamuitaje.
Gwajima ameongezea mifano ya watoto wa viongozi (Mwinyi, Kikwete, Majiliwa, Magufuli) ikiwa watatekwa na kung'olewa macho wazazi wao watajisikiaje?
Baada ya kukemea mauaji na utekaji, imezaliwa terminology ya Gwajimanization.
Kwenye hili suala sitayumba, nitahakikisha kila aliyetekwa yuko wapi na anafanya nini. Vaeni silaha kamili za Bwana ili kushindana na pepo wabaya na tutashinda.
Kwa CCM, Gwajima ni hazina yenu, mnaye mtu ambaye hamjamjua bado. Ni mtu wa Mungu wa watu wote. Natetea waislam waliotekwa, Wakristo waliotekwa bila kujali chama. Kama mtu amekosea si apelekwe mahakamani. Vyombo vya ulinzi na usalama hawateki, bila shaka kunaweza kuwa na kakikundi ka utekaji na ndiko nakatumia ujumbe.
Ponjoro wa Kinondoni anachezesha kamari ambazo hata Mungu hapendi, mimi nilitaja watoto wa watu wengi ila Ponjoro kasikitika kisa mtoto mmoja niliyemtolea mfano. Nampa onyo, nikimuamkia atabaki vipande vipande na atanuka kinyesi maana mimi ni Jasusi la Mbinguni.
Naishia hapo, ila mtu akinichokoa chokoa, nitaitisha press. Na nikiitisha ya pili moshi utafuka hutoweza kufumbua macho.
Tutashusha maombi, ili damu ya mtu anayetekwa imrudie yule anayeteka.
Ni ka kiume mbona weupe wake si wa kawaida?
Ndo iko vivyo.Mtumishi wa Mungu anazidi kuwachachafya watekaji na wauaji wa Wawatanzia.
Aaapa mbele za Mbingu, ataendelea kuwachachafya Hadi Utekaji Ukome mara Moja.
Chadema ni lini mtamchukua huyu Chizi maana ndio mnawapenda watu wa aina ya huyu mzeeMtumishi wa Mungu anazidi kuwachachafya watekaji na wauaji wa Wawatanzia.
Aaapa mbele za Mbingu, ataendelea kuwachachafya Hadi Utekaji Ukome mara Moja.
Unaweza kuangalia Live kwenye Youtube yake muda huu link hyo hapo
View: https://www.youtube.com/live/NhpB9Zh2_6Y?si=uZS3utczNbmB1b1A
Ningekuwa na uwezo aisee huyu Gwajima ningempiga risasi hadharaniYaani anataka kusema hata Samia ndio mtekaji huyu ashikwishwe adabu...
Mibutuano tu mkuu, hakuna lingine tofauti.Nina uliza Nini linaendelea kati ya gwajima na Samia?
Unaweza kuangalia Live kwenye Youtube yake muda huu link hyo hapo
View: https://www.youtube.com/live/NhpB9Zh2_6Y?si=uZS3utczNbmB1b1A
Kuna mtu alitabiriwa hiko kitu huu mwakaNingekuwa na uwezo aisee huyu Gwajima ningempiga risasi hadharani