Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Askofu Mkuu Jimbo la Dar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania, Juda Thadeus Ruwa'ichi anatoa tamko sasa hivi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Katika mkutano na Wanahabari unafanyika kwenye viunga vya 'Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji mpya Relini.
Askofu Ruwa'ichi ametaja baadhi ya mauaji ya wanasiasa na raia yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na yale yaliyotokea Novemba 26, 2024 huko Tunduma mkoani Songwe na Manyoni mkoani Singida sambamba na mauaji yaliyotokea jijini Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu, ambayo Kanisa hilo limetaja mauaji hayo yote kuwa ni ya kukusudia
"Mwanzoni mwa mwezi huu (Novemba 2024) kule Iringa na Bukoba waliuawa pia wanasiasa wawili (2), Tanzania tunaelekea wapi kwa kujenga tabia hii?, kitendo cha mauaji ya wanasiasa kinapaswa kulaaniwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hakuna mwenye mamlaka ya kumuuwa mwenzake, kutekeleza ama kudai haki za kisiasa wakati wa uchaguzi wakati wa uchaguzi sio vita ni ushindani"
Aidha, Kanisa Katoliki limesema tabia ya kuchukulia mauaji ya wanasiasa na raia kama vifo vya kawaida na vinavyopaswa kuzoeleka ni tendo baya sana linaloweza kupelekea kujengeka tabia ya kupoteza na kukosa ulinzi wa haki ya uhai kama ilivyo kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"Wapo waliokabidhiwa jukumu la kulinda Ibara hii, tunapoona mauaji haya yakiongezeka tunajiuliza maswali mengi juu ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi"
Kuhusu mweendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa liofanyika Novemba 27
"Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana maeneo mbalimbali ya nchi yetu inaonekana kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa umegubikwa na mapungufu mengi, ambayo wengi ninyi kama wanahabari mnayajua. Shughuli zito kama hii ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inapoenda kiholela hatuipendi nchi yetu, hatuwatendei raia haki na hatushughulikii raia wote".
"Viongozi mbalimbali wa dini walitoa matamko kuhusu mwenendo wa maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matamko yale yalikuwa ni tahadhali tufanye hilo zoezi kwa hali inayokidhi. Ni zoezi (niliite takatifu) katika nchi yoyote, Uchaguzi halali na haki ni zoezi takatifu la kiraia, kwahiyo ni lazima lifanywe kwa uzito, uangalifu na uadilifu unaotakiwa"
"Nchi yetu ni ya Siasa ya vyama vingi, hata kama tunaweza kuelekea kuwa na ulemavu wakujihisi kwamba ni nchi ya chama kimoja lakini Tanzania ni nchi ya Vyama vingini na raia Mtanzania kuwa mshiriki wa chama chochote hiyo ni haki yake kiraia hakuna raia yoyote ambaye amezaliwa nakufungamanishwa na CCM, CHADEMA au CUF na vingine, hivyo vyama vyote ni machaguo au maamuzi ya raia mwenyewe na raia anapoamua kwamba anataka kujihusisha anapaswa kuheshimiwa. Watanzania tuendelee kujenga utayari wakuithamini nchi yetu, kuipigania nchi yetu na kupendana, kushikamana na kutendeana haki"
Tumetamka mara kadhaa kwamba inabidi tujipange, tujipange kutazama nyanja mbalimbali zinazohitaji maboresho au marekebisho katika mwenendo wa siasa za nchi yetu, hilo sio haki ya Wanasiasa ni haki ya raia wote kuwa na mpangilio na mwelekeo wa kisiasa ambao unatendea haki na unalinda usitawi na unapania maendeleo ya nchi yetu. Mtu yeyote mwenye nia njema na nchi yetu hawezi acha kulipigia kelele hili na yeyote anayeona tamko kama hili linawameng'enya ni vizuri wakajitadhimini.