LGE2024 Askofu Juda Ruwa'ichi atoa tamko kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

LGE2024 Askofu Juda Ruwa'ichi atoa tamko kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
..umechanganya madawa.

..kilichotokea Rwanda ni Kanisa kufungamana na Serikali, na Interahamwe [ umoja wa vijana wa chama tawala] wakati wa mauaji ya kimbari.

..Kanisa lingesimama upande wa haki mauaji yale yangeweza kuepukwa, au Kanisa lisingechafuka na kulaumiwa.

..Maaskofu na viongozi wote wa Dini wa Tanzania wanapaswa kupata sauti pale wanapoona kuna mmomonyoko wa haki ktk jamii.
Sahihi kabisa watu wanauliwa kama kuku kisa uchaguzi
 
Halafu sijui ana mapengo, ila ni mchaga, wanachadema wengi wanatokea huko. Kitima yeye anamuunga mkono msingida mwenzake. Wakatoliki wakiona Rais muislamu wanakuwaga na midomo mirefu
 
Kama Serikali haitaingilia kati na kuwashughulikia Hawa viongozi uchwara wa dini nchi itaingia kwenye machafuko muda sio mrefu. Huko Rwanda hawa Maaskofu wa Kikatoliki walihusika sana kwenye kuchochea na kisabisha Genocide. Serikali iwe makini!!!
Amka kumekucha, usije ukakojoa kitandani. Nawa au oga uende shule. Mia tano ya maandazi ipo hapo mezani. Uwe makini unapovuka barabara sawa?
 
Naunga mkono tamko la Baba Askofu Juda Thadeus Ruwa'ichi ila halikupaswa kuharakishwa haraka hivi!,tamko lingesubiri matokeo ya uchaguzi yatangazwe rasmi,ili tamko pia lihusishe comments kuhusu uchaguzi na kuwapongeza the majority winners as well as the minority winners.

Niliwahi kuuliza,kwanini kila rais wa Tanzania anapokuwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?,sikuwahi kujibiwa,kuna baadhi wakasema inatokea tuu by a coincidence!,sasa kipindi nchi ikiwa chini ya Mkatoliki,TEC,hawawi wakali sana kama nchi ikiwa chini ya wa upande wa pili!。

Pia nipongeze tamko hili limetolewa kwenye press conference,na sio mimbarini ili kuepuka kuchanganya dini na siasa。Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?
P
Kwani walipokuwa wanamkemea Magufuli alikuwa KKKT ?
 
Wakuu,

Askofu Mkuu Jimbo la Dar na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania, Juda Thadeus Ruwa'ichi anatoa tamko sasa hivi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, Katika mkutano na Wanahabari unafanyika kwenye viunga vya 'Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji mpya Relini.

Askofu Ruwa'ichi ametaja baadhi ya mauaji ya wanasiasa na raia yaliyotokea hivi karibuni kuwa ni pamoja na yale yaliyotokea Novemba 26, 2024 huko Tunduma mkoani Songwe na Manyoni mkoani Singida sambamba na mauaji yaliyotokea jijini Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu, ambayo Kanisa hilo limetaja mauaji hayo yote kuwa ni ya kukusudia

"Mwanzoni mwa mwezi huu (Novemba 2024) kule Iringa na Bukoba waliuawa pia wanasiasa wawili (2), Tanzania tunaelekea wapi kwa kujenga tabia hii?, kitendo cha mauaji ya wanasiasa kinapaswa kulaaniwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria, hakuna mwenye mamlaka ya kumuuwa mwenzake, kutekeleza ama kudai haki za kisiasa wakati wa uchaguzi wakati wa uchaguzi sio vita ni ushindani"

Aidha, Kanisa Katoliki limesema tabia ya kuchukulia mauaji ya wanasiasa na raia kama vifo vya kawaida na vinavyopaswa kuzoeleka ni tendo baya sana linaloweza kupelekea kujengeka tabia ya kupoteza na kukosa ulinzi wa haki ya uhai kama ilivyo kwenye Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

"Wapo waliokabidhiwa jukumu la kulinda Ibara hii, tunapoona mauaji haya yakiongezeka tunajiuliza maswali mengi juu ya uwajibikaji wa serikali kwa wananchi"

Kuhusu mweendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa liofanyika Novemba 27

"Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana maeneo mbalimbali ya nchi yetu inaonekana kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa umegubikwa na mapungufu mengi, ambayo wengi ninyi kama wanahabari mnayajua. Shughuli zito kama hii ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa inapoenda kiholela hatuipendi nchi yetu, hatuwatendei raia haki na hatushughulikii raia wote".

