Wakuu,
Askofu Mkuu Jimbo la Dar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania, Juda Thadeus Ruwa'ichi anatoa tamko sasa hivi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Katika mkutano na Wanahabari unafanyika kwenye viunga vya 'Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji mpya Relini.
Askofu Ruwa'ichi ametaja baadhi ya mauaji ya wanasiasa na raia yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na yale yaliyotokea Novemba 26, 2024 huko
Tunduma mkoani Songwe na
Manyoni mkoani Singida sambamba na mauaji yaliyotokea jijini Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu, ambayo Kanisa hilo limetaja mauaji hayo yote kuwa ni ya kukusudia
"Mwanzoni mwa mwezi huu (Novemba 2024) kule Iringa na Bukoba waliuawa pia wanasiasa wawili (2), Tanzania tunaelekea wapi kwa kujenga tabia hii?, kitendo cha mauaji ya wanasiasa kinapaswa kulaaniwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hakuna mwenye mamlaka ya kumuuwa mwenzake, kutekeleza ama kudai haki za kisiasa wakati wa uchaguzi wakati wa uchaguzi sio vita ni ushindani"
Aidha, Kanisa Katoliki limesema tabia ya kuchukulia mauaji ya wanasiasa na raia kama vifo vya kawaida na vinavyopaswa kuzoeleka ni tendo baya sana linaloweza kupelekea kujengeka tabia ya kupoteza na kukosa ulinzi wa haki ya uhai kama ilivyo kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"Wapo waliokabidhiwa jukumu la kulinda Ibara hii, tunapoona mauaji haya yakiongezeka tunajiuliza maswali mengi juu ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi"