Askofu Jude Ruwa'ichi: Nchi yetu sasa hivi haisimami kwenye misingi ya uadilifu. Katika mengi tunaenda ovyo

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

"Nchi yetu sasa hivi haisimami kwenye misingi ya uadilifu. Katika mengi tunaenda ovyo.

Ubinafsi umeshamiri, ufujaji umeshamiri. Na karibu misingi yote ya maadili hakuna anayeihangaikia tena. Ni kweli kanisa linatambua kwamba tunapaswa kutembea katika misingi ya uadilifu na kanisa linahubiri na kufundisha uadilifu, fadhila tunu zilizo bora, tunu za kiutu, tunu za kikristo, tunu za kibinadamu kwa ujumla.

Lakini nachelea kusema kanisa linalopambana kukuza hizi tunu ni kama linakabili upepo kinzani ambao hauzijali wala kuzithamini tunu hizo.

Kwa bahati mbaya taifa lolote ambalo linataka kutozingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, ni taifa ambalo linajichimbia mwina.

Mwalimu kutangazwa mwenye heri unaendelea. Kwa sasa wale tuliowakabidhi jukumu wanawainterview watu. Mtu yeyote ambaye anatambua kwamba anachakuchangia kuhusu mchakato wa Mwalimu anakaribishwa akaonane na wale wanaoshughulikia huo mchakato atoe maelezo yake."

Hayo yamesema na Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar, Jude Ruwa'ichi
 
Hata hayo makanisa ya tecdema hayafuati maadili

Tazama watawa wanavyoishi ya dhiki na shida kuu, mapdri wa huku chini wanaishi maisha ya ajabu tena magumu na masongo wa mawazo hadi wengne wanaishi maisha ya kubeti...wakati huo maaskofu uchwara akiwemo ruwaich mnaponda mali za kanisa bila huruma?

Tangu lini wenye madhambi wakawa na majukumu ya kutawaza watu kuwa watakatifu? Tazama kashfa za ngono makanisani mwenu, tazama unyanyasaji ulivyojaa madhabahuni kwenu...

MMEKOSA KUWA WAPATANISHI, BADALA YAKE MMEKUWA WACHONGANISHI TENA MLIOSHIKWA NA MARUHANI.
 
Umekosa cha kuandika hiyo mihemko yako peleka lumumba kwa kijani wenzako.huna hata aibu kuandika hiyo rubish.
 
"Nchi yetu sasa hivi haisimami kwenye misingi ya uadilifu. Katika mengi tunaenda ovyo.

Ubinafsi umeshamiri, ufujaji umeshamiri. Na karibu misingi yote ya maadili hakuna anayeihangaikia tena. Ni kweli kanisa linatambua kwamba tunapaswa kutembea katika misingi ya uadilifu na kanisa linahubiri na kufundisha uadilifu, fadhila tunu zilizo bora, tunu za kiutu, tunu za kikristo, tunu za kibinadamu kwa ujumla.

Lakini nachelea kusema kanisa linalopambana kukuza hizi tunu ni kama linakabili upepo kinzani ambao hauzijali wala kuzithamini tunu hizo.

Kwa bahati mbaya taifa lolote ambalo linataka kutozingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, ni taifa ambalo linajichimbia mwina.

Mwalimu kutangazwa mwenye heri unaendelea. Kwa sasa wale tuliowakabidhi jukumu wanawainterview watu. Mtu yeyote ambaye anatambua kwamba anachakuchangia kuhusu mchakato wa Mwalimu anakaribishwa akaonane na wale wanaoshughulikia huo mchakato atoe maelezo yake."

