zaleo
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 1,902
- 765
Mzee six ni muhuni tu
Jamani mwacheni 6 ni mzee kanisa msasani. Pale anatafuta nkate tu, hali ikichafuka si atakimbilia kwa wakwe Zambia?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee six ni muhuni tu
Utake usitake Kakobe ni mhuni na Kama wewe ni mmoja wa waumini wake wote ni walewale.
Wala siyo askofu mganga wa jadi tu kama waganga wengine.
Kakobe ni mtumishi wa Mungu aliye hai, ahsante sana kwa ukweli huu mchungu na safari hii nikija dar itabidi nimwe muumini wa kanisa lake kabisa ili nichote maarifa.
Sitakaaa nimuamin huyu mchungaj kwan n mchonganishi sana na n mtu wa kuwagawa wananch ,ukiona mtu anatumia mwanvuli wa dini kuingia kwnye mambo ya siasa muogope kama ukoma kama sio kumpuuza
mwisho wake wa siasa umefika
Huyu mganga wa kienyeji naye anyamaze tu asitusumbue kabisa na madawa yake ya jadi.
unashangaa nini wakati watu wanakushangaa wewe unayelilia serikali tatu!CCM wanachezea sana Tanzania halafu nazidi kushangaa watu wanawashangilia
.................................................................................................................................................................Kabla ya mahubiri ya Neno la Mungu katika Ibada Kuu ya leo Jumapili 7.9.2014, Mwenge, Dar-Es-Salaam; Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zachary Kakobe, alianza kwanza kusoma kwa waumini wote Tamko zima la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Mchakato wa Katiba. Alisema kwamba Kanisa la FGBF linaunga mkono tamko hilo, siyo kwa asilimia 100%, bali kwa asilimia 200%. "Tamko hili limekuwa likisomwa katika Makanisa ya Katoliki, KKKT, na mengineyo kuanzia Jumapili iliyopita, na leo nitalisoma kwenu, neno kwa neno. Wakati umepita wa Wakristo kugawanywa, ili Shetani atawale. Tofauti zetu Wakristo tunaziweka pembeni, tunaunganishwa na msalaba. Jukwaa la Wakristo Tanzania linawaunganisha wote wanaoamini juu ya msalaba - TEC, CPCT, CCT na SDA. Hivyo kauli ya Jukwaa la Wakristo Tanzania, ni kauli ya FGBF, kwa sababu sisi tuko ndani ya CPCT."
Aliendelea kusema,"Kama tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania linavyosema, Rasimu ya Pili ya Katiba ni Waraka halali na rasmi, na ndiyo mawazo ya Watanzania. Katiba ni ya Wananchi na inahitaji maridhiano, na siyo ubabe. Huu ndiyo pia msimamo wa Kanisa la FGBF. Kinachoendelea sasa katika Bunge Maalum la Katiba, ni uhuni tu wa mchwa wanaotafuna fedha za Watanzania bila huruma kwa wananchi wasio na uwezo hata wa kununua dawa ya Malaria", alisema Askofu Kakobe. Baada ya kusoma tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, la Agosti 28, 2014, aliwauliza waumini,"Anayeunga mkono tamko hili asimame na kupunga mikono yake." Ndipo wote Kanisani maelfu kwa maelfu waliposimama na kupunga mikono yao huku wakishangilia. Kisha Kakobe akasema, "Pamoja na umuhimu wa maombi, haitoshi tu kuomba. Baada ya kufunga na kuomba, Esta alichukua hatua ya kumwambia ukweli Mfalme. Pamoja na maombi, hatua ya Jukwaa la Wakristo Tanzania kutoa sauti ya Kinabii kama hii, ni muhimu, ili mwenye masikio asikie."
Alimaliza kwa kusema,"Wapuuzeni watu wanaosema kwamba kufanya hivi ni kuchanganya dini na siasa! Katiba siyo siasa, ni zaidi ya siasa. Siasa imo ndani ya Katiba, lakini ndani ya Katiba kuna mambo mengi pia ambayo siyo siasa, kama vile Dini, Majeshi, Mahakama, Elimu, Kilimo, Ardhi, Ufugaji, Haki za binadamu n.k. Kwa ujasiri wote, kila Mkristo apaze sauti yake kukemea uhuni unaoendelea katika Bunge la Katiba, mpaka masikio ya walioko huko yazibuke!"
kwa sababu kasoma tamko lililotolewa na baraza la wakristo? Bado waislamu nao watatoa tamko lao kuhusu kuchakachuliwa kwa maoni yao na maccm hasa swala la kadhi. Jiandae kubeba majeneza ya magamba kisiasa wee choo sijui cha kikeKakobe ni askofu kanjanja.
Tunaomba upande wa pili na nyinyi pazeni sauti hawa mahahafidhina waumbuke!
Namwamini Zachary Kakobe.
Lakini kwa nini asifute na ile kauli aliyotoa mwaka 2005 kuwa Kikwete ni Mteule wa Mungu? Sasa Kakobe amefunguka macho. Alikuwa kipofu hapo awali.