Askofu Gwajima: Tanzania inashindwa kuendelea mbele kutokana na kutokuwa na muendelezo wa utawala mmoja kwenda mwingine

Sababu hatuna NATIONAL POLICY, hakuna Takwa la Kikatiba linalotoa mwongozo kila Rais anaefuata afanye nini. Kama Katiba inasema ushauri anaopewa Rais na wasaidiz wake ana hiari wa kuufuata au kuachana nao, kuna jipya gani linaloweza kutendeka ili kua na mwendelezo? Katiba mpya ingeweza kurekebisha dosari!
 
Hata Mkapa aliwahi kuliongelea hilo, hiyo ni dalili kuwa CCM hawana uwezo wa kuongoza taifa hili. Ila tutafanyaje sasa maana hata hao upinzani ndio hawako serious kabisaaaa.
 
Hata Mkapa aliwahi kuliongelea hilo, hiyo ni dalili kuwa CCM hawana uwezo wa kuongoza taifa hili. Ila tutafanyaje sasa maana hata hao upinzani ndio hawako serious kabisaaaa.
Walishawahi kutawala hata awamu moja ili tujue kuwa upinzani ni tatizo?
 
Kama waziri mkuu anaomba pesa nyingiiii za matumizi alafu kiduchu kwa ajili ya maendeleo unategemea nini hapo? uozo
 
Mbaya zaidi walisema amefanya makubwa hayo makubwa ni yapi kama siyo maendele?
 
Sikweli 'it ia a big NO'
 
Ameongea point sana , leo hi iko wapi
Kilimo kwanza, sijui big results now hatujui zilipo ishia na achievement zake , tuka anza upya tz ya viwanda , madenge , na mengine , nini suluhisho
Cha kwanza ni katiba ibadilishwe Rais awe guided kuhusu mtazamo wa Taifa sio aje tu na mambo yake
Tuna resources nyingi lakini kama Taifa tuna zi overlook, Embu tufanye decentralization kila kanda isimamie resources zake vizuri ayo madini aliyo yataja Gwajima , unakuta hata Waziri wa madini hajui yapo katika mikoa gani lakini
ninacho amini ni kwamba kila eneo katika Taifa hili lina potentials na resources zake ambazo Kama zikisimamiwa vizuri tutaendelea tu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sio mshabiki wake kutokana na namna alivyopata huo ubunge lakini hapo ameongea jambo la maana sana.
Hasa kutokuwa na malengo na vipaumbele vya pamoja vya maendeleo kama taifa.

Ili wagombea wetu wa urais wakati wa kugombea kazi yao iwe ni kutuambia watatumia mbinu na njia zipi katika kuyatimiza hayo malengo na si kilamgombea kuja na ilani na mipango yake binafsi.
 
ameongea kitu cha maana sana, ameongea point sana na ameonyesha uwezo mkubwa kichwani na nia njema kwa tz. ila sijapenda alipomalizia kwa subihana wataala na Yesu sijui nini nini.....najua anaongea kitu ambacho hakitoki moyoni mwake. mimi huwa napenda mtu real, ukiona moyoni mwako ipo dini moja tu, acha usiongelee zote, nyamaza , kuliko kuongea kitu kilicho usoni ila moyoni unang'ong'a.
 
Jamani jamani why not give mama Samiah na sisi a break?Jiwe amekwenda na mambo yake, mwacheni mama aendelee na mipango yeye ndio Rais kwa sasa, tusipangiane tafadhali!
Nyokoo, tusipangiane ndio nn..... Hata CCM tunaitaka hiyo katiba mpya
 
Kweli mkuu tunatubu
 
Ameongea vizuri.. kimsingi, maneno yake yanataka
1. Katiba mpya, ili akija raisi asiye mzuri asichafue
2. Kuimarisha mifumo
 
Gwaji boy ni hopeless, concerns zake zote zingetimizwa kwa kupitia katiba mpya na HURU, Cha kushangaza wakati wapinzani walipokuwa wakizungumzia kuhusiana na KATIBA wao Ccm hawakutaka hata kusikia habari hizo, kwa kifupi wanadhani Katiba mpya ni kwa faida ya wapinzani
 
Vizuri sana
 
Ameongea vizuri.. kimsingi, maneno yake yanataka
1. Katiba mpya, ili akija raisi asiye mzuri asichafue
2. Kuimarisha mifumo
Kati ya michango Bora katika Bunge letu hili, ni huu, na bila Shaka tumechelewa Sana sababu ya kukosa miunganiko kutoka utawala A Hadi B n.k

Tukiweza hili, tutaondokana na mipango na vision ya mtu mmoja anayeitwa Kwa cheyo cha Raisi na badala yake itakuwa, maoni na mawazo ya wengi ndio yanaongoza nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…