Hayo yamesema na Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar, Jude Ruwa'ichi
Askofu Ruwaichi yuko sahihi 100%,
maadili nchini yameshuka kidogo,
watu hawaheshimu hata viapo na nadhiri zao kwa Mungu.

leo hii unakuta watawa wakike na wa kiume wanafanya mambo yakushangaza mpaka unaona aibu wewe mlei,
Na hakuna wa kukemea hilo kwasababu hata ndani ya kanisa lenyewe wote wanashiriki uchafu na fedheha hizo za kimaadili na kukimbilia madhabauhuni kuungama. Ulevi, ngono na ufuska njenje miongoni mwa watawa kwa watawa, lakini watawa kwa waamini n.k. Haijulikani kimebadilika nini ndani ya kanisa. Hakuna tena kizuri cha kuiga ndani ya kanisa, ni uchafu mtupu ni kubugia tu masakramenti kama kiporo vile. hakuna tena heshika kwa ekaristi takatifu.

hata mivurugano ya ndoa nyingi humu nchini hususani za kikatoliki,
chimbuko la mafarakano na kusambaratika kwa familia hizo ni watawa kukosa maadili na kuingilia familia za walei mpaka ndani kabisa na kuwajibika kama baba wa ndoa kenye familia za wenyewe.

Na hata ukifuatilia kwa karibu hivi sasa kuhusu watovu wengi wa kimaadili humu nchini,
ambao ndio wanahusika na ufisadi, wizi na ujambazi, uchochezi na ghasia na hata mauaji utagundua wengi ni wakristo hasa wakatoliki. Na hapa, utagundua chimbuko la yote haya ni kanisa kuvurugika na kushindwa kusimamia maadili yake na waamini wake.

Na ndio maana,
kwa maoni yangu,
napendekeza kama taifa, kuketi chini, kujitathimini, kujirekebisha na kujisahihihisha na hatimae kuja na majawabu muafaka ya kunusuru mila, desturi na utamaduni wa kuishi na kufanya kazi kwa maadili wa waTanzania wote :NoGodNo:
 
Tazama watawa wanavyoishi ya dhiki na shida kuu, mapdri wa huku chini wanaishi maisha ya ajabu tena magumu na masongo wa mawazo hadi wengne wanaishi maisha ya kubeti...wakati huo maaskofu uchwara akiwemo ruwaich mnaponda mali za kanisa bila huruma?
Mjomba haulijui kanisa katoliki.
Hakuna mtawa au Padre yeyote anaye ishi maisha ya dhiki na shida kuu.
Huyo anayeishi hivyo itakuwa kwa sababu zake binafsi au kwa mahamuzi yake. Labda ana nadhiri ya umasikini.
 
Hoja ni hii
Ubinafsi umeshamiri, ufujaji umeshamiri. Na karibu misingi yote ya maadili hakuna anayeihangaikia tena.
Ufafanuzi wa hoja ni huu
Ni kweli kanisa linatambua kwamba tunapaswa kutembea katika misingi ya uadilifu na kanisa linahubiri na kufundisha uadilifu, fadhila tunu zilizo bora, tunu za kiutu, tunu za kikristo, tunu za kibinadamu kwa ujumla.
Mchango wa kanisa ktk kuisaidia serikali kuongoza bila ukinzani wa wananchi ni huu
Lakini nachelea kusema kanisa linalopambana kukuza hizi tunu ni kama linakabili upepo kinzani ambao hauzijali wala kuzithamini tunu hizo.
Askofu analalamika kazi wanayoifanya inakuwa bure sababu uadilifu hamna
Kwa bahati mbaya taifa lolote ambalo linataka kutozingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, ni taifa ambalo linajichimbia mwina.
Askofu anaonya
 
Mjomba haulijui kanisa katoliki.
Hakuna mtawa au Padre yeyote anaye ishi maisha ya dhiki na shida kuu.
Huyo anayeishi hivyo itakuwa kwa sababu zake binafsi au kwa mahamuzi yake. Labda ana nadhiri ya umasikini.
Hli dhehebu la rc tunalijua sana, tunaishi nao, wengne ni ndugu...na isitoshe rc haipo sayari nyingne na si special eti labda wamejificha..

Watawa na mapadri wana maisha magumu kuliko kawaida...

Na mbaya zaidi wanawatumia kuzalisha mali katika mashirika yao ya kitawa lakin returns zao ni fedheha.
 
