Majira ya saa 11.45 jioni ya leo, mfanyakazi mmoja wa TRA amewasilisha barua katika ofisi ya mapokezi ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lililoko barabara ya Sam Nujoma, Dar-Es-Salaam.
Ingawa mtu aliyekuwa mapokezi hakuwa tayari kuzungumzia barua hiyo, kwa kuwa yeye siyo Msemaji wa Kanisa, hata hivyo, uchunguzi umethibitisha kwamba barua hiyo imemtaka Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zachary Kakobe, kufika tena kwa mahojiano TRA Mwenge, kesho Jumatano 24.1.2018, saa 4 kamili asubuhi.
Jumatatu iliyopita 15.1.18, Askofu Kakobe alihojiwa kwa mara ya kwanza katika ofisi hizo, na baada ya kuhojiwa, alitolewa kwa mlango wa nyuma kwa gari nyingine, na kuwaacha solemba waandishi wa habari, waliokuwa mbele ya ofisi hizo, kusaka habari.
Mahojiano haya mapya yanaibuka tena, baada ya taarifa za ndani kueleza kwamba, mahojiano hayo yalikuwa yamefika tamati.