Mkuu unachoongelea ni tofauti na tahadhari niliyoitoa.
1. Kwenye BLUU. Kimsingi unakubaliana na mimi kuwa Kakobe ni mtu mdogo sana, thats right! Tatizo lipo ni je kama ni mtu wa kuonge upupu huoni serikali ina wekeza miguvu mingi sana kwa non-issues zake? Nakuhakikishia serikali ingekaa kimya ikaacha apite na huo upupu wake hiyo wala isingekuwa news kwenye media for 2 days.
2. Kwenye RED. Hayo mambo nimeyaelezea kwenye post yangu vizuri. Hayo ni mambo ya imani kati yake na wale anaowaongoza (nimeweka msisitizo kuwa mambo ya imani magumu sana). Wewe unaona kuwa anaongea upupu kama wewe, lakini je hao maelfu ya waumini wake wanaona hivyo? Kwangu mimi serikali ingeingilia pale tu anapovuka mipaka ya sheria za nchi, mfano mzuri ni uliotoa ni kuhusu issues zake na Tanesco lakini si vinginevyo.
3. Ugomvi wa sasa wa Kakobe unatokana na Serikali ya sasa kutopenda kukosolewa. Na wala si kwamba Kakobe ni wa kwanza kupata misukosuko ya aina hiyo kutoka kwa serikali hii. Wapo wengine wengi tu. Tatizo linapokuja unaponza kuzozana na Viongozi wa dini(Kumbuka issue ya Askofu wa kanisa katoliki kule Kagera kama sikosei) wanapokukosoa kwa kutumia Vyombo vya serikali kama Uhamiaji, Polisi, TRA e.t.c ina weka a very bad percedence.
4. Nimeona hapo juu una sema quote "Hakuna Nchi Duniani inayoruhusu Rais wake kunenewa vibaya. Unajua kilichomkuta Diego Maradona kwa Rais Trump?" end quote. Hiyo sio kweli hata kidogo. Hakuna rais duniani anayesemwa vibaya tena si tu na raia wa nchi yake bali hata wa nje kama wa Marekani. Leo hii kama Rais wetu angepokea hata 1/10 ya kejeli, mizaha, matusi e.t.c wanayopokea wanaokuwa marais wa Marekani, hii nchi ingekuwa ina waka moto sasa hivi, na magereza yasingetosha. Itoshe kusema tu kuwa rais/kiongozi wa mengi ya Mataifa yaliyoendelea inataka uwe na roho ngumu sana, freedom of speech kwenye nchi zao (compared to African countries and the like) tunaweza kusema ni Extended.