Askofu Ruwaichi yuko sahihi 100%,
maadili nchini yameshuka kidogo,
watu hawaheshimu hata viapo na nadhiri zao kwa Mungu.

leo hii unakuta watawa wakike na wa kiume wanafanya mambo yakushangaza mpaka unaona aibu wewe mlei,
Na hakuna wa kukemea hilo kwasababu hata ndani ya kanisa lenyewe wote wanashiriki uchafu na fedheha hizo za kimaadili na kukimbilia madhabauhuni kuungama. Ulevi, ngono na ufuska njenje miongoni mwa watawa kwa watawa, lakini watawa kwa waamini n.k. Haijulikani kimebadilika nini ndani ya kanisa. Hakuna tena kizuri cha kuiga ndani ya kanisa, ni uchafu mtupu ni kubugia tu masakramenti kama kiporo vile. hakuna tena heshika kwa ekaristi takatifu.

hata mivurugano ya ndoa nyingi humu nchini hususani za kikatoliki,
chimbuko la mafarakano na kusambaratika kwa familia hizo ni watawa kukosa maadili na kuingilia familia za walei mpaka ndani kabisa na kuwajibika kama baba wa ndoa kenye familia za wenyewe.

Na hata ukifuatilia kwa karibu hivi sasa kuhusu watovu wengi wa kimaadili humu nchini,
ambao ndio wanahusika na ufisadi, wizi na ujambazi, uchochezi na ghasia na hata mauaji utagundua wengi ni wakristo hasa wakatoliki. Na hapa, utagundua chimbuko la yote haya ni kanisa kuvurugika na kushindwa kusimamia maadili yake na waamini wake.

Na ndio maana,
kwa maoni yangu,
napendekeza kama taifa, kuketi chini, kujitathimini, kujirekebisha na kujisahihihisha na hatimae kuja na majawabu muafaka ya kunusuru mila, desturi na utamaduni wa kuishi na kufanya kazi kwa maadili wa waTanzania wote :NoGodNo:
Haya uliyoandika umeyafanyia utafiti au ni utashi wako.una uhakika wezi,watekaji,mafisadi ni wakatoliki?mbona hakuna tajiri mkatoliki au unaugonvi na ukatoliki!kuna askofu mkatoliki ni tajiri? Una uhakika ndoa zinazovurugika hapa nchini ni wakatoliki.weka takwimu basi au majina ya wakatoliki mafisadi ili tuende kwa hoja.hata uuchukie vipi ukatoliki utaendelea kushamiri tu.mimi ni mwamba na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.
 
"Nchi yetu sasa hivi haisimami kwenye misingi ya uadilifu. Katika mengi tunaenda ovyo.

Ubinafsi umeshamiri, ufujaji umeshamiri. Na karibu misingi yote ya maadili hakuna anayeihangaikia tena. Ni kweli kanisa linatambua kwamba tunapaswa kutembea katika misingi ya uadilifu na kanisa linahubiri na kufundisha uadilifu, fadhila tunu zilizo bora, tunu za kiutu, tunu za kikristo, tunu za kibinadamu kwa ujumla.

Lakini nachelea kusema kanisa linalopambana kukuza hizi tunu ni kama linakabili upepo kinzani ambao hauzijali wala kuzithamini tunu hizo.

Kwa bahati mbaya taifa lolote ambalo linataka kutozingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, ni taifa ambalo linajichimbia mwina.

Mwalimu kutangazwa mwenye heri unaendelea. Kwa sasa wale tuliowakabidhi jukumu wanawainterview watu. Mtu yeyote ambaye anatambua kwamba anachakuchangia kuhusu mchakato wa Mwalimu anakaribishwa akaonane na wale wanaoshughulikia huo mchakato atoe maelezo yake."

Hayo yamesema na Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar, Jude Ruwa'ichi
Naam,

Kibaya zaidi, hizi hoja ni rahisi sana kuzielekeza kwa watawala, wakubwa, wanasiasa, watu wenye nguvu.

