PreGE2025 Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!

PreGE2025 Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Askofu Gwajima amesema Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuwa entertained

Gwajima anasema huwa haongei kwa kubahatisha, mpaka anakuja kuongea mbele za watu ni kwasababu ana data, na data hizo amekuzikusanya kutoka matukio yaliokuwa yanafanyika miaka kadahaa na kupata orodha ya watu takribani 83 waliopitia matukio haya ya utekaji, amewataja Mzee Soka, Mdude Nyangali, wanaharakati wa Kenya na Uganda na wengine wengi akijenga hoja kuwa kuendelea kunyamaza Katika Hali hii hauwezi kujua atayefuata kutekwa ni nani, hivyo Bora kusema na kushauri Ili mambo yatatuliwe.

"Utekaji si utamaduni wetu wa kitanzania na ni jambo ambalo halitakiwi kuvumiliwa na mtu yeyote, nitoe mfano mimi natokea jimbo la Kawe kuna huyu bwana anaitwa Ali Kibao alikuja akashushwa kwenye gari watu wanaona, abiria wote wanaona halafu kesho yake akapatikana amekufa"

"Nataka nimuulize mtu yeyote kama baba yako akishushwa mbele yako wewe mwenyewe halafu kesho yake akapatikana amekufa utajisikiaje? lakini siyo huyo tu, tumeona juzi juzi kule Mbeya mtu anaitwa Mdude"

"Watu wamekuja nyumbani kwake wamevunja mlango wamemchukua akiwa hai mbele ya familia yake wameondoka nae na mpaka leo hatujui yuko wapi na hatujui nani sasa anaefuata unaweza ukanyamaza kumbe unafuata wewe"

"Juzi juzi hapa tena mwanaharakati wa Uganda anaitwa Agather Atuhaire amekuja hapa amehudhuria mahakamani huyo mtu amechukuliwa na watu waliojitambulisha kama watu wa vyombo nimeona anaongea kwenye Youtube"

"Kwa uchungu kabisa kwamba wakaenda mahali akavuliwa nguo akafanyiwa udhalilishaji na akaenda kutupwa mpakani, sasa hebu tujaribu kuwaza kama angekuwa ni mama yako mzazi anachukuliwa anavuliwa nguo anadhalilishwa anatupwa mahali ungejisikiaje au kama angekuwa ni dada yako kabisa wa tumbo moja"

View attachment 3344279
Uteo ni mbinu inayotumika sana na Watawala wadhalimu ili kuwatisha Watu wasiweze kuhoji juu ya Udhalimu unaofanywa na Watawala
 
..Rev ni kama anauliza kwamba hao WATEKEJI wana MBINU,MAARIFA na UWEZO kuliko Vyombo vyetu vya Usalama??
 
Hapa kuna tatizo la kuelewa hawa wanasiasa ni wachawi sasa inakaribia uchaguzi ndio anasema kuna matokeo yakupotea watu na kupigwa Risasi awamu ya 5 Alikuwa wapi lakini tumeelewa Rais Samiha atarufi kwa kishindo mpaka 2030
 
Jumapili itabidi nifike ufufuo na uzima maana mtu wa maana kabisa Gwajima hanaga shoo ndogo shoo zake za kibabe.

Mulaga musiba alitahadharisha mapema ccm iweke lineup iliyoshiba akiwemo Polepole ili ku counter hoja.za.upinzani akirefer TAL. Dr Slaa. JOHN Heche na Mnyika.

Gwajima mtu ambaye angekuwa na hadhi ya kumjibu ni Dr Mwakyembe labda kidogo kafulila.

Shida kubwa hoja alizoziibua ni cross cutting issue za utekwaji. Kuuwawa na worst case scenario hii move ya Kina Agather. Mwangi. KARUA. isinge solviwa kwa mabavu. Maana ule uongo wote umejulikana duniani.

Gwajima sio mtu wa kujibiwa ni wa kumyamaziwa ila hoja zake zimeeleweka sana.
 
Ngoja siku atekwe shemeji yako anayekuweka mjini au yule dada yako unayempenda sana ndo utaona umuhimu wa aliyoongea Gwajima. Kabla ya hapo sikuwa najua kama Tanzania Ina WAPUMBAVU kiasi hiki. Ila nadhani ni njaa iliyojaa mpaka kwenye ubongo.
 
Alidhani kwamba ataweza kuwalaghai Watanzania wote.
Lakini watu wapo makini.
Lakini katika mkutano wa Chama kesho asiruhusiwe tena kuongea maneno yake ya uongo.
Awepo kama observer tu.
Yeye ameshaongea,amesikilizwa.
Kwa hiyo nawe unasapoti unafiki?

Madini ya thamani aliyoyatema wee kwako ni magalasa?

Mngelikua mnaandika mada baada ya kufanya utafiti kwanza kwenye mitandao kuona namna upepo wa waTz unavyovuma kumuunga mkono Gwajiboy, wala msingelithubutu kuleta pumba zenu kwenye kadamnasi, maana mnaonekana ni vioja!

Kila kitu kakiweka wazi, anayeleta madhila kwa waTz keshajulikana kwa jina, usiendelee kuupotosha umma, hawatakuelewa.

Moto aliouwasha Gwajiboy, kamwe hamuwezi kuuzima kwa hoja nyepesi namna hii, tafuteni hoja zenye mantiki, maana kila anayejifaragua kumjibu anaonekana ni chawa asiye na hoja.

'Press' ya Gwajiboy imekuwa ni spray aliyoipuliza ghafla bila kutarajia, makunguni na machawa yote hata ambayo hatukuyaelewa, yametoka hadharani kwa kuchanganyikiwa.
 
Alidhani kwamba ataweza kuwalaghai Watanzania wote.
Lakini watu wapo makini.
Lakini katika mkutano wa Chama kesho asiruhusiwe tena kuongea maneno yake ya uongo.
Awepo kama observer tu.
Yeye ameshaongea,amesikilizwa.
Uchawa wa uzeeni mbaya sana,au kwa vile hata baba yako naye aliwapoteza akina Khasim Hanga.
 
Alidhani kwamba ataweza kuwalaghai Watanzania wote.
Lakini watu wapo makini.
Lakini katika mkutano wa Chama kesho asiruhusiwe tena kuongea maneno yake ya uongo.
Awepo kama observer tu.
Yeye ameshaongea,amesikilizwa.
Wachache wenye akili zao wamemuelewa, Ila wenye akili za kushikiwa itawachukuwa mda mrefu kumwelewa.
 
Back
Top Bottom