"Viongozi mbalimbali wa dini walitoa matamko kuhusu mwenendo wa maandalizi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, matamko yale yalikuwa ni tahadhali tufanye hilo zoezi kwa hali inayokidhi. Ni zoezi (niliite takatifu) katika nchi yoyote, Uchaguzi halali na haki ni zoezi takatifu la kiraia, kwahiyo ni lazima lifanywe kwa uzito, uangalifu na uadilifu unaotakiwa"

"Nchi yetu ni ya Siasa ya vyama vingi, hata kama tunaweza kuelekea kuwa na ulemavu wakujihisi kwamba ni nchi ya chama kimoja lakini Tanzania ni nchi ya Vyama vingini na raia Mtanzania kuwa mshiriki wa chama chochote hiyo ni haki yake kiraia hakuna raia yoyote ambaye amezaliwa nakufungamanishwa na CCM, CHADEMA au CUF na vingine, hivyo vyama vyote ni machaguo au maamuzi ya raia mwenyewe na raia anapoamua kwamba anataka kujihusisha anapaswa kuheshimiwa. Watanzania tuendelee kujenga utayari wakuithamini nchi yetu, kuipigania nchi yetu na kupendana, kushikamana na kutendeana haki"

Tumetamka mara kadhaa kwamba inabidi tujipange, tujipange kutazama nyanja mbalimbali zinazohitaji maboresho au marekebisho katika mwenendo wa siasa za nchi yetu, hilo sio haki ya Wanasiasa ni haki ya raia wote kuwa na mpangilio na mwelekeo wa kisiasa ambao unatendea haki na unalinda usitawi na unapania maendeleo ya nchi yetu. Mtu yeyote mwenye nia njema na nchi yetu hawezi acha kulipigia kelele hili na yeyote anayeona tamko kama hili linawameng'enya ni vizuri wakajitadhimini.

Cc Lucas Mwashambwa
 
Kama Serikali haitaingilia kati na kuwashughulikia Hawa viongozi uchwara wa dini nchi itaingia kwenye machafuko muda sio mrefu. Huko Rwanda hawa Maaskofu wa Kikatoliki walihusika sana kwenye kuchochea na kisabisha Genocide. Serikali iwe makini!!!
Kwahiyo mkielezwa ukweli mnageukia kuwashughulikia watu! Halafu unalinganisha yanayoendelea Tanzania na Rwanda genocide vitu viwili tofauti! Kwamba yaliyotokea kwenye mchakato wa uchaguzi Ndio yanayofaa kuigwa na jamii ikiyostaarabika kabisa. Kwamba mnauwa watu halafu viongozi wa dini wawe kazi Yao ni kuzika na kutokemea mauaji. Mpumbavu wewe.
 
Anawashwa na nini mwambieni atulize makalio, km vp avue joho aanzishe chama au ajiunge na chagadema SACCOSS ya nyumbani. Shida ya hao wanafiki ni Rais kuwa muislam. Tanzania siyo Vatican hao ni wapumbavu. Ruwaichi ni mbaguzi sana anajulikana, ni mkabila na ni mdini.
Hakuna shule ya ujinga sijui hii masters ya upumbavu uliisomea wapi. Hata huyo Rais anaona kabisa alipokosea
 
Hao mashetani wana unabii gani, wametubu wapi dhambi ya kuwaangamiza wanyarwanda.
Utakua umehama kutoka Facebook ukaja jukwaa hili kuchafua Hali ya hewa Kwa maslahi ya watawala ambao Mikono Yako Ina damu za watu wasio na hatia
 
Naunga mkono tamko la Baba Askofu Juda Thadeus Ruwa'ichi ila halikupaswa kuharakishwa haraka hivi!,tamko lingesubiri matokeo ya uchaguzi yatangazwe rasmi,ili tamko pia lihusishe comments kuhusu uchaguzi na kuwapongeza the majority winners as well as the minority winners.

Niliwahi kuuliza,kwanini kila rais wa Tanzania anapokuwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?,sikuwahi kujibiwa,kuna baadhi wakasema inatokea tuu by a coincidence!,sasa kipindi nchi ikiwa chini ya Mkatoliki,TEC,hawawi wakali sana kama nchi ikiwa chini ya wa upande wa pili!。

Pia nipongeze tamko hili limetolewa kwenye press conference,na sio mimbarini ili kuepuka kuchanganya dini na siasa。Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?
P
Neither right NOR Left doctrine rules
 
Kemea kemea hii isipoheshimiwa kwa serikali ya CCM kutubu na kujisahihisha kujiondoa katika hali ya ukiburi, kuna mambo mazito yanaweza kushamiri.