Na pengine ni sawa, wao ndio viongozi, wao ndio wamepewa talanta kubwa na kwa hiyo watadaiwa zaidi, kwa kanuni ya "noblesse oblige" kama kwenye mfano wa Bwana Yesu (as in Lord Jesus, as in Lord Russell) kuhusu tajiri aliyewapa watu fulani pesa, wengine wakipewa nyingi, wengine wakipewa kidogo, wale waliopewa nyingi watadaiwa kurudisha nyingi pia.

Lakini, matatizo haya yapo kwenye jamii yote.

Ukiangakia rushwa, wananchi wa kawaida waneshaifanya rushwa kuwa kama sehemu ya maisha tu. Kabla hata mtu hajaombwa rushwa, yeye ndiye anaanza kutoa, kuoata haki yake.

Inakuwa rahisi kukaumu viongizi kwa juwa wao wanaonekana zaidi, wao wanakula kwa kamba ndefu zaidi, lakini matatizo haya yapo kwenye jamii nzima.

Na ukiangalia kuwa hata hao viongozi wanatoka katika jamii yetu, vijana wa keo wanachojifunza ni kwamba, ukioata cheo, umefikiwa na zamu yako ya kula rushwa. Na oengine wanakubaki mfumo wa rushwa keo wakati hawana cheo kwa kuamini kuwa kuna siku na wao wataoata cheo, zamu yao ya kula rushwa itafika.

Kwa hiyo, kuliangazia tatizo vizuri zaidi, tunatakiwa tuiangalie jamii nzima, si kuangalia matatizo ya uongozi tu.
 
Hata hayo makanisa ya tecdema hayafuati maadili
Huu mstari wa kwanza tu unakushtaki mwenyewe, kwamba chochote utakachoandika huko chini hakina thamani yoyote ya kupotezea muda.
Lakini ufahamu huo haukunizuia niendelee kusoma takataka zilizopo huko chini hadi nilipofikia mwisho kabisa:
MMEKOSA KUWA WAPATANISHI, BADALA YAKE MMEKUWA WACHONGANISHI TENA MLIOSHIKWA NA MARUHANI.
Kuna popote ulipowahi kuona au kusikia majambazi/waharifu wakapatanishwa na waliowafanyia ujambazi badala ya kuwapeleka gerezani wanakostahili kupelekwa?
 
Hata hayo makanisa ya tecdema hayafuati maadili

Tazama watawa wanavyoishi ya dhiki na shida kuu, mapdri wa huku chini wanaishi maisha ya ajabu tena magumu na masongo wa mawazo hadi wengne wanaishi maisha ya kubeti...wakati huo maaskofu uchwara akiwemo ruwaich mnaponda mali za kanisa bila huruma?

Tangu lini wenye madhambi wakawa na majukumu ya kutawaza watu kuwa watakatifu? Tazama kashfa za ngono makanisani mwenu, tazama unyanyasaji ulivyojaa madhabahuni kwenu...

MMEKOSA KUWA WAPATANISHI, BADALA YAKE MMEKUWA WACHONGANISHI TENA MLIOSHIKWA NA MARUHANI.
Nitajie shule za kiislamu,nitajie vyuo vya kiislamu ova
 
Huu mstari wa kwanza tu unakushtaki mwenyewe, kwamba chochote utakachoandika huko chini hakina thamani yoyote ya kupotezea muda.
Lakini ufahamu huo haukunizuia niendelee kusoma takataka zilizopo huko chini hadi nilipofikia mwisho kabisa:

Kuna popote ulipowahi kuona au kusikia majambazi/waharifu wakapatanishwa na waliowafanyia ujambazi badala ya kuwapeleka gerezani wanakostahili kupelekwa?
Na wewe umeandika takataka

Nazungumzia upatanishi wa KIMUNGU na si kimwili na mambo ya gereza...

tatzo lenu tecdema mnalitumia dhehebu la waroma kwa ajili ya mahitaji yenu ya kimwili ikiwemo uchonganishi na vurugu badala ya kulitumia kwa ajili ya misingi ya kiroho.

uwe hai....(yesu yu hai)
 
Back
Top Bottom