Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimekuwa nikifuatilia hilo linaloitwa kongamano la kuiombea amani nchi yetu na kumpongeza Rais wetu Samia Suluhu Hassan, linalofanyika jijini Mbeya, hivi leo.
Lakini cha kushangaza ni kila kiongozi wa dini, anayekuja hapo mbele, kusisitiza Taifa letu liendelee kudumisha amani nchini, bila kusisitiza watawala wetu pia kuongoza nchi hii kwa kutumia HAKI, kwa kuwa inajulikana wazi kuwa HAKI na AMANI ni pacha.
Hata kwenye maandiko ya Biblia, Katika kitabu cha Mithali, 14:34 imeandikwa hivi nikinukuu "Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.
Hivi hawa viongozi wa dini, hawayaoni hayo maandiko muhimu sana yaliyoandikwa Katika kitabu hicho cha Mungu na kutakiwa kuyasisitiza?