Kemea kemea ni tamko la kinabii, lifanyiwe kazi wenye mamlaka wawe wasikivu ama sivyo raia watawaadhibu
Kwa sasa roho wa uongo, uovu na kiburi cha madaraka kimewapofusha ccm. Maaskofu wametoa hili tamko, litakuwa ni rejea ya unabii wao kwa kile kitakachotokea huko mbeleni.
 
Wewe ni kama farisayo ama sadukayo tu wa kale, hivyo haishangazi. Unachojali ni tumbo lako tu basi, haki ya wengine hapana. Endelea hivyo waache wanaojali waseme.
haki yako ni nguvu zako,

uvivu tu unakutia wivu, kaza kiuno hicho mwanaume.

ng'we ng'we ng'we za nini kama zuzu na huna pwainti!!alaaah!🐒
 
2020 huyo mnafiki alikuwa bado hajazaliwa? Magu alivyokuwa anaua alijitokeza kusema lolote? Hao maaskofu wote ni km Policap Pengo, hawaonagi hata aibu. Huwa nawadharau sana, wanajaribu kuleta uchochezi kwa kuokoteza vitakataka.
Kama kuna taasisi ilikemea uovu wa magu ni hiyo RC. Usidhani hatukuona matamko yao wakati wa yule kiongozi muovu. Hilo tamko la maaskofu ni baadhi tu ya viashiria vya mwisho wa ccm. Kwasababu ccm wanafaidika na huu udhaifu wa katiba, ni lazima wamchukie kila anayeweka uhalifu wao hadharani. Maaakofu wameweka msimamo wao hadharani, wakati wa mahesabu mikono yao itakuwa safi.
 
Wewe kichaa, si bure. Ni wananchi gani waliamua kuwaua wagombea au viongozi wa CHADEMA? Hayo mmeyafanya ninyi mashetani, halafu kwa uwendawazimu mkubwa, mnasema ni maamyzi ya wananchi!!
wagombeaji uongozi wa chadema hawakua na sifa wala vigezo vya uongozi kikatiba.

kuenguliwa ilikua ndiyo haki na stahiki yao ya msingi kabisa.

Lazima muwe wastaarabu na wangwana kukubali matokeo ndrugu zango 🐒
 
Kama Serikali haitaingilia kati na kuwashughulikia Hawa viongozi uchwara wa dini nchi itaingia kwenye machafuko muda sio mrefu. Huko Rwanda hawa Maaskofu wa Kikatoliki walihusika sana kwenye kuchochea na kisabisha Genocide. Serikali iwe makini!!!
Kama ni machafuko yataletwa na ccm ndani ya nchi hii, hao maaskofu ni wajumbe tu. Uovu wote unafanywa na ccm ndani ya nchi hii kwa kushirikiana na vyombo vya usalama. Ifahamike ccm imefikia mwisho, hakuna uwezekano wa kuendelea kudanganya tena wananchi, zama zenu zimefikia mwisho.
 
Naunga mkono tamko la Baba Askofu Juda Thadeus Ruwa'ichi ila halikupaswa kuharakishwa haraka hivi!,tamko lingesubiri matokeo ya uchaguzi yatangazwe rasmi,ili tamko pia lihusishe comments kuhusu uchaguzi na kuwapongeza the majority winners as well as the minority winners.

Niliwahi kuuliza,kwanini kila rais wa Tanzania anapokuwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?,sikuwahi kujibiwa,kuna baadhi wakasema inatokea tuu by a coincidence!,sasa kipindi nchi ikiwa chini ya Mkatoliki,TEC,hawawi wakali sana kama nchi ikiwa chini ya wa upande wa pili!。

Pia nipongeze tamko hili limetolewa kwenye press conference,na sio mimbarini ili kuepuka kuchanganya dini na siasa。Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?
P
Supu nzuri ikiwa ya moto, bora wao wamejitokeza kusema siku zote, wakati wa zoezi la kujiandikisha, walijitokeza kuhamasisha wananchi wajitokeze kupiga kura, na sasa wanatoa tathmini ya uchaguzi.

Matokeo tuliyajua kabla, ila tuliamini watawala wangekubali kufuata utaratibu kama walivyo ahidi, na hawakufuata hivyo, hakuna haja kusubiri matokeo tunayoyafahamu.

HUkusikia vyama vile vinavyounga mkono ccm, vimeshasema uchaguzi, ulienda vizuri, na ulikuwa huru na haki? Wao vipi hawakupaswa kusubiri?
 
Back
Top